Kwa nini tuwaombee waliokufa?

Kwa nini tuwaombee waliokufa?

N. simzungumzii yule mungu wa sodoma na gomora(wa agano la kale), bali namzungumzia yule aliye sirini Mungu mkuu mwenye upendo na huruma...
Kwahiyo Mungu amebadilika eeh? Tunaomba hiyo version yake Mpya mkuu
 
kuwaombea dua waliokufa inaruhusiwa...but kuwaomba msaada wowote kwa waliokufa ni ushirikina na dhambi kwa muumba...kwa yeye pekee ndio wa kumueleza matatizo yetu yotee
Sijaelewa hapa mkuu maana kama ukifa unaombewa unakwenda mahala pazuri basi kufuata maelekezo ya Mungu ukiwa hai ni useless na kwa kauli hiyo kuzimu hakuna MTU hata mmoja wote wapo paradiso maana wote wanaokufaa wanaombewa. Kuna redio moja wanakipindi cha kuombea wafu daah watu wanaomba sana. Ila reality ni kuwa baada ya kifo ni hukumu sio maombi
 
Last edited:
kuwaombea dua waliokufa inaruhusiwa...but kuwaomba msaada wowote kwa waliokufa ni ushirikina na dhambi kwa muumba...kwa yeye pekee ndio wa kumueleza matatizo yetu yotee

Kama kutubu dhambi na kutengeneza njia za kumpendeza MUNGU ni hapa duniani,na mtu akishakufa hajafanya hayo ni kweli waweza kumuombea na MUNGU akasikiliza maombi yako na kutenda juu yake?late say unamuombea rehema ilihali alikufa akiwa mdhambi,hii ni imani inatoka wapi na tunaamini nini kua huko alilo ktk mauti yupo wapi,anafanya nini,atasamehewa dhambi kwa maombi ya huku duniani kwa walio hai dhidi yake wakimuombea?mbona kama na hili nalo ni ukakasi..
 
Kama kutubu dhambi na kutengeneza njia za kumpendeza MUNGU ni hapa duniani,na mtu akishakufa hajafanya hayo ni kweli waweza kumuombea na MUNGU akasikiliza maombi yako na kutenda juu yake?late say unamuombea rehema ilihali alikufa akiwa mdhambi,hii ni imani inatoka wapi na tunaamini nini kua huko alilo ktk mauti yupo wapi,anafanya nini,atasamehewa dhambi kwa maombi ya huku duniani kwa walio hai dhidi yake wakimuombea?mbona kama na hili nalo ni ukakasi..
hapo ndipo waumini wanapondanganyana na kukesha makaburini wakipalilia na kuomba.
 
Hapa watu mnachanganya vitu v3

1. Kuwaombea marehemu
2. Kuwaomba marehemu
3. Baada ya kifo ni hukumu(kuna siku ya hukumu,somen Bible vzur,IPO siku ya hukumu ambapo Yesu atawatenga kondoo na mbuz na kuuliza maswali Yale ya nilikua na njaa,nilikua uchi,nilikua mgonjwa nk nk sasa pipo znachanganya hiz states )

Nianze na nmba 3

Ni kweli baada ya kifo ni hukumu BT calculate time ya day ya hukumu kutoka siku unakufa had siku ya hukumu,kuna muda apo ambapo departed souls znakua zpo somewhere nafikir hivo



Namba2
Kuwaomba marehemu

Hii inategemea huyo marehemu,kuna ambao wanaish inafaa kuwaomba mfano Yesu alienda kusali akatokea Musa na Elia mtasema Elia alipaa sawa ila Musa alikufa
So kuna watakatifu ambao hutusaidia kama Yesu alisaidiwa labda Faraja /Confort na hawa ndugu Musa na Elia sembuse wewe/Mimi kwann nisiombe Msaada wao


