Kwa nini SAUDI ARABIA na UAE hazielewani na IRAN licha zote kuwa nchi za Kiislamu

Kwa nini SAUDI ARABIA na UAE hazielewani na IRAN licha zote kuwa nchi za Kiislamu

Ndio utashanngaa sasa. Hapo Urusi na Ulaya hawapatani na wanachukiana kweli kweli lakini kamwe huwezi kuwasikia wakiingiza huo ugomvi wao na ukristo japo wote hao ni wakristo.

Hata inapokuja muhalifu kama uhalifu au mauaji yamefanywa na muislamu utasikia wanasema terrorist lakini akiua Mkristo utasikia wanasema shooter.

Hatutishiki na maneno yenu tushawazoea mtasema weeee mkichoka mtaacha
Yaani hawa watu huwa wanafanya kila namna ili mradi tu waislam waonekane ni tatizo.
 
Dini ni za raia. Dini za serikali ni siasa tu. Mbona urusi na Ukraine wako vitani na dini yao mpaka dhehebu ni moja ?
 
Mvutano kati ya Saudi Arabia, UAE, na Iran unakuwepo licha ya mataifa haya kufuata falsafa za pamoja za dini ya Kiislamu lakini utofauti wa kikabila, kijeshi, na kiitikadi unafanya mataifa haya yasiwe na nia moja.

Licha ya mataifa ya UAE na Saudi Arabia kuwa na utajiri wa kutosha na kuwa kwenye Top 3 ya nchi tajiri Mashariki ya kati, lakini zimekuwa zikipata shida kutoka kwa jirani yao Iran. Iran hata kwenye Top 10 ya nchi tajiri mashariki ya kati haimo. Nchi yenye utajiri ikiwa ni Qatar ikifatuwa na UAE, Saudi Arabia, Kuwait, Bahrain, Oman, Israel, Uturuki, Iraq n.k

Sababu zinazopelekea nchi hizi kuwa kwenye Tension ni pamoja na;

1. Mgawanyiko wa Kidini (Sunni vs. Shia)

Saudi Arabia na UAE: Ni nchi zinazotawaliwa na Waislamu wa Sunni ambayo ndio dhehebu lenye Waislamu wengi duniani takribani 90% ya Waislamu wote, ambapo Saudi Arabia hujiona kama kiongozi wa ulimwengu wa Kiislamu wa Sunni.

Iran: Ni nchi yenye Waislamu wengi wa Shia ambao ni 10% ya Waislamu wote Duniani, ikijitangaza kama kiongozi wa ulimwengu wa Kiislamu wa Shia.

Mgawanyiko huu wa kidini unachochea ushindani wa kiitikadi, ambapo kila upande unatafuta kuongeza ushawishi wake miongoni mwa nchi za Kiislamu.

2. Mapambano ya Nguvu za Kanda

Saudi Arabia na UAE: Zinataka kudumisha udhibiti wao katika Ghuba na Mashariki ya Kati kwa ujumla. Wameungana na Marekani na mataifa ya Magharibi, wakiunga mkono baadhi ya mambo ambayo yanawanufaisha.

Iran: Inajitahidi kupinga hali ya Saudi Arabia na UAE kudhibiti ghuba na Mashariki ya kati kwa kupanua ushawishi wake kupitia nchi washirika na vikundi vya wapiganaji katika nchi kama Iraq, Syria, Lebanon, na Yemen.

3. Vita vya Wakala (Proxy Wars)

Pande zote mbili zinashiriki katika vita vya wakala katika maeneo mbalimbali:

Nchini Yemen - Saudi Arabia na UAE zinaunga mkono serikali ya Yemen, wakati Iran inaunga mkono waasi wa Houthi.

Nchini Syria - Saudi Arabia na UAE ziliunga mkono makundi ya upinzani, huku Iran ikiunga mkono uongozi wa Bashar al-Assad.

Nchini Lebanon - Iran inaunga mkono Hezbollah, kundi ambalo Saudi Arabia huliona kama tishio kwa utulivu wa Mashariki ya Kati.

4. Tofauti za Kiitikadi

Iran: Inapigia debe falsafa za uongozi wa kimapinduzi wenye kupinga sera za nchi za Magharibi, uliopata nguvu kupitia Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979. Inajiona kama mpinzani wa kweli wa ushawishi wa Marekani na Israel katika ukanda wa Mashariki ya Kati.

Saudi Arabia na UAE: Zinapigia debe sera za kihafidhina lakini zenye mwelekeo wa kuunga mkono baadhi ya sera za Magharibi kama Amani katika ukanda huo na kupinga maadili ya kimapinduzi ya Iran na msaada wake kwa wanamgambo.

5. Mashindano ya Kiuchumi na Mafuta

Nchi za Ghuba, ikiwemo Saudi Arabia na UAE, zinashindana na Iran katika masoko ya kimataifa ya mafuta na gesi. Vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran vimewapa faida mataifa ya Ghuba kwa kuzuia uwezo wa Iran kuuza mafuta.

Juhudi za Iran za kukwepa vikwazo na kupanua biashara zinapingana na utawala wa kiuchumi wa mataifa ya Ghuba.

6. Misimamo ya Kisiasa ya Kanda

Saudi Arabia na UAE: Zinaungwa mkono na Marekani na mataifa ya Magharibi, ikiwa pamoja na msaada wa kijeshi na kiuchumi.

Iran: Inaungana na mataifa kama Urusi, China, na vikundi vinavyopinga ushawishi wa Marekani, hali ambayo inazidisha mgawanyiko wa kisiasa.

7. Migogoro ya Mipaka

UAE na Iran zina mgogoro wa muda mrefu kuhusu visiwa vitatu katika Ghuba ya Uajemi: Greater Tunb, Lesser Tunb, na Abu Musa. Iran inadhibiti visiwa hivi, lakini UAE inadai umiliki wake.

8. Uhusiano na Israel

Saudi Arabia na UAE zimeanza hatua za kufanikisha uhusiano wa kawaida na Israel (kwa mfano, UAE kupitia Mkataba wa Abraham wa 2020). Iran inapinga vikali Israel na huelezea hatua hizi kama usaliti. Katika mkataba huo UAE na Israeli zilikubaliana kuanzisha ubalozi, kubadilishana mabalozi, na kuanzisha safari za moja kwa moja za ndege, zikionyesha dhamira ya kuwa na uhusiano wazi na wa amani. Kama sehemu ya makubaliano, Israeli ilikubali kusitisha mipango yake ya kuunganisha sehemu za West Bank, jambo lililokuwa muhimu kwa UAE kushiriki katika makubaliano haya. Mataifa haya mawili yalijitolea kushirikiana katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji, afya, na teknolojia, kwa lengo la kukuza uchumi na ubunifu. Makubaliano yalifungua njia za juhudi za pamoja katika usalama wa kanda, kupambana na ugaidi, na kushirikiana kijasusi, hasa kwa kuzingatia masuala ya utulivu wa kikanda. Ili kukuza uelewa wa pamoja, makubaliano yalihimiza mipango kama ubadilishanaji wa wanafunzi, utalii, na mazungumzo ya kidini kati ya watu wa mataifa yote mawili. Marekani ilichukua jukumu la kuhamasisha, ikitoa motisha za kitaalamu, ikiwa ni pamoja na mazungumzo juu ya mauzo ya vifaa vya kisasa vya ulinzi kwa UAE, ili kusaidia mchakato wa kawaida wa mahusiano.
Unawezaje kuwa na uhusiano mzuri na kubwa la magaidi?
 
Hivi kwanini linapo kuja suala la ushindani na uhasama wa kisiasa na kimaslahi kwenye nchi zenye waislam wengi ni razima migogoro hiyo mnarazim8sha kuivika sura za kidini?
Urusi na Ukraine ambao wapo wanauana sasa hivi wote ni wakristo tena wanatoka kwenye dhehebu moja ya kiothodox lakini huwezi kusikia vigagura wakiviusisha hiyo vita na dini.

Marekani ina uadui mkubwa na Venezuela, Cuba na Nicaragua, hali yakuwa wote ni wakatoliki lakini huwezi kuona kigagura kama huyu mleta mada akihusisha migogoro yao na dini yao.

