Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 982
- 1,179
Nijuavyo mie, kazi ya Mchezaji Mpira (Professional player) ni kazi ya ajira kama ilivyo kazi nyingine.
Sasa, kwa ushamba wangu na kutokujua kwangu huwa nashangaa mambo haya:
- Mikataba haiwapi wachezaji uhuru wa kuvunja mikataba yao wakati wowote kama ilivyo kwa waajiriwa wengine. Mikataba inapokuwa flexible, inampa room mchezaji kutafuta fursa sehemu nyingine yoyote kwa muda apendao yeye kama ilivyo kwa ajira nyingine. Yaani kama ajira nyingine zinaruusu mwajiriwa kuacha kazi na kuajiriwa sehemu nyingine wakati wowte, iweje iwe ngumu kwa ajira ya Mpira? Hatuoni kuwa huu ni ukoloni?
-Hakuna kanuni za wazi za kubainisha kiasi gani mchezaji alipwe kama ilivyo kwa ajira nyingine. Mfano ukiwa Daktari, inafahamika kabisa kuwa range za mishahara ni kiasi flani. Kutofahamika bayana mishahara ya wachezaji hupelekea sintofahamu kati ya timu husika na mchezaji pengine kutofikia maelewano.
Mie kwa mawazo yangu kazi ya mpira ilitakiwa itangazwe kwenye public na wachezaji waweze ku-apply. Inteview yao inakuwa ni uwanjani kwa muda kadhaa. CV zao zioneshe wazi experience yake na mfano kama ni striker aseme amefunga magoli mangapi kwa muda gani kwa ligi ipi... Sio mambo kuwa gizani gizani kama shughuli za Mganga wa Jadi..
Kwa sasa naomba kuishia hapo. Nitaendelea kubainisha ukoloni wa mikataba ya wachezaji..