Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Hizi timu mbili zinazoitwa za wanachama kwa nini uongozi wao hawaweki hesabu zao za kifedha hadharani?
Ukirejea haya malalamiko ya huyu anayeitwa mzee wa Yanga, Magoma na Hamis Kigwangala wa Simba inaonyesha kuna ujanja mkubwa sana katika hizi timu. Hii yote ingeweza kuwekwa sawa kama masuala ya kifedha na biashara katika hizi timu yangekuwa wazi.
Kwenye hizi timu ilitakiwa ijulikane,
Nani ameweka shilingi ngapi kila mwaka, ionyeshe kama ni pesa za mkopo, udhamini au mtu amejitolea sadaka tu kwa kuipenda timu. Pia mapato mengine yote kuanzia ada za uanachama, viingilio vya mechi hadi na mapato ya kushiiki michuano au kuchukua makombe yalitakiwa yawe wazi. Gharama zote pia zilitakiwa kuwekwa wazi. Kwa kifupi hizi timu kila mwaka zinatakiwa kuandaa na kuchapisha hadharani financial statements.
Huyo mzee magoma anasema Yanga katika mauzo ya jezi moja wanapata Tsh 1,300 wakati jezi inauzwa 35,000. Tajiri anaagiza mzigo wa jezi mwenyewe, anafunga na kufungua kontena mwenyewe, anauza mwenyewe. Kwa mwaka wanaambiwa wanapata mapato zaidi ya bilioni 13 kutoka kwa tajiri na wadhamini tu ila mwisho wa siku wanaambiwa timu imepata hasara. Kuna mambo ya hovyo sana kwenye hizi timu.