Kwa nini mpango wa kijani wa China ni muhimu kwa vita vya kimataifa vya kuenea kwa jangwa

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121


Hali ya jangwa imekuwa mojawapo ya changamoto kubwa zaidi za kimazingira zinazowakabili wanadamu, kwani inasababisha dhoruba nyingi za mchanga na vumbi, kuhatarisha usalama wa chakula, kufanya jamii zihame makazi yao na kuchochea migogoro.

Disemba mwaka jana wajumbe kutoka duniani kote walikutana kwenye kikao cha 16 cha Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa Jangwa ili kuingia makubaliano na kuharakisha hatua za pamoja za kusaidia usimamizi endelevu wa ardhi na kuhimili hali ya hewa.

Tangu mkataba huo usainiwe miaka 30 iliyopita, China imekuwa mchangiaji mkubwa zaidi wa maendeleo ya kijani duniani na mfano wa kimataifa wa kudhibiti kuenea kwa jangwa. China ina moja ya maeneo makubwa zaidi yaliyoathiriwa duniani, haswa katika maeneo ya kaskazini-magharibi, kaskazini na kaskazini mashariki ambayo yana sehemu kubwa ya ardhi kame na jangwa.

Moja ya miradi muhimu ya kiikolojia nchini ni Mpango wa Misitu Mitatu Inayolindwa ya Kaskazini (TNSFP). Tangu mwaka 1978, mradi huu umeongeza hekta milioni 32 za maeneo ya upandaji miti na kutibu hekta milioni 85.3 za uwanda wa nyasi ulioharibiwa na hekta milioni 33.3 za ardhi yenye jangwa.

Kupitia mpango huo, China pia imekuwa na msitu mkubwa zaidi duniani uliotengenezwa na binadamu huko Saihanba Mkoa wa Hebei, imekamilisha mradi mkubwa zaidi duniani wa kurejesha ikolojia huko Maowusu katika Mkoa wa Shaanxi, na kugeuza Jangwa la Kubuqi lililoko katika mkoa wa Mongolia ya Ndani kuwa ardhi ya kijani.

Naibu Katibu Mtendaji wa UNCCD Andrea Meza Murillo, amesema katika mchakato huu wa kuondoa jangwa, amevutiwa na picha za vizazi tofauti vya watu wa China wakipambana na kuenea kwa jangwa pamoja na uongozi wa China. Amepongeza dhamira ya muda mrefu ya taifa hilo na mbinu bunifu ya kupambana na kuenea kwa jangwa.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Ukuta Mkuu wa Kijani nchini Mauritania, Sidna Ahmed Ely, alisema nchi yake yenye asilimia 84 ya ardhi yenye jangwa, imetiwa moyo na kupata nguvu na azma kutoka "Ukuta Mkuu wa kijani wa China."

Teknolojia mpya ambazo China imetumia katika kudhibiti kuenea kwa jangwa zilionyeshwa kwenye Banda la China kwenye maonesho yaliyofanyika sambamba na mikutano ya kilele, mazungumzo ya mawaziri, utunukaji ya tuzo, na siku za kaulimbiu wakati wa mkutano wa COP16.

Wageni walivutiwa na kielelezo cha roboti cha upandaji miti cha AI kilicholetwa na kampuni ya “Eason Intelligent Equipment ya Beijing Co., Ltd”. Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Bian Lijun alisema kwa kutumia mfumo wa AI wa uongozaji satelaiti wa BeiDou na nishati ya kijani, roboti zinaweza kupunguza gharama za upandaji miti kwa asilimia 20 mpaka 25, kuongeza viwango vya upandaji kwa asilimia 10 mpaka 20, na zina ufanisi zaidi ya mara tano kuliko njia za mikono.

Baada ya kujua kuwa roboti zinaweza kupanda miti kwa sekunde 20 hadi 30 zikiwa mbali, Msaidizi wa Usimamizi wa Kituo cha Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, Majed Al-Mebairik, alionesha kuvutiwa sana.

Licha ya kukabiliwa na changamoto kali zaidi duniani za kuenea kwa jangwa, China imechukua njia ya kipekee inayounganisha kurejesha ikolojia na kuboresha maisha, ikiendeshwa na sera za ngazi ya juu, sheria na uvumbuzi wa teknolojia.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi, asilimia 53 ya ardhi ya jangwa inayoweza kutibika ya China imerejeshwa, na kupelekea kupunguzwa kwa takriban hekta milioni 4.33 za ardhi iliyoharibika. China imekuwa taifa la kwanza kufikia sifuri kwenye uharibifu wa ardhi huku ikipunguza maeneo yenye jangwa na mchanga.

China imetetea ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na kuenea kwa jangwa, kuanzisha kituo cha kimataifa cha usimamizi wa maarifa na UNCCD na kuandaa Kongamano la Kimataifa la Jangwa la Kubuqi ili kuelezea utafiti wa kimataifa na ufahamu wake wa uchumi wa ikolojia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…