China na Japan ni maadui wakubwa hali ya kuwa wote ni wabudha lakini huwezi sikia wahusisha mgogoro wao na dini wanazo ziamini.
Lakini ikitokea Algeria na Morocco wamekwaruzana kidogo basi hapo uislamu unahusika watu watakuja kuandika ni jinsi gani waislam hawana akili wanagombana wenyewe kwa wenyewe.
Hata hapa Tz wakristo kutwa kupondana makanisani kwa misingi ya madhehebu yao lakini waislam wakitofautiana kidogo tu inakuwa nongwa.
Tukio la Uharifu likifanywa na mtu mwenye jina la kiarabu basi jf itachafuka kwa matusi dhidi ya waislam lakini jina likiwa la kizingu huwezi kusikia hata kwa bahati mbaya likihusishwa na dini yake.
Utofauti ni kuwa Nchi hizo zenye asili ya Kiislamu wanapigana vita huku wakitumia vifungu vya Quran na kutaja maneno au aya za kwenye quran.... Mrusi na Muyukreini hawawezi na hawajawai kutumia neno la biblia wakati wanapigana vita, ni Israel pekee yake ndio uwa anatomia vifungu vya Torati (Biblia Agano la Kale).... hizo nchi zote ulizotaja kuwa ni za kikristo haziongozwi na sheria za Kikristo hata kidogo, lakini Iran, UAE na Saudi Arabia zote hizo ni nchi za Kiislamu na zinaongozwa na sheria za Kiislamu...
 
Ndio utashanngaa sasa. Hapo Urusi na Ulaya hawapatani na wanachukiana kweli kweli lakini kamwe huwezi kuwasikia wakiingiza huo ugomvi wao na ukristo japo wote hao ni wakristo.

Hata inapokuja muhalifu kama uhalifu au mauaji yamefanywa na muislamu utasikia wanasema terrorist lakini akiua Mkristo utasikia wanasema shooter.

Hatutishiki na maneno yenu tushawazoea mtasema weeee mkichoka mtaacha
Urusi na Ukraine au nchi za Ulaya haziongozwi na Sheria za Kikristo labda Vatcan tu....

Nitajie nchi inayoongozwa na sheria za kikristo na hipo Vitani au ina viashiria vya vurugu.... kwanza ni nchi chache sana zinazoongozwa na sheria za Kikristo hata 5 hazifiki, nchi pekee inayoongozwa kikristo kwa asilimia 100 ni Vatican tu.... lakini nchi zinazoongozwa na sheria za Kiislamu ni nyingi sana na kwa asilimia kubwa ndio ziko vitani kila siku
 
UAE?

UAE na Iran wana mahusiano mazuri Mamia ya miaka, inshort Dubai ni zao la Iran na India, isingekua Iran na India wafanyabiashara wao kusupport hilo eneo sidhani kama ingekuepo.

Hii trade ya Iran na UAE miezi 7 ni zaidi ya 16B usd na ni trade ambayo hai involve mafuta

Nchi kugombea visiwa haimaanishi watu wana ugomvi kama unavyo exagerate huko juu,

Ni kama hapa kwetu useme Malawi na Tanzania ni nchi hasimu hazielewani sababu ya mpaka wa ziwa Nyasa
Kuwa Maadui hakuzuii kufanya Biashara, Urusi ni adui wa Marekani na Ulaya, lakini Ulaya nzima inanunua mafuta na ngano kutoka Urusi...

Vita haizuii biashara, vita inapigwa na pesa na baishara inafanyika.... UAE iko mikononi mwa Marekani, hata ulinzi inasapotiwa na Marekani.... UAE ni neutral kwa Marekani, lakini anafanya kazi na yeyote, UAE hipo kibiashara, hata sheria za Kiislamu hazifuatwi kama huko Iran, na ndio maana kiuchumi inashika namba 2 huko Uarabuni baada ya Qatar
 
Ila hii hali kwa usa na israel ndo furaha yake maana yake usa akiwaambia iran ni tishio anaenda kufunga biashara ya dollr bill 30 ikijumuisha ulinzi na usalama na vilipuzi ..waarabu amna kitu hapo iran baba lao na kadiri wanavyomchukia iran ndo ushawishi wake unazidi kuongezeka
 
Ulaya na Marekani wame sanction Urusi, na hata hizo Biashara wanaofanya ni Necessity, na Neither Ulaya ama Marekani imejengwa na Urusi.

