Kwa nini mvumbuzi wa Chipsi Mayai/ zege, chakula cha kipekee cha kitaifa cha Watanzania wote hajapewa tuzo ya kitaifa?

Kwa nini mvumbuzi wa Chipsi Mayai/ zege, chakula cha kipekee cha kitaifa cha Watanzania wote hajapewa tuzo ya kitaifa?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Mataifa mengi huwa na vyakula vyao vya kipekee ambavyo ni kama sehemu ya utamudini wao kitaifa.
Wako walio na piza, mabaga, taco, shawarma, matoke, githeri, kimchi n.k. Nafikri kwa sisi Tanzania Chipsi mayai ndio chakula cha kipekee kinachotuunganisha kiutamudini Watanzania wote kama taifa na ambacho ni cha kipekee kwetu.

Wale wanaohangaika na vazi la kitaifa wanalo la kujifunza katika hilo jukumu lao la kutafuta kitu cha utamaduni kinachotuunganisha Watanzania wote ambacho ni Chipsi. Mvumbuzi wa Chips mayai/zege awekwe katika vitabu vya kumbukumbu vya historia na pia apewe tuzo.
 
Chips asili yake siyo Tanzania mkuu!

Walau ukisema wali na maharage naweza kuelewa!

Maana jamii zote za mijini na vijijini, matajiri kwa masikini wanakula wali na maharage.
 
Watanzania tunapenda kulakula tu laiti tungekuwa na weledi kama huu wa kulakula kwa kujituma kupiga kazi kwa bidii maporini huko tungekuwa mbali sana.
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Aanze kwanza aliyegundua ugali maharage na Mtori
Ugali Maharage unaliwa na nchi zote zinazotuzunguka, sio chakula unique kwetu pia ni chakula cha hadhi ya chini ndio maana wanapewa wafungwa na wanafunzi zaidi.

Mtori ni chakula cha wachaga zaidi.
 
Tatizo Tanzania haina utamaduni wa kufuatilia wavumbuzi wa vitu mbalimbali. Kwanza huyo mvumbuzi wa chips mayai hajulikani.
 
Back
Top Bottom