Kwa nini Pendekezo la Ustaarabu Duniani limepongezwa sana barani Afrika?

Kwa nini Pendekezo la Ustaarabu Duniani limepongezwa sana barani Afrika?

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111517518306.jpg


Tarehe 15, Machi, wikiendi hii, Pendekezo la Ustaarabu Duniani litatimiza miaka miwili tangu lilipotolewa na rais wa China Xi Jinping. Katika kipindi hicho, kutokana na kanuni zake za kusisitiza uwazi na ujumuishi, usawa na kufunzana, Pendekezo hilo limetoa hekima ya China katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimataifa, na kupongezwa sana na jamii ya kimataifa, hasa barani Afrika.

Hivi Karibuni, Marekani, kwa kisingizio cha "suala la ardhi", ilianzisha vita ya itikadi na kusitisha msaada kwa Afrika Kusini, ikijaribu kuingilia kati siasa za ndani za nchi hiyo ya Afrika kwa kutumia mantiki ya "ukuu wa weupe" na umwamba wa "msaada kubadilishana na siasa." Mbinu hii haionyeshi tu urithi wa ukoloni katika siasa za kigeni za Marekani, bali pia inadhihirisha jinsi Marekani inavyoangalia suala la ustaarabu.

Kinyume kabisa na hii, China imekuwa ikisisitiza dhana ya heshima, usawa, na ushirikiano wa kunufaishana, na kupitia Pendekezo la Ustaarabu Duniani, imetoa chaguo lingine kwa nchi za Afrika, ambalo ni njia ya kutafuta maendeleo inayoheshimu utofauti wa ustaarabu na kuepuka mgogoro wa kiitikadi.

Sababu kuu ya Pendekezo la Ustaarabu Duniani kupongezwa sana barani Afrika ni kwamba, limekabiliana na hamu ya nchi za Afrika na kuwa na haki na usawa. Bara la Afrika liliteseka kwa muda mrefu kutokana na unyonyaji wa ukoloni, na hadi leo linakutana na changamoto za kutokuwa na usawa katika maendeleo, na udhaifu katika uwezo wa utawala. Pendekezo la Ustaarabu Duniani lililotolewa na China linasisitiza mazungumzo na kufunzana kati ya nchi zenye ustaarabu tofauti katika msingi wa usawa, jambo ambalo linalingana kikamilifu na matarajio ya nchi za Afrika, ya kutafuta maendeleo kwa kujitegemea na kufufua ustaarabu mzuri. Majukwaa ya ushirikiano wa kivitendo kama vile Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika na ujenzi wa Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ni mifano hai ya utekelezaji wa Pendekezo hilo, na yametoa fursa halisi ya maendeleo kwa nchi za Afrika.

Pili, Pendekezo la Ustaarabu Duniani limetoa suluhisho la China kwa nchi za Afrika katika kukabiliana na changamoto za kimataifa. Katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi, usalama wa chakula, afya ya umma na masuala mengine ya kimataifa, nchi za Afrika zinahitaji msaada na ushirikiano wa jamii ya kimataifa. China, kupitia Pendekezo la Ustaarabu Duniani, inasisitiza ujenzi wa jamii ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na inahimiza jamii ya kimataifa kushirikiana na kujenga umoja badala ya kupigana na kugawanyika ili kukabiliana na changamoto hizo.

Zaidi ya yote, Pendekezo la Ustaarabu Duniani limeziongezea nchi za Afrika nguvu ya kujivunia na ustaarabu wao. Afrika ina historia ndefu na tamaduni za kupendeza, lakini katika mfumo wa kimataifa unaotawaliwa na nchi za Magharibi, imekuwa katika nafasi ya pembezoni kwa muda mrefu. Pendekezo la Ustaarabu Duniani linapigia debe utofauti wa ustaarabu na kupinga mtazamo wa ustaarabu bora na duni, jambo ambalo linatoa fursa muhimu kwa nchi za Afrika kuthamini zaidi ustaarabu wao na kuboresha ushawishi wao katika mazungumzo ya kimataifa. Katika miaka ya hivi karibuni, nchi za Afrika zimekuwa na sauti kubwa zaidi kwenye jukwaa la kimataifa, na hili ni kielelezo cha kujivunia kwa ustaarabu wao.

Pendekezo la Ustaarabu Duniani linakubalika barani Afrika, sio tu kwamba limeleta nguvu mpya katika uhusiano wa China na Afrika, lakini pia linatoa mwanga muhimu kwa mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa dunia. Inaonekana kwamba, ili kufikia ushirikiano wa kweli kati ya nchi zenye ustaarabu tofauti, ni lazima tuchukue mbinu ya mazungumzo ya usawa na ushirikiano wa kunufaishana, badala ya kutegemea mtazamo wa ustaarabu bora na mantiki ya umwamba.


Mwaka huu ni mwaka wa kuanza utekelezaji wa makubaliano ya mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika mwaka jana, na China na Afrika zinashirikiana katika kuendeleza "Hatua kumi za Ushirikiano," zinazolenga kujenga usasa, ambapo kufunzana kiustaarabu inachukua nafasi ya kwanza katika hatua hizi, na hii inadhihirisha umuhimu wake wa kipekee.

Katika siku za baadaye, kadri Pendekezo la Ustaarabu Duniani linavyohimizwa, ndivyo ushirikiano kati ya China na Afrika utachangia hekima na nguvu zaidi katika ujenzi wa utaratibu wa kimataifa ulio wa haki na usawa.
 
Back
Top Bottom