Dubai kama mji wa kibiashara from Scratch ni wahindi na Wapersia hapo ndio wamepaendeleza. Kama Hufahamu wabulushi ni wengi mno Oman na UAE hao ndio wana run Majeshi na vitu vyote critical. Oman kuna raia kama milioni 2 ila milioni 1 wana asili ya kibulushi, same kwa UAE wapo kama Milioni 1 na upuuzi ila Takriban laki 2 mpaka laki 4 ni wabulushi.

Ukitoa wabulushi kuna Expart na wafanyabiashara kibao wa KI Iran hapo, in short ni ngumu kugawanyisha hizo nchi na unlike Saudia, UAE ni Nchi ambayo Iran Akikohoa Tu miaka Michache tu inakua haipo tena, Uchumi wao unategemea Dubai creek ambayo ni Bahari wanayoshea Iran na UAE.

images (41).jpeg

Pia UAE ni mtu wa opportunity hapo Dubai hawana hata Mafuta kama wenzao wanategemea Investment za nje, baada ya London sasa hivi Moscow inaitwa 8th Emirate sababu Warusi wengi baada ya sanction wamehamia Dubai, ingekua Usa ana Influence kubwa hapo siku nyingi tu Urusi angeshapigwa pini.
 
Ila hii hali kwa usa na israel ndo furaha yake maana yake usa akiwaambia iran ni tishio anaenda kufunga biashara ya dollr bill 30 ikijumuisha ulinzi na usalama na vilipuzi ..waarabu amna kitu hapo iran baba lao na kadiri wanavyomchukia iran ndo ushawishi wake unazidi kuongezeka
Ambaye kashikwa masikio ni huyo Saudia tu, sababu ana ambition na yeye kuwa super power wa mchongo, ila Nchi nyingi za kiarabu hapo hazina vision kama Saudia.
 
Utofauti ni kuwa Nchi hizo zenye asili ya Kiislamu wanapigana vita huku wakitumia vifungu vya Quran na kutaja maneno au aya za kwenye quran.... Mrusi na Muyukreini hawawezi na hawajawai kutumia neno la biblia wakati wanapigana vita, ni Israel pekee yake ndio uwa anatomia vifungu vya Torati (Biblia Agano la Kale).... hizo nchi zote ulizotaja kuwa ni za kikristo haziongozwi na sheria za Kikristo hata kidogo, lakini Iran, UAE na Saudi Arabia zote hizo ni nchi za Kiislamu na zinaongozwa na sheria za Kiislamu...
Huko ndo kukosa akili kuliko kujaa kichwani, kwahiyo Urusi na Ukraine zingekuwa zinaongozwa kikristo basi huo uhasama walio nao wasinge kuwa nao?
Au Marekani na Cuba nchi zao zingekuwa zina ongozwa kwa sheria za kikristo huo uhasama wao usingekuwepo?
Au Iwapo Iran na Saudia wasingekuwa wanaongozwa na sheria za kiislam basi wasingekuwa na uadui?
Tangu kuisha kwa vita ya pili ya dunia nchi chache sana za kiislam zilizo kubwa na vita ukilinganishwa na nchi mlizo jaa nyinyi.
Tangu kuisha kwa vita ya 2 ya dunia hizi ndo nchi zilizo kumbwa na vita.
Ni Angola 🇦🇴, Libya 🇱🇾, Siaralion,Libelia, Ugosilayvia,Syria, Iraq, Afghanistan, Somalia, Yemen, Sudan, Congo, Rwanda, Burundi, Urusi, Ukraine, Vietnam, Barma, Every Cost, Bolivia, Cuba, Nigeria,msumbiji, Argentina,Africa ya kati.

Hapo nimekutajia nchi 26 ambazo vimekubwa na vita tangu ilipo mazika vita ya 2 ya dunia na kati ya nchi hizo kuna nchi 7 tu ndo zenye waislam wengi ,pia tukiindoa Vietnam, Barma ambazo zina mabudha wengi zilizo baki zote ni zile mlizo jazana nyinyi.
 
Wewe hata hesabu hujui
Hapo nchi zenye Waislamu wengi ni Libya, Sierra Leone, Syria, Iraq, Afghanistan, Somalia, Yemen, Sudan, Ivory Coast, Nigeria, Afrika ya kati

Hapo nchi zenye wakristo wengi ni chache sana, Angola, Liberia, Congo, Rwanda, Burundi, Urusi, Ukraine, Bolivia, Cuba, Msumbiji na Argentina.

