Kwa nini vita huanza na msisimko mkali mwanzo halafu baadae hupooza ?

Kwa nini vita huanza na msisimko mkali mwanzo halafu baadae hupooza ?

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
6,406
Reaction score
12,736
Ukitazama vita vya Urusi na Ukraine namna vilivyoanza na sasa hali ni tofauti kabisa unaweza hisi labda Ukraine hakuna vita.

Ukija vita vya Gaza navyo vilianza kwa msisimko mkali baadae vikapoa hata ukisikia mabomu yamerushwa Gaza hakuna jipya,rockets zimerushwa Israel hakuna jipya.

Hivyo hivyo vita Sudan namna vilivyoanza na sasa kuzungumwa kwake ni tofauti na mwanzo.

Pia hivi vita vya sasa vya Marekani & Israel dhidi ya Iran msisimko wa mwanzo unazidi kushuka kila siku si ajabu wakaenda siku,wiki,miezi,miaka na watu wakaanza kuchukulia kama maisha ya kawaida tu.

Hivi kwa nini inakua hivi ?
 
Kwa sababu matokeo ya vita huwa tofauti kabisa na malengo au mategemeo ya wale wanaovianzisha.

Putin alianzisha vita Ukraine akifikiri atavimaliza ndani ya wiki moja sasa hivi ana miaka minne akiendelea navyo.

Bush hakutegemea majeshi Marekani ingekuwa Iraq na Afghanistan miaka 20 na bado Taliban irudi madarakani.

Hamas hawakutegemea uvamizi na ugaidi wa October 7 2023 ungepelekea Israel kujibu kwa kufanya genocide kwa watu wao.

Trump hakutegemea Iran ingejibu mashambulizi ya uvamizi wake kwa kulipia hadi maeneo ya raia ya nchi za uarabuni.
 
Back
Top Bottom