3. Kuwaombea wafu/marehemu

Hapa nakuja ngoja niweke charge simu inazma



Nimerudi

Namba 3.
Kuwaombea wafu/marehemu Biblical cjawah ona ANDIKO linalokataza waamin wasi WAOMBEE wafu, I stand to be corrected,kama kuna MTU ana verse inayokataza directly ashushe hapa. BT nishasoma verse inayokataza "KUWAOMBA WAFU"

Kuna tofaut kati ya "kuwaomba" na "kuwaombea"

Sasa turud kuwaombea marehemu,

Katka kusoma nimegundua kuombea wafu ni tamaduni ya wayahudi( Google Praying for the dead in Judaism) pia Kwa baadhi ya Wakristo wanayo hyo tumaduni hasa hasa Catholics, Anglicans,Methodist,pia Luther naye ktk baadhi ya maandko yake aliandka prayer ya kuwaombea watoto waliofark ingawa badae alifuta hiz mambo ktk kanisa lake.

Tofauti na Kitabu cha pili cha Wamakabayo,pia kuna hii verse ambayo Bible scholars wanaitafsir kuwa Onesiphori Alikua amefark, emu isome.....

Prayer for the dead

New Testament
A passage in the New Testament which may refer to a prayer for the dead is found in 2 Timothy 1:16-18, which reads as follows:

"May the Lord grant mercy to the house of Onesiphorus, for he often refreshed me, and was not ashamed of my chain, but when he was in Rome, he sought me diligently, and found me (the Lord grant to him to find the Lord's mercy on that day); and in how many things he served at Ephesus, you know very well."

As with the verses from 2 Maccabees, these verses refer to prayers that will help the deceased "on that day" (perhaps Judgement Day, see also end times). It is not stated that Onesiphorus, for whom Saint Paul prayed, was dead, though some scholars infer this, based on the way Paul only refers to him in the past tense, and prays for present blessings on his household, but for him only "on that day". And towards the end of the same letter, in 2 Timothy 4:19, Paul sends greetings to "Prisca and Aquila, and the house of Onesiphorus", distinguishing the situation of Onesiphorus from that of the still living Prisca and Aquila.


Mytake
Sala za waamin huenda znasaidia sana hasa Kwa wale waliokufa katka hali ya NEEMA hata pia ktk madhehebu yanayoombea marehemu wanatanguliza hilo neno,waliokufa ktk hali ya Neema.

Hasa inakua na umhimu zaid kulingana na kanisa,kuna kitu kinaitwa communion of saints (hii inajumuisha wazima na marehemu) huu ni mwili mmoja ktk Kristo


Pia kuna hii situation

Marehemu K alikua mkristo Mwema ila pindi anapatwa na mauti let's say ajar,hakuwa ametubu dhambi fulan say z,bt Maisha yake yalikua masafi bt kafa hajatubu dhambi z, na tunasoma kwamba hakuna kichafu chochote kitakachoingia mbinguni,je huyu marehemu K ataenda wapi?
Mbinguni? Au Jehanamu ? Au ndo itabd apitie purification inayoitwa Purgutory in Catholics ? Au aombewe na waamin?


Nitaendelea...
 
W here is pagatory in the bible?


Mkuu hili ni fundisho hasa la kanisa Katoliki, nmejaribu kupitia maelezo yao inaweza toa mwanga wa existance ya Purgutory/Toharani

Fuatana nami apa
Toharani/Purgutory
The Catechism of the Catholic Church teaches:

All who die in God’s grace, but still imperfectly purified, are indeed assured of their eternal salvation; but after death they undergo purification, so as to achieve the holiness necessary to enter the joy of heaven.

Hii ndo ile state kuwa mtu ni mkristo mzuri ila kafariki huku akiwa ana dhambi fulani fulan amabazo hajaztubu, so ndo wanasema (still imperfectly purified) bt amekufa akiwa ktk hali ya neema.

katika agano jipya kuna hiz verses ambozo ntaomba tuztafakari taratibu.

