Kwa nini mtu aliyekamatwa akiwa mzima afie katika kituo cha Polisi?

Kwa nini mtu aliyekamatwa akiwa mzima afie katika kituo cha Polisi?

Tujadili nini na wakati inajulikana wazi! Kwani hujawahi kusikia mahabusu wamejinyonga ndani ya kituo cha polisi, na wakati hawaruhusiwi kuingia na vitu hatarishi vya kusababisha hatari kama hiyo ya kujinyonga!
Naunga mkono hoja
 
Tujadili kidogo
Kuna wkt fulani niliona humu kwamba PT wameshika nafasi ya 9 Afrika kwa kufanya kazi kwa weledi. Sasa hizo takwimu zilikuwa cooked au! Maana Kwa hii hali weledi ni 0.
 
Afisa Hajui medical record ya mtu anapiga makofi mazito ili mtu aseme alipopeleka laptop iliyopotelea mazingira yake kumbe mtu alishapataga ajali fuvu lina ufa za kutosha.
 
"Wananchi hawaridhiki na utendaji wa jeshi la polisi. Kuna malalamiko mengi ya wananchi, watuhumiwa kufia kwenye mahabusu za polisi. Tujichunguze na mlifanyie kazi, hatuwezi kuendelea hivyo" - Rais Samia (Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi Yote).
Kiufupi kila kitu katika dunia kina weledi wake, wao naamini wamekosa weledi wa kazi na badala yake wanatumia excessive force (nguvu kupitiliza).
Kwahiyo wanatakiwa wajitune warudi kwenye mafunzo wanayofundishwa na sio matumizi ya nguvu na uonevu kupitiliza
 
Kiufupi kila kitu katika dunia kina weledi wake, wao naamini wamekosa weledi wa kazi na badala yake wanatumia excessive force (nguvu kupitiliza).
Kwahiyo wanatakiwa wajitune warudi kwenye mafunzo wanayofundishwa na sio matumizi ya nguvu na uonevu kupitiliza
Huwa wanafundishwa nini?
 
Tujadili kidogo
Haya mambo hayataisha bila kuwa na serikali inayowajibika kwa wananchi. Na hatutakuwa na serikali inayowajibika kwetu bila sisi wananchi kuacha woga na kudai haki zetu. Wewe hushangai mtu anaua na polisi halafu hapo hapo ndugu zake wanalia kwa mzuka mbele ya kamera eti wakimwomba mama Samia, awasaidie kupata haki? Yaani huyo huyo anayesababisha matatizo ndiyo huyo huyo anayeliliwa kuyatatua. Ina maana hatujui kuwa polisi wanafanya yote haya kwa sababu viongozi hawajali?
 
Mahabusu/kituo cha polisi tunaamini ni mahali penye usalama, mtuhumiwa kufia mahabusu/kituo cha polisi inawezekana kama atakuwa amepigwa kipigo cha kutosha aidha ili atoe ushahidi/kukiri kosa au kwa maelekezo ya yule alie mtuhumu au hasira za mkamataji ambae hapa ni askari polisi. Vilevile anaweza kufa kwa kupewa sumu na mahasimu wake lakini mara nyingi wanatumia kwa kutoa kipigo na kusingizia amejinyonga.

NB. Kipigo hakifanya mtu akiri kosa bali wanaokiri kosa baada ya kipigo ni kwasababu tu ya maumivu. Wengi wapo jela au magereza kwasababu ya kukiri kosa kutokana na kipigo.
 
Nchi yetu inatakiwa iwe na chombo huru kitakachohusika na mambo ya uchunguzi
 
Back
Top Bottom