Jobless_Billionaire
JF-Expert Member
- Aug 9, 2022
- 5,603
- 14,183
Kwanza kabisa, kama kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na ujuzi wote, kwa nini shwtani awepo?Habari za wakati huu wakuu.
Nina swali ambalo limekuwa likinitatiza kimantiki, ikiwa shetani alimuasi Mungu kwa kiburi na chuki, mantiki ya yeye kumtesa mwanadamu inatoka wapi?
Kwa nini asielekeze "nguvu" zake kwa huyo aliyemuasi badala ya kumshambulia mwanadamu ambaye hana hatia katika ugomvi wao wa awali? Je, mwanadamu anatumika kama "fidia" au kuna siri gani hapa eti?
Huyo Mungu anayezungumziwa miaka nenda rudi wala hajawahi kujitokeza kujidhihirisha mwenyewe.