I Corinthians 3:11-15
11 Hakuna mtu awezaye kuweka msingi mwingine badala ya ule uliokwisha wekwa, yaani Yesu Kristo. 12 Juu ya msingi huo mtu anaweza kujenga kwa dhahabu, fedha au mawe ya thamani; anaweza kutumia miti, majani au nyasi. 13 Iwe iwavyo, ubora wa kazi ya kila mmoja utaonekana wakati Siku ile ya Kristo itakapoifichua. Maana, Siku hiyo itatokea na moto, na huo moto utaipima na kuonyesha ubora wake. 14 Ikiwa alichojenga mtu juu ya huo msingi kitaustahimili huo moto, atapokea tuzo; 15 lakini kama alichojenga kitaunguzwa, basi, atapoteza tuzo lake; lakini yeye mwenyewe ataokolewa kana kwamba ameponyoka kutoka motoni.

Emu tufikilie hiz verse znazungumzia nn?
maana inasema kaz ztapimwa kwa moto kuonyesha ubora, kuna amboa kaz zao ztastahimili wao watapokea tuzo,
kuna ambao kazi zao haztastahimili, ztaunguzwa so atapoteza tuzo lakini yeye mwenyewwe ataokolewa kwa moto

katika Biblia moto pia unatumika kutakasa(Purifying agent) so swali la kujiuliza huu utakaso upo before death or after death? Jibu kabisa ni after death, soma hii verse ya 13 uone " Iwe iwavyo, ubora wa kazi ya kila mmoja utaonekana wakati Siku ile ya Kristo itakapoifichua. Maana, Siku hiyo itatokea na moto, na huo moto utaipima na kuonyesha ubora wake."
so swali jingine where is that place?

Emu soma na hii verse
I Peter 3:19
After being made alive, he went and made proclamation to the imprisoned spirits.

kwahyo kumbe kuna gereza huko??? maana hzo spirit hazpo jehanamu ya moto bt zpo somewhere St.Peter named it prison. ----endelea kufikilia


Soma na hapa
Matayo 5:25-26
25 “Mtu akikushtaki, patana naye kabla hamjafika mahaka mani; ili mshtaki wako asije akakukabidhi kwa hakimu, na hakimu akamwamuru askari akufunge gerezani; 26 nami nawaambia hakika, hutatoka huko mpaka deni lako lote litakapolipwa.”

hii ni parable, sawa inatumika sasa katika ulimwengu huu, ila pia ukitanua fikra ukaona hapa hakimu ni Mungu,unaweza pata picha kabisa kuwa mtu hataingia mbinguni hadi alipe deni lake lote.
Huyu mtu yupo gerezani inawezekana ikawa ni apa dunian ila pia fikiri hyo prison anayoisema Petro hapa (1 Petro 3:19)

so tunaweza sema kuwa mtu hataingia mbinguni had alipe den yake, alipie dhambi alizotenda, apitie utakaso.

ila tena tusome hapa ndo pana tanua zaid fikra


Matayo 12:32
32 “Na mtu atakayesema neno kumpinga Mwana wa Adamu ata samehewa, lakini ye yote atakayempinga Roho Mtakatifu hatasame hewa, katika ulimwengu huu wala katika ulimwengu ujao.”

Tunaona juu ya msamaha wa dhambi anaoutoa Yesu
ila hapa kwa maneno ya Yesu mwenyewe anaainisha misamaha katka ulimwengu huu na ulimwengu ujao
swal la kujiuliza huo ulimwengu ujao ni upi? kama ukifa unahukumiwa kwenda mbinguni au jehanamu sasa kwann tena kuna msamaha katka huo ulimwengu ujao?

Kwahyo baada ya kifo kuna tena msamaha, i stand to be corrected maana cjasomea theologia ila ni fkra tu apa huo ulimwengu ujao kwann tena tusamehewe na huku baada ya kifo ni hukumu?

so from these clarifications tunaona kabisa kuna PRISON ambayo roho za marehemu ztawekwa kupimwa kazi zao kama znastahili tuzo au kuokolewa tu kwa moto bila tuzo, so katka that prison mtu ana undergo purifications,analipia madeni yake nashawishka kuamin huko ndiko TOHARAN/Purgatory

Tuendelee kutafakari.....
 
