Kwa nini mtu aliyekamatwa akiwa mzima afie katika kituo cha Polisi?

Kwa nini mtu aliyekamatwa akiwa mzima afie katika kituo cha Polisi?

Kidogo ungetoa maelezo ukaweka na reference tungeweza kujadili

"Wananchi hawaridhiki na utendaji wa jeshi la polisi. Kuna malalamiko mengi ya wananchi, watuhumiwa kufia kwenye mahabusu za polisi. Tujichunguze na mlifanyie kazi, hatuwezi kuendelea hivyo" - Rais Samia (Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi Yote).
 
Mbona ht mtaani watu ni wenye afya tuu wanadondoka wanakufa
 
Tujadili kidogo
Tujadili nini na wakati inajulikana wazi! Kwani hujawahi kusikia mahabusu wamejinyonga ndani ya kituo cha polisi, na wakati hawaruhusiwi kuingia na vitu hatarishi vya kusababisha hatari kama hiyo ya kujinyonga!
Kufa ni mojawapo ya sifa Kuu za kibaiolojia za kiumbe hai chochote kile hapa duniani. Lakini kwa Tanzania, mtu akifa akiwa ndani ya mikono ya Jeshi la Polisi mara nyingi huwa inakuwa siyo Kifo kitokanacho na kudra za Mungu katika kutimiza sifa hii ya kiumbe hai.
 
"Wananchi hawaridhiki na utendaji wa jeshi la polisi. Kuna malalamiko mengi ya wananchi, watuhumiwa kufia kwenye mahabusu za polisi. Tujichunguze na mlifanyie kazi, hatuwezi kuendelea hivyo" - Rais Samia (Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi Yote).
Wananchi wana malalamiko hata na serikali yake kwa ujumla,nani wa kulichunguza hilo kama sio yeye!!!!
 
Back
Top Bottom