Kwa nini Nyerere aliukataa Utanganyika akaruhusu Uzanzibar?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Kwa mujibu wa clip:
1. Anajinasibu kwa Utanzania na si Utanganyika
2. Anakiri kuwa Wazanzibar ni Wazanzibar
3. Inaonekana kuna watu walitamani ajitambulishe kwa Utanganyika lakini yeye akaamua kukomaa na Utanzania

Kama Wazanzibar waliweza kubaki na Uzanzibar wao, kwa nini yeye aliukana Utanganyika wake? Wazanzibar walikuwa na nguvu ya ushawishi kumzidi?
 

Attachments

  • MWALIMU_JULIUS_NYERERE_ALIMAANISHA_NINI_HAPA_JUU_YA_WAZANZIBARI._#innolighttv_#magufuli_#nyere...mp4
    1.1 MB
Mwl Nyerere ni chimbuko la matatizo mengi unayoyaona leo Tanganyika.

Tatizo kubwa kuliko yote ni katiba mbaya aliyoitengeneza kwaajili ya yake mwenyewe na ambayo alishindwa kurekebisha kabla hajaondoka madarakani.

Alipigania uhuru wa Tanganyika dhidi ya mkoloni,halafu yeye akawa mkoloni mweusi.
 
Chanzo cha matatizo alitaka kuwafanya wazenji wafuate sheria zao huko alikopewa maelekezo , zanzibar hata wangebaki kuwa huru hamna shida , ushirikiano ungebaki pale pale mbona kenya na nchi nyingine tunashirikiana fresh tu .

Jmaa huyu aliyemtuma kuunganisha zenji ni mtu wa ovyo . Mpaka leo huku bara kuna mapori kikao kuna haja gani ya kuunganisha na zenji wakati tuna eneo kubwa ... Huyu alitaka kubadili utawala wa kule ili wafuate mila za wazungu akashindwa.
 
Simple
Simple':aliogopa upinzani Toka Tanganyika ikabidi aiue tanganyika
 
Unajua tanzania mpaka leo watu wake wakiwa na vyeo,pesa au nguvu wanajiona wao ndio wana akili kuliko wengine.
we angalia wabunge pale wanacho kiongea mpaka unaweza kuona aibu
 
Mzanzibari, mchaga, msukuma, mhaya, mgogo mmakonde, mdigo, mpare, msambaa ni watu au kabila LA huo mkoa tu kwa hiyo sio ishu kuuubwa
 
Sidhani kama akishindwa kurekebisha Katiba! Aliamua tu, ingawa alijua ni Katiba mbovu sana.
 
Nyerere alikuwa na akili kubwa ? mpya hii
 
Hii pointi yako Ingekuwa na mashiko zaidi kama Wanzazibar wasingukuwa wanatawala hadi Tanganyika, lakini haiko hivyo kwani Wanzanzibar wanaweza kuwa watawala pande zote mbili.
 
Nyerere alikuwa mbinafsi.Yaani aliona sifa yeye kuwa Rais wa Tanzania. Unafikiri Abeid angelazimisha yeye ndo awe Rais wa Tanzania,Nyerere angekubali muungano.Nyerere alipenda sana madaraka.Tena alipenda kutawala hata Africa nzima basi tu.Nyerere ubinafsi wake wa kupenda madaraka ndo umetufukisha hapa hadi tunatawaliwa na kina Abdul na mama yake.
 
Nyerere alikiri hadharani kwamba kuna vitu alikosea yeye kama yeye na/au serikali na chama chake.Akatuachia uamuzi wa kubadilisha,kuboresha na kuanzisha mengine mengi.Sioni haja ya kutumia muda mwingi kujadili makosa badala ya kuchukua uamuzi na kutenda kadiri ya matakwa na mahitaji ya muda.Sioni.
Na,ikumbukwe,alishauri kwamba tuchukue yaliyo mazuri na yaliyo mabaya tuyaache.Huko kulikuwa ni sawa kabisa mtu mzima kutubu hadharani kiutu uzima.Sasa kushinda siku nzima kulaani,kushitumu,kumtukana na kumbeza ni wehu huo.
 
Yeye ndiye alitakiwa atengeneze msingi imara kama founding father kuwapa wepesi wale waliofuatia.
 
Yeye ndiye alitakiwa atengeneze msingi imara kama founding father kuwapa wepesi wale waliofuatia.
Sawa.Lakini,tuelewe na litukae vichwani,hakufanya hayo ya matarajio yetu.Kukosea kwake kusitufanye tutumie muda vibaya.Tujisahihishe.Wakati ni huu.
 
Kuruhusu Tanganyika kutawaliwa na Zanzibar ndiyo usmart?

Labda sijakuelewa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…