Mkutano wa NICEA kanisa lilikuwa moja tu?
Kwann kila mtu ana juhudi ya kudanganya akitaka akubarike?
Jifunze tena makanisa mangapi yalikuwapo mkutanoni?
Pole sana....rudi usome upya historia ya kanisa na tafuta kuhusu mkutano wa Nicea (425 AD kama sijakosea) enzi za Constantine (aliyeanzisha rosali ndani ya kanisa), ndipo utajua nani aliviondoa na ujue kuwa wakati huo kanisa lilikuwa moja tu. Wa kwanza kujitoa alikuwa Martin Luther (miaka ya 1500) kwa hiyo kusema si kanisa katoliki waliotoa nakusamehe bure, pengine hujui, make a research. Mkutano wa Nicea ndiyo uliweka msingi mkubwa wa imani ya ukristo kikanisa-katoliki ikiwa hujui (mwulize padri au mjuzi wa historia ya kanisa katoloki atakuthibitishia hili)

KITABU cha Yakobo kinahusu Neema....Mwanzoni Martin Luther hakuwa na uelewa kuhusu neema. Na ukisoma nyaraka (thesis) zake za baadaye anakiri kuwa alitaka kufanya kosa kubwa kwa sababu ya kutomwacha Roho Mtakatiifu kumfundisha hapo mwanzo kwa kukipuuzia kitabu hiki na katika vitu ambavyo anakiri kuwa mwanzoni vilimtatizo ni neema na hakutaka kuondoa kitabu hicho tu hata kitabu cha Warumi na vingine vinavyosisitiza neema/grace. Na mwishowe anakiri kuwa Kitabu cha Yakobo ni mojawapo ya backborne za NT kwa sababu kila mtu anaokolewa kwa neema. (SIYO MAOMBI YA WAFU KAMA ULIVYOAMINISHWA NA WAPAGANI WALIOLITEKA KANISA). SO is Ufunuo, mwanzoni Luther hakuwa na ufahamu kuhusu Eschatology na hiyo mpaka sasa mapadre wengi hawana ufahamu wa kutosha kuhusu eschatology hata sasa.

Usijaribu kuleta mjadala tuanze kujadiliana "if"

Na elewa kuwa huu mjadala si vita ya kidini.

Hivyo vitabu vya deutrocanony ulishavisoma? vitafute uvisome kwanza ndipo utajua ni kwa nini viliondolewa na ni kwa vipi vinaweza kummislead mtu asipokuwa mwangalifu. Ni vitabu vya historia tu za vita na mapinduzi (coup) vya Israeli na watawala katika kipindi cha miaka 453 kati ya kitabu cha Malaki mpaka kuzaliwa Kristo (Mathew). Hata katika tanack havimo. vipo katika nyaraka za historia ya waisraeli kama vitabu vya Yosephas/josefus...na wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkutano wa NICEA kanisa lilikuwa moja tu?
Kwann kila mtu ana juhudi ya kudanganya akitaka akubarike?
Jifunze tena makanisa mangapi yalikuwapo mkutanoni?

Sent using Jamii Forums mobile app
Yalikuwa makanisa mangapi vile....karne ya nne....wewe ni mji.nga. Hujui hata hiyo conference ya NECEA ilifanyika lini. karne ya nne makanisa yalikuwa mangapi?
 
