matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Watu wa imani sala ndio kila kitu. Yaani wakati wasio na imani wanajisifia nyumba ni choo, wao wanatakiwa kusema nyumba ni chumba cha sala.
Watu wengi wa kipato cha kati wakifikilia kujenga, ramani ni masterbedroom, chumba cha vijana wa kike, cha vijana wa kiume, choo cha ndani, sebule na dining, jiko na store. Muonekano wa nje ni mbwembwe tu ila ndani pataishia hivyo.
Akijitahidi ataweka kanyumba ka nje (servant quarter) ili asilale na wageni wenye hadhi ya Chini kwenye nyumba kubwa au ndugu ambao hawapendwi saana.
Huu mtego hadi watu wa imani wamenasa. Kulipaswa kuwa na chumba maalumu cha ibada ambacho sio cha mchezo wala masihara. Chumba hicho ni faragha hata baba mambo yakikusibu unajifungia humo ukiungurumisha dua kwa Mwenyezi Mungu.
Dunia ilipofikia inataka watu wenye misimamo kwenye wanachoamini na kuonyesha kwa vitendo.
Kqma unaimani na mazoezi, Weka chumba cha Gym.
Kama unaamini Mizimu, weka kilinge cha matambiko,
Kqma unaamini katika Uislam, weka kamsikiti kadogo nyumbani
Kama unaamini katika Yesu ambaye ni Mungu, weka chumba cha sala nyumbani tena kizuri kuliko vyumba vyote.
Ni hayo tu....
Kama umeelewa, fanyia kazi. Ishi kwa vitendo unavyoviamini.