Kwa nini Wakristo wameweka mkazi kusali kabla ya kulala na wakiamka asubuhi?

Kwa nini Wakristo wameweka mkazi kusali kabla ya kulala na wakiamka asubuhi?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Kwa nini Kusali iwe kabla ya kulala usiku na unapoamka asubuhi? Usingizi wa usiku unatisha ?

Ni kama vile binadamu wanaogopa wakilala wanaweza wasiamke, watakufa usingizini usiku!🤣

Sijui wanaofanya kazi usiku nao huwa wanaomba kumshukuru mungu kwa kuwafikisha asubuhi wakimaliza shift yao !
 
Hahahhhhhh sio kweli maombi kwa mkristo wa kweli hayana mda mkuu.... ni wakati wowote!!!

Unapoanza siku mpya lazima ujiweke mkononi mwa MUNGU na hatuombi MUNGU atulinde bali awe pamoja nasi....
 
Hahahhhhhh sio kweli maombi kwa mkristo wa kweli hayana mda mkuu.... ni wakati wowote!!!

Unapoanza siku mpya lazima ujiweke mkononi mwa MUNGU na hatuombi MUNGU atulinde bali awe pamoja nasi....
Mbona kanisani ni J2 tu?
 
Ni mazoea tuu na sio sheria wala haijaandikwa popote.
 
Ishu sio kufa usingizini. Usiku umeficha mambo mengi kiroho. Mambo mengi mabaya hufanyika usiku.
 
Ishu sio kufa usingizini. Usiku umeficha mambo mengi kiroho. Mambo mengi mabaya hufanyika usiku.
Mambo gani ya kiroho yamefichwa na usiku? Mfano wa mambo gani mabaya hufanyika usiku na hayafanyiki mchana ?
 
Sijajua kwa nini umetumia neno "Wakristo" ni ufahamu wako umeishia hapo au una agenda nyingine?

1. Uislamu

Unapoamka:
Waislamu husali swala ya Al-Fajiri
Kabla ya kulala: Waislamu husali swala ya Isha (swala ya mwisho ya usiku). Baada ya hapo, kuna sunnah (utaratibu) wa kusoma dua maalum ya kulala na sura fupi za Qur'ani (kama vile Ayat Al-Kursi na Surah Al-Ikhlas, Al-Falaq, na An-Nas) kwa ajili ya ulinzi usiku.

2. Ukristo
Unapoamka (Maombi ya Asubuhi): Wakristo wengi huanza siku kwa kufanya maombi ya kumshukuru Mungu kwa ulinzi wa usiku, kukabidhi siku mpya mikononi mwake, na kuomba baraka na mwongozo.

Kabla ya kulala (Maombi ya Usiku): Kabla ya kulala, Wakristo hufanya maombi ya kutubu dhambi za siku nzima, kumshukuru Mungu kwa mambo yaliyofanyika, na kuomba ulinzi dhidi ya ndoto mