jogoolashamba
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 348
- 71
Nimeshangaa kusikia eti Wabunge wa Bunge la Katiba wamemnyamazisha Mtikila na kumfukuza asiongee. Mimi nadhani hilo Bunge limeanza kujidhihirisha limejaa vibaraka wa watu wenye matakwa maalumu.
Ustaarabu ulikuwa, Mtikila aachwe aongee, ambaye hataki kusikiliza ndiyo atoke nje kungoja anaotaka kuwasikia. Kumfunga mdomo Mtikila ni dalili ya wagumu kulazimisha hoja zao kwa kuzuia za wengine. Wabunge zomea zomea nina mashaka nao!
Hata mimi sikukubaliana na Rais kuteua Wabunge wa Bunge la Katiba kwa utaratibu alioutumia kwa sababu matokeo yake ndiyo hayo, ya Wajumbe kukasirishwa na mawazo ya wajumbe wengine badala ya kuyakataa kwa ustaarabu wa kura.
Kwa nini Rais awachagulie MEWATA mwakilishi badala ya MEWATA kutoa wao kwa kuombwa na Rais? Matokeo yake ndiyo Kingunge kuwakilisha Waganga wa Kienyeji (Tiba Asili) wakati hata biashara yenyewe nina hakika hana!
Tangu lini kundi maalumu likapendekeze watu 12 halafu ateuliwe mmoja?? Nguvu ya kikundi ingekuwa kupendekeza wawili akateuliwa mmoja lakini 12 halafu anateuliwa mmoja ni mbinu ya kuotea.