Sio kweli, inaweza kuonekana ni Ubaguzi, lakini sababu kubwa hasa ya hao unaowaita Wachaga kuchukua nafasi nyingi kubwa, ni kwamba Mkoa wa KLM ndio unaoongoza kwa Elimu TZ na imekuwa hivyo kwa sababu za kihistoria, Hakuna Mkoa ambao unatilia mkazo Elimu kama KLM, na hakuna Mkoa wenye shule nyingi kama KLM, na imekuwa hivyo kwa karibu miaka 100, hivyo haishangazi popote unapoenda TZ au nje ya TZ utakuta watu wa KLM ndio wana kazi nzuri!
Hata ukienda kwenye Vyuo Vikuu, vitengo vingi vinaongozwa na watu waliosoma KLM, ukienda Nairobi Kenya UN, ukiwa na mawazo kama yako utasema pia kuna Ubaguzi kwa maana karibu kila mfanyakazi Mtanzania utakayemuona amesomea mkoa wa KLM, sasa UN wanajua nini kuhusu huo unaouita Uchaga au sio Uchaga? hivyo sio Ubaguzi bali ni kwamba Mkoa wa KLM umebahatika kutambua umuhimu wa ELIMU tangu zamani sana kwa sababu za kihistoria!