Vp
Source: Log into Facebook

KWA NINI TUNASEMA IBADA ZA WAFU NI IBADA ZA KIPAGANI SEHEMU YA I
ANGALIZO:
a. Ninajua, tena nina uhakika sio wote ambao watakubaliana na mafundisho haya, wapo ambao ni kwa sababu hawaujui ukweli, wapo ambao ni kwa sababu tu wamekaririshwa na dini zao na wapo ambao ni mawakala ‘typically' wa Ibilisi kwa hiyo wako kwa kazi maalumu ya kumsaidia shetani kuipindisha kweli ya Neno la Mungu.
b. Jambo la pili nimegundua kwamba, kuna watu ambao wanajiita Wakristo na nafsi zao zimeshiba dini na madhehebu yao, wako tayari kuchinjwa kwa ajili ya kufia madhehebu yao, lakini kamwe hawajui kilichoandikwa kwenye Biblia, wao wamekaririshwa historian a heresies na viongozi wao wa madhehebu, kwa hiyo itikadi za dhehebu ndizo wanazodhani ni fundisho la Neno la Mungu, hawa ni wasumbufu, wanasimamia wasivyovijua, na watakwambia viko kwenye Biblia wakati ukweli ni kwamba havipo na havijawahi kuwepo.
Hapa ninakuja na somo kuhusu IBADA ZA WAFU. Ibada hizo ziko sehemu mbili, ya kwanza ni ile ya kuwaomba Watu (au watakatifu) waliokufa zamani nay a pili ni ile ya kuwaombea watu waliokufa. Kwa mujibu wa Neno la Mungu ibada zote hizi mbili hazikubaliki na neno la Mungu.
KUWAOMBEA WAFU
Mnamo tarehe 24 Januari 2013, Askofu mmoja wa dhehebu fulani hapa Dar es salaam aliwahi kusema kwamba "Kanisa linawaombea marehemu ili WATAKASWE, IKIWA WANAHITAJI KUTAKASWA kabla ya kupokelewa mbinguni wakati miili yao inapobaki ardhini ikingoja kurudi kwa Kristo na ufufuko wa wafu.
Hii ndiyo sababu kanisa linatolea sadaka ya misa kwa ajili ya marehemu. Pia kanisa linasali na kuwaombea marehemu kusudi wapate msaada wa kiroho na waamini walio bado hai wapate matumaini ya uzima ujao mbinguni"
KATIKA KAULI HII YA ASKOFU HUYU TUNAPATA YAFUATAYO;
1. Anakiri kwamba Kanisa huwa linawaombea wafu
2. Anakiri kwamba Kanisa huwa linatoa sadaka kwa ajili ya marehemu
ISAYA 34:16 inasema "Tafuteni katika kitabu cha Bwana mkasome….." Tutafute kwenye Kitabu cha Bwana yaani Biblia, tuone, Je, kuna mahali popote Biblia imewahi kuagiza kuombea wafu?
Na YEREMIA 6:16 inasema Bwana asema hivi, "Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo"
Swali langu hapa ni hili, je, kuna tukio lolote la mtu aliyekufa kuwahi kuombewa kwenye Biblia? Twende tusimame katika njia kuu, tuone, tuulize habari za mapito (walioenenda) zamani, je, kuna mtu aliyewahi kufa kwenye Biblia akaombewa ili atakaswe?
Wako watu ambao hawatakosa majibu, hata hivyo sidhani kama majibu yao yatazidi mawili, ambayo ni, kwanza watasema wafu ambao Yesu aliwaombea na Dorcas aliyeombewa na Petro. Katika hili itakuwa ni matumizi mabaya ya muda kujadili suala hili la Yesu kuombea wafu kama Binti Yairo, Lazaro na wengine. Ukweli ni huu, hawa watu hawakuombewa ili dhambi zao zitakaswe, waliombewa ili warudi katika maisha haya (uhai).
Jibu la pili wanaweza kujibu hivi; watasema kuwa maagizo ya kuombea wafu na kutoa sadaka kwa ajili ya dhambi za wafu yanapatikana kwenye VITABU VYA MAKABAYO; wako wanaodai kuwa vitabu hivi ni vitabu vya Biblia vilivyopotea.
Ukweli ambao wengi hawaujui na wataendelea kufichwa ni huu; vitabu hivi havikuwahi kupotea, isipokuwa vilikataliwa kwa sababu HAVIKUWA NA UVUVIO wa KIMUNGU zaidi ya hadithi na simulizi za kweli zilizowahi kutokea zamani. Simulizi hizi zinawahusu mashujaa wa zamani wa KIYAHUDI walioitwa MAKABAYO.
Katika Kitabu 2MAKABAYO 12:43-46: kwa kiingereza inasema hivi "And making a gathering, he [Judas] sent twelve thousand drachms of silver to Jerusalem for sacrifice to be offered for the sins of the dead, thinking well and religiously concerning the resurrection, (For if he had not hoped that they that were slain should rise again, it would have seemed superfluous and vain to pray for the dead,) And because he considered that they who had fallen asleep with godliness, had great grace laid up for them. It is therefore a holy and wholesome thought to pray for the dead, that they may be loosed from sins."
