Kwa nini tusichapishe hela mpya?

Nyambala

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Posts
4,465
Reaction score
1,171
Mimi si mtaalamu wa uchumi wa la mtaalamu wa fedha, lakini nna wazo ambalo naomba wadau tulijadili. Kinachoonekana hivi sasa ni kwamba watu wengi sana wana cash money either kwenye masefu, uchagoni, au hata chini ya ardhi, sina uhakika pia kama hili ni kosa kisheria especially kwenye hii new tz order. Hii imedhihirika hata wakati wa kurudisha fedha za EPA ambapo kuna watuhumiwa walirudisha hizo hela cash kwenye mabegi. Kwa maana hiyo nadhani mitaani kuna hela nyingi tu chafu na ni mabilioni kama sio matrilioni. Hela hizi zinaweza kuwa aidha kutokana na drugs, ufisadi mabao haujawa exposed, illegal arms dealing na hata labda viungo vya binadamu who knows!!!!!!!

Hivyo basi si busara kwa serikali kubadili fedha kipindi hiki na ikiwezekana tukate sifuri tatu i.e mfano 1USD = 1250TZS iwe 1USD = 1.250TZD.

Katika kipindi hiki cha kubadilisha basi inaweza kuwa possible kunail down baadhi ya watu wenye mapesa yasiyoeleweka ( Note: I am not trying to bring the country back in those days when being rich was perceived to align with evilness). Pesa zinabadilishwa zote na maswali yanakuja next. Hii pia itatoa chanagamoto kwa watu kuweka feza benki.

Article hii inaweza kusaidia for wider thinking of this with the current world economic status: Redirect to the target website

Nakaribisha maoni..............
 
Nimekusoma!
Sounds Like A Brilliant Idea ila sina maoni ya ziada coz siyo mchumi hope wachumi wetu humu ndani wanaweza kutupa mwanga kwenye hili suala!
 
Unataka pesa mpya zichapwe zifanyeje?
A. kubadilisha hizi zilizopo,
B. kuziongeza katika mzunguko,
C. vyote viwili
D. None of the above
 
Nyambala, tatizo jingine ni kwamba hela nyingi zilizo ibiwa hapa Tanzania zilikuwa kwenye foreign currency tayari. Na ndipo hapo ukaona watu wanaweza kuzipeleka hata kwenye ma offshore accounts... Hivyo kubadilisha kuna weza kusilete difference yoyote kama itakuwa ni kwa ajili ya kukamata wezi wa EPA na wezi wengine wakubwa.

Hawachelewi kuzileta hizo hela benki na kutoulizwa maswali yoyote, maana tulishasikia zile zilizotupwa nje ya benki without a trace and no one was reprimanded for that.

Either way, It is an idea with good intention.

SteveD.
 
Idea yako nzuri ila kama ni katika zoezi la kuwadhibiti mafisadi wa EPA sidhani kama itafanya kazi. Tumeshuhudia MR PRESIDENT akiwabembeleza mafisadi wa EPA warudishe hizo pesa so its possble hata ukichapisha pesa mpya wao ndio wakawa wa kwanza kubadilisha bila hata maswali kama watakuwa bado wamehifadhi hayo madafu UCHAGONI!
 
Wana uchumi mwagikeni point jamani!!!
 
Watu wamejaa porojo badala watoe sababu za kiuchumi zilizojaa akili!
 
Wangeanza Zimbwabwe kama ni rahisi hivyo...

Zimbabwe wamefanya hiyo kama mara nne hivi na of recent waliondoa sifuri kumi. Kinachowaathiri wazimbabwe ni high inflation kwa maana kwamba hela yao inaloose tena thamani muda si mrefu kwa mfano mwezi septe. walipoondoa sifuri kumi waliipeg US$1 kwa Zim $200 kama sikosei lakini sasa ni more than zim$1,000,000 sasa ukijumlisha na zile sifuri kumi walizotoa ndio unakua unasikia some fun denominations like sextillion, quadrillion n.k .Nchi nyingine pia iliyofanya hivyo ni Ghana na hela yao sasa ni more stronger kuliko hata USD. Just about three years ago hela ya bongo ilukwa na thamani ndogo kuliko Bongo. I remember I once bought a beer in Accra at 150,000 cedes
 
Watu wamejaa porojo badala watoe sababu za kiuchumi zilizojaa akili!

We hatakama si mchumi hii inawezekana kweli tuchapishe pesa! Kama ndo hivyo si tungeshakuwa matajiri!hebu wachumi tusaidieni bwana!
 

Nyambala, mbona conversion ya dollar to cedis kwa leo inasema tofauti?... naomba uende kwenye link ifuatayo huwa naitumia sana na ninafikiri ina approximation nzuri tu: U.S. Dollar to Ghanian Cedi Exchange Rate - Yahoo! Finance
 

Steve D. Unachokisema ni sawa kabisa lakini mimi naamini bado kuna pesa chafu nyingi tu around sema sasa hii system yetu inaweeza kuaccomodate a true censorship. But well what if we try, I a mean the govt tries?
 
Nyambala, mbona conversion ya dollar to cedis kwa leo inasema tofauti?... naomba uende kwenye link ifuatayo huwa naitumia sana na ninafikiri ina approximation nzuri tu: http://finance.yahoo.com/currency/convert?amt=1&from=USD&to=GHC&submit=Convert

Angalia hata hiyo zim$
 
Ghanian currency as of now ni GHS and not GHC kama ilivyokuwa zamani, na kama ukiangalia vizuri hata mimi kwenye post yangu nimezungumzia TZS na TZD but for those who did'nt read it btn letters wamekuwa kidogo confused
 
Nchi kama nchi inaweza kuzuia fedha yake isianguke thamani yake kwa njia kama hiyo ama kwa serikali kukataa kuishusha thamani kwa maelekezo ya WB au IMF.. Tanzania iliwahi kufanya hivyo katika utawala wa Nyerere. Na hata awamu ya Mwinyi kuingia madarakani alikubaliana na masharti yao na thamani ikashuka kadili vyombo hivyo vya fedha vilivyotaka.

Katika Nchi za Tiger miaka ya Mwishoni wa Tisini uchumi katika kanda hiyo ulishuka sana, baadhi ya nchi walikubali kushusha thamani ya pesa zao. Malaysia iligoma na kuifix fedha yao. Hali hii ilidumu kwa muda na hata baada ya uchumi wa nchi hizo kurudi kwenye hali yake, ringgit iliachiwa na ikashuka thamani.
 
Angalia hata hiyo zim$


kweli Zim dollar zina uafadhali.

The bottom line sisi tunahitaji utawala wa sheria tu. Sheria zote za kuzuia matatizo zipo ila hazifuatwi. Au basi lijitokeze jitu moja dikteta lililo zalendo haswaa ndani ya nchi yetu kama Rwanda la kutuongoza!!!! And that would be cutting to the chase..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…