Kwa nini Tunaoa? Ni Lini Ndoa ina-expire na hautakiwi kufikiri Kutoa Talaka.

Kwa nini Tunaoa? Ni Lini Ndoa ina-expire na hautakiwi kufikiri Kutoa Talaka.

Kila mtu na imani yake na mafundisho aliyoyapokea, mimi siamini kuachana kwa sababu nyingine tofauti na kifo, sio kama sioni watu wakiachana ila imani yangu sijaiweka huko.
Mathayo 19:3-12
3 Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?

4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,

5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

6 Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.

7 Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?

8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.

9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

10 Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.

11 Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.

12 Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno
hili, na alipokee.
 
Kazi ni shughuli yoyote inayokufanya upate mahitaji yako ya kila siku yanayokufanya uishi.

Ukijifulia au kumfulia mtoto, au ukisafisha nyumba yako unapata Mahitaji yako?

Nafikiri unashindwa kutofautisha kati ya KAZI NA SHUGHULI, MAJUKUMU NA WAJIBU.

Maneno hayo yanaingiliana lakini yanatofauti za msingi
Unapata mahitaji kwa sababu ya kazi hizo ndio maana mume anakutunza kwa imani yetu.

Hakuna cha bure na mke mvivu ni janga.
 
Back
Top Bottom