Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 2,818
- 7,940
Mascot ni mavazi yenye umbo mbalimbali yanayovaliwa hili kuleta uchachu wa shughuli fulani.
Mfano wa mascots ni hizo chini
Au hii
Mimi natamani zile kamati za hamasa na vikundi vya ushangiliaji zingekuwa zinabuni hizi mascot na kwenda nazo viwanjani, hususani kwenye mechi za kimataifa. Hii ingekuwa njia nzuri ya kutengeneza attention, kuongeza mvuto wa mechi na hatimaye kufanya timu zetu zizidi kufuatiliwa na kuwa maarufu zaidi.
Hizi mascot zina uwezo wa kuvutia umakini wa wageni na hata mashabiki wa timu tunazocheza nazo. Zinawafanya watu si wafurahie zaidi ya kutazama mpira tu, wanafurahia pia kuona ubunifu wa mashabiki na namna wanavyoweza kupendezesha na kuleta uhai kwenye ushabiki.
Kwa kifupi, mpira sio dakika 90 tu; ni pia burudani, utamaduni na experience ya mashabiki. Tukiongeza ubunifu kama huu, tunaweza kuifanya Tanzania ionekane zaidi kwenye ramani ya soka la Afrika.