Kwa nini vijana wengi wa Dar es Salaam wanapenda kuita wanaume wenzao baba flani?

Kwa nini vijana wengi wa Dar es Salaam wanapenda kuita wanaume wenzao baba flani?

Mara nyingi kuitana baba fulani sio kama ni jambo geni na hasa kwa maisha ya mjini. Kuna watu ambao hawataki kutambulika majina yao kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiusalama au hata za kishirikina kwani mtu akikujua jina lako inakuwa ni rahisi kukufanyia ushirikina ila baba Mwema hawezi kukupata wewe moja kwa moja. Sijaona shida kwahapo kwa kweli labda kama ulikuwa unatafuta njia ya kuwadhalilisha kina baba fulani ila kumbuka pia kuitwa baba kwa wakati huu si jambo dogo hasa kwa nyie vijana wa leo wenye changamoto lukuki
 
Iko namna hii.
Kwa sisi waislamu,wewe mwanamme kama una watoto anaetakiwa akuite baba fulani ni mkeo au mwanamke ambae si ndugu yako yaani waweza msababishia mimba,wengine kama wanaume wenzio wakuite tu jina lako,kama kassam au chandrah,kama wa kike wakuite kaka,mjomba.
Yaani nimuite man mwenzangu baba fulani? Hapana aisee.
Kwani mtu ukimuita baba juma.
Ina maana wewe ni mama juma?
Uislam wa wapi huo sheikh?
 
Hii nimeikuta hapa Dar es Salaam, unakuta mwanaume anamuita mwanaume mwenzake baba flani na wanaona sawa tu.

Kama mimi mtu unakuta mwanaume mwenzangu ananiita baba Nyangwegwe, au baba Kazurungu. Unajiuliza hivi huyu hajisikii aibu? Na hii naona ni kama utamaduni wa watu wa Dar es Salaam kuita wanaume wenzao baba flani.

Na unakuta mtu anajitambulisha eti naitwa baba flani.
ukizaa njoo utupe mrejesho
 
Back
Top Bottom