Hizo nchi zenye wakristo ulizotaja ni chache sana zenye kuendeleza vita, hapo nchi zenye vita labda Congo tu, tena hao Msumbiji vita vyao vinasababishwa na Waislamu waliounda kundi la kigaidi na kujiita Ahlu Sunna Wa-Jama, ambao wanafahamika kama sehemu ya kundi la Islamic State.
 
Nyie na ukristo wenu mnaelewana? Au ndio kila siku utamsikia Mzee wa upako akiwananga wakatoliki. Mzee wa upako ni Mkristo mwenzako lakini anawapenda walislamu kuliko wakatoliki.

Tuacheni na dini yetu hangaikeni na hiyo dini yenu hata nyinyi hamna afadhali ni wale wale tu
Mkuu, wewe unaweza kuwa muislamu kidini lakini hauwezi kuwa Mwarabu mweupe mwenye nywele ndefu na nyingi kama nyani. Nenda kwao uone kama watakuchekea na kukushobokea. Hiyo inaapply kwa walokole vilevile, hawawezi kuwa Europeans.

Wafia dini wanaodhani wanauhusiano wowote na mataifa zilizotoka hizo dini ni bunch of dumbasses.
 
Hivi kwanini linapo kuja suala la ushindani na uhasama wa kisiasa na kimaslahi kwenye nchi zenye waislam wengi ni razima migogoro hiyo mnarazim8sha kuivika sura za kidini?
Urusi na Ukraine ambao wapo wanauana sasa hivi wote ni wakristo tena wanatoka kwenye dhehebu moja ya kiothodox lakini huwezi kusikia vigagura wakiviusisha hiyo vita na dini.

Marekani ina uadui mkubwa na Venezuela, Cuba na Nicaragua, hali yakuwa wote ni wakatoliki lakini huwezi kuona kigagura kama huyu mleta mada akihusisha migogoro yao na dini yao.

China na Japan ni maadui wakubwa hali ya kuwa wote ni wabudha lakini huwezi sikia wahusisha mgogoro wao na dini wanazo ziamini.
Lakini ikitokea Algeria na Morocco wamekwaruzana kidogo basi hapo uislamu unahusika watu watakuja kuandika ni jinsi gani waislam hawana akili wanagombana wenyewe kwa wenyewe.
Hata hapa Tz wakristo kutwa kupondana makanisani kwa misingi ya madhehebu yao lakini waislam wakitofautiana kidogo tu inakuwa nongwa.
Tukio la Uharifu likifanywa na mtu mwenye jina la kiarabu basi jf itachafuka kwa matusi dhidi ya waislam lakini jina likiwa la kizingu huwezi kusikia hata kwa bahati mbaya likihusishwa na dini yake.
Sababu Europeans wengi, hasa in position of power hawana dini wala kujali uwepo wake. They're too sophisticated for beliefs or a book written over a thousand years ago full of barbaric stories and fairly tales. Otherwise wangekuwa masikini na wanaishi porini mpaka leo. Hicho kitu ni conversely kwa waarabu.
 
usiniletee udini peleka kule. Wakristo ni wamoja dunia nzima japo wana madhehebu mbalimbali
"blaza" unakuwaga na chuki sana sijui kwa nini halafu dini zinabadilishika ujue? kuna mwenzio huku mama yake kipenzi kasilimu😅 mfano tu sijui kama utanielewa😎 "eniwei" afadhali ya waislam wanaswali pamoja na kuelewana popote duniani,lakini sisi roma roma ,shahidi shahidi, sabato sabato na lokole lokole..kuna angilikana pia...😎ukijichanganya huko utakaa kimya🙏
 
WANACHOHOFIA NI UFALME WAO TU HAO ULIOWATAJA...HAKUNA CHA DINI WALA CHA NINI....😎
 
Hebu tuambie kwanza kwa nini Urusi na majirani zake wa nchi za Ulaya hawaelewani na hali ya kuwa wote ni wakristo?
Urusi ni WAKRISTO? Wakati wa vita baridi, kipindi cha Ukomunisti, Wakristo wameuawa sana kwenye hizo nchi including Russia/USSR, Romania, Cuba, Korea ya Kaskazini, Yugoslavia nk. Nauliza tena, lini Urusi imekua nchi ya Kikristo? Au ndio ile, kila mzungu ni Mkristo?
 
Back
Top Bottom