Kuhusu vidonda vya tumbo chanzo ni vitu vitatu
1. Msongo wa mawazo/stress. Maisha yamekuwa magumu hivyo kufanya watu wengi kuwa na msongonwa mawazo hatimaye kupata vidonda vya tumbo. Msongo wa mawazo husababisha mwili kuwa acidic.
2. Lishe duni. Ugumu wa maisha husababisha watu kupata mlo mmoja kwa siku badala ya milo mitatu. Hivyo kufanya tumbo kuwa empty muda mwingi na kuwa rahisi kushambuliwa na acid
3. Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin na panadol. Mtu hajala vizuri, hivyo kufika jioni kichwa kinauma kutokana na upungufu wa sukari mwilini anabugia dawa za maumivu ili alale. Style hii ya maisha mwisho wa siku husababisha ugonjwa wa vidonda vya tumbo.