Kwa nini Mtikila anyamazishwe?

Kwa nini Mtikila anyamazishwe?

jogoolashamba

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
348
Reaction score
71
Nimeshangaa kusikia eti Wabunge wa Bunge la Katiba wamemnyamazisha Mtikila na kumfukuza asiongee. Mimi nadhani hilo Bunge limeanza kujidhihirisha limejaa vibaraka wa watu wenye matakwa maalumu.

Ustaarabu ulikuwa, Mtikila aachwe aongee, ambaye hataki kusikiliza ndiyo atoke nje kungoja anaotaka kuwasikia. Kumfunga mdomo Mtikila ni dalili ya wagumu kulazimisha hoja zao kwa kuzuia za wengine. Wabunge zomea zomea nina mashaka nao!

Hata mimi sikukubaliana na Rais kuteua Wabunge wa Bunge la Katiba kwa utaratibu alioutumia kwa sababu matokeo yake ndiyo hayo, ya Wajumbe kukasirishwa na mawazo ya wajumbe wengine badala ya kuyakataa kwa ustaarabu wa kura.

Kwa nini Rais awachagulie MEWATA mwakilishi badala ya MEWATA kutoa wao kwa kuombwa na Rais? Matokeo yake ndiyo Kingunge kuwakilisha Waganga wa Kienyeji (Tiba Asili) wakati hata biashara yenyewe nina hakika hana!

Tangu lini kundi maalumu likapendekeze watu 12 halafu ateuliwe mmoja?? Nguvu ya kikundi ingekuwa kupendekeza wawili akateuliwa mmoja lakini 12 halafu anateuliwa mmoja ni mbinu ya kuotea.
 
Nasema hivi hakuna katiba mpya ya wananchi kuna katiba mpya ya ccm na hapa tulipo tumepoteza hela zetu walipa kodi. Ngojeni muone hizo hila na vituko vitakavyotokea kwa watu kuleta ushabiki wa kitoto ndani ya bunge maalum la katiba. Ila wananchi msijali ngojeni wapitishe hii ya kwao sisi hapo mbeleni tutatengeneza ya wananchi. Kwahiyo napenda kuwahakikishia watz wasitarajie katiba ya wananchi kwa bunge hili lilijaza wanaCCM
 
Dawa ya ccm ni kuwapiga chini kwenye chaguzi zote zinazofuata.
 
Si Bunge tena hilo... kama hawajachaguliwa na wananchi basi ni kikundi cha raisi na yeyote atakayehoji atapingwa na hilo kundi... hii inanifanya nilidharau hicho wanachokiita Bunge la Katiba Ovyooooo...
 
Back
Top Bottom