Nimeipata hii kwa Kiingereza, maana sina vitabu hivyo kwa Kiswahili.
Hapa ndipo baadhi ya watu wanachukulia fundisho la kuombea wafu kuwa ni sahihi; lakini sio kweli, kwa sababu kitabu hiki na vingine vine sio vitabu vya BIBLIA. Vilikataliwa kuingizwa katika orodha ya vitabu vya Biblia kwa sababu vilijaa hadithi kuliko uvuvio wa ROHO MTAKATIFU. Ziko sababu zaidi ya 21 za vitabu hivi kukataliwa, lakini kwa sababu sio somo lake, tuendelee na kuangalia kwa nini MISA ZA KUOMBEA WALIOKUFA NI IBADA ZA KIPAGANI.
WAEBRANIA 9:27 "Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu" Kumbe mtu anapokata roho tu anakutana na hukumu yake instantly, kuwaambia watu eti wamuombee na kumtolea marehemu sadaka ili atakaswe ni kuwaibia watu pesa zao na tena ni kuwaibia muda wao.
UFUNUO WA YOHANA 14:13 inasema "Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, HERI WAFU WAFAO KATIKA BWANA TANGU SASA. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao"
Yesu anajua fika kwamba, hakuna nafasi ya mtu kutengeneza na Mungu baada ya kufa, baada kuachana na maisha haya ya duniani, ndio maana anatangaza kwenye andiko hilo, ili watu wajiandae wakiwa bado duniani, na ni angalizo kwa wale ambao wanangoja kuingia Mbinguni kwa lifti ya sala za marehemu.
JE, KUNA MAHALI PANAITWA PUGATORI?
Kuna dini zinafundisha kwamba kuna sehemu inaitwa purgatory au toharani ambapo mtu anapokufa huenda huko kwanza, na wakati ndugu, jamaa na marafiki wanamuombea huku duniani dhambi zake zinatakaswa kule aliko, na zikishatakaswa zote ndipo sasa anaweza kupokelewa na Mungu. Na ili kutakaswa kwake kuwe kwa haraka, kuna pesa ambayo inatakiwa kutolewa kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya marehemu.
NI AJABU SANA!!! kama mambo haya yangekuwa ya kweli sioni ni kwa nini Yesu alikuja kupoteza muda wake hapa duniani ahubiri Injili ya watu kutubu na kuacha dhambi wakiwa bado wako duniani. Sioni ni kwa nini basi aliacha heshima na Utukufu Mbinguni kama dhambi zingekuwa zinaondolewa kwa shilingi za Tanzania au dola za Kimarekani, Yen ya Japan na Faranga za Kifaransa.
Kwenye Biblia hakuna kitu kinaitwa PURGATORI, HAKUNAAAA!!!!!! Inasadikiwa kwamba Gregory ndiye aliyeanzisha uzushi huu na wengi wakaufuata baadae. Hii ni kama miradi ya watu kujipatia Pesa kutoka kwa masikini na matajiri. Na YESU aliliona na akaonya katika MATHAYO 23:14 akisema;
" [Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapata hukumu iliyo kubwa zaidi.]"
NDUGU ZANGU: Sadaka za misa za wafu haziwezi kutusaidia, ZABURI 49:6-7 inasema hivi "Wa hao wanaozitumainia mali zao, Na kujisifia wingi wa utajiri wao; Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake, Wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake"
WARUMI 6:23 inasema "Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu" Je, ni lini pesa ya mtu inaweza kutakasa dhambi ya mtu kama hakutakaswa na damu ya Yesu alipokuwa duniani?
NUSU HITIMISHO:
Misa za kuwaombea wafu, au arobaini, au hitima ya msiba, kama zinahusisha masuala ya kuombea watu waliokufa hizo ni ibada za KIPAGANI na sio ibada za Wakristo. Haijalishi zinafanywa na nani, ana wadhfa gani na ni maarufu kiasi gani. Ukweli ni kwamba sala hizi hazipo kwenye Maandiko Matakatifu.
MBINGUNI HAKUNA LIFTI: Yesu alikuja duniani ili tuhubiriwe, tutubu, maombi ya waliobaki duniani hayawezi kuwa lifti ya mimi kuingia Mbinguni kama nilikufa katika maisha ya dhambi.
Sadaka za kutoa kwa ajili ya kuwaombea marehemu ni batili, ni watu wasiojua maandiko ndio watakaoendelea kuliwa, maana tumesoma katika ZABURI 49:6-7 "Wa hao wanaozitumainia mali zao, Na kujisifia wingi wa utajiri wao; Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake, Wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake"
AKILI KICHWANI KWAKO,
SEHEMU YA PILI YA SOMO HILI ITAFUATA.

