Kwa nini tuwaombee waliokufa?

Kwa nini tuwaombee waliokufa?

Duh! Mkuu sio makabayo ni Matayo labda kama ulimaanisha kitabu nisichokijua lakini kama ni Matayo 12:43 hapa Yesu alikua anazungumzia pepo wachafu. tena anazungumzia pepo saba walio waovu, sasa ukweli tunaoutafuta wa kuwaombea wafu na kupeleka shida zetu kwa wafu upo wapi katika mistali hii?

au umechukua kitabu kingine cha Mungu nisichokijua ndo maana nilitaka kusaidiwa kujua umaana wa kuwaombea wafu, bado hujanijibu nikakuelewa ndugu!
MAKABAYO wewe, kasome acha ubishi
 
MAKABAYO wewe, kasome acha ubishi
hivyo ni vitabu vimetungwa na warumi kujaribu kuingiza utamaduni wao kwenye ukristo
lakini biblia ipo clear wafu hawapaswi kuombewa

Waebrania 9:27-28​

Basi, kama vile kila mtu hufa mara moja tu, kisha husimama mbele ya hukumu ya Mungu, vivyo hivyo Kristo naye alijitoa tambiko mara moja tu kwa ajili ya kuziondoa dhambi za wengi. Atakapotokea mara ya pili, si kwa ajili ya kupambana na dhambi, bali ni kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaomngojea.

Mhubiri 9:5​

kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.

Zaburi 115:17​

Wafu hawamsifu Mwenyezi-Mungu, wala wale wanaoshuka katika nchi ya kimya.
 
Back
Top Bottom