😂😂 Mkuu, mascot sio mizimu wala mambo ya waganga. Hii ni sehemu ya entertainment na branding kwenye mpira wa kisasa. Dunia nzima wanatumia ubunifu huu kuvutia mashabiki, watoto na hata wageni.
Tukisema kila kitu kipya ni “mambo ya kizungu,” tutabaki tunashangilia mpira kwa style ileile wakati wenzetu wanabadilisha mpira kuwa entertainment industry. Mascot haiondoi utamaduni wetu, tunaweza hata kubuni mascot yenye sura, mavazi na identity ya Kitanzania kabisa. Hapo ndipo tunapoweza kuonyesha ubunifu wetu. 😄⚽