Kwa nini vijana wengi wa Dar es Salaam wanapenda kuita wanaume wenzao baba flani?

Kwa nini vijana wengi wa Dar es Salaam wanapenda kuita wanaume wenzao baba flani?

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Hii nimeikuta hapa Dar es Salaam, unakuta mwanaume anamuita mwanaume mwenzake baba flani na wanaona sawa tu.

Kama mimi mtu unakuta mwanaume mwenzangu ananiita baba Nyangwegwe, au baba Kazurungu. Unajiuliza hivi huyu hajisikii aibu? Na hii naona ni kama utamaduni wa watu wa Dar es Salaam kuita wanaume wenzao baba flani.

Na unakuta mtu anajitambulisha eti naitwa baba flani.
 
Mbona mikoani ni vitu mnavifanya sana hivyo i.e Baba Flora, Baba Nani..nimeshasikia mara kadha wa kadha huko mikoani kwenu lakini sikustajabu chochote kile..
 
mimi ni wa mkoani wananiita baba Ephraim
 
Hakimu jitaidi upate hata wa kupandikiza kama imeshindikana kupata mtoto kwa njia ya kawaida
 
Suburi wameenda kunywa supu ya pweza watarudi mda sio mrefu..

Wewe kwani ulikuwa unataka uitwe shost au Best ndo uridhike?
 
Hii nimeikuta hapa Dar es Salaam, unakuta mwanaume anamuita mwanaume mwenzake baba flani na wanaona sawa tu.

Kama mimi mtu unakuta mwanaume mwenzangu ananiita baba Nyangwegwe, au baba Kazurungu. Unajiuliza hivi huyu hajisikii aibu? Na hii naona ni kama utamaduni wa watu wa Dar es Salaam kuita wanaume wenzao baba flani.

Na unakuta mtu anajitambulisha eti naitwa baba flani.
Toa maoni yako sasa na upendekeze unapenda tuite vp
 
Iko namna hii.
Kwa sisi waislamu,wewe mwanamme kama una watoto anaetakiwa akuite baba fulani ni mkeo au mwanamke ambae si ndugu yako yaani waweza msababishia mimba,wengine kama wanaume wenzio wakuite tu jina lako,kama kassam au chandrah,kama wa kike wakuite kaka,mjomba.
Yaani nimuite man mwenzangu baba fulani? Hapana aisee.
 
Back
Top Bottom