MLIMA WA MAKIMBILIO - BOKO Basiyaya (Basihaya??)
DAR ES SALAAM TANZANIA
Vipi suala lakuwafanyia usafi sehemu za makaburini?lile ni tendo la ibada ama?
 
Unasema M/MUNGU hayupo
Je? Wewe upo
Na upo wapi? Kwa mujibu wa Nani!?
 
Whats your point?

Mjinga hatukanwi ana elimishwa.

So lilikuwa Roman peke yake?

Ilihali before constantine wakristu walikuwa wakiuawa....

Akalazimishe wote waingie Roman.

Yesu amasema shetani anapanda magugu ambayo ni imani ya Roman inayofanana na ya Yesu wa kweli...
Yalikuwa makanisa mangapi vile....karne ya nne....wewe ni mji.nga. Hujui hata hiyo conference ya NECEA ilifanyika lini. karne ya nne makanisa yalikuwa mangapi?
 
Mtu aliyekufa akiwa anamuamini yesu ataishi milele(hatakufa anaendelea kuishi na kunena kama habili)
 
Nimekua najiuliza ni kwa nini mala nyingi hasa mwisho wa mwaka utasikia watu wengi wanakimbia majumbani mwao hasa vijijini na lengo ni kwenda kuwaomba ndugu walioishatangulia kwa maana ya kufa.

Wanaenda mbali na kupeleka maombi yao juu ya maisha yanayowazunguka kwa hao waliokufa,ni kweli kuna maana yoyote au kuna ulazima wa kufanya hili?kama ni kweli MUNGU tunaemuabudu na kuamini kua yupo na ndiyo alietuumba anapata nafasi ipi iwapo tutafikia kupeleka shida zetu kwa wafu?
= mara
 
Waliokufa roho inarudi ilipotoka, kwa kuwa Mungu ni roho, wana uwezo wa kuonana na Mungu ili kutuombea sisi tuliobaki duniani.
 
Mfalme Sauli yalipomfika shingoni akaenda kwa mganga(kwenye mizimu)ili amuite Nabii wa Mungu Samweli ambaye alikuwa kashakufa kitambo ili Samweli amuombee msamaha kwa Mungu maana Mungu aliziba masikio yake hakutaka kusikia maombi ya Mfalme Sauli.
Marehemu Samweli aliitwa na roho yake ikaitika akaongea na mfalme Sauli akampasha yale ambayo Mungu amepanga kuyafanya juu yake na juu ya taifa la Israel. Kwahiyo tunaposema ukifa huna umuhimu tena tuwe makini kidogo tusijekuwa tunapumbazwa ili kupoteza kilichochetu.
 
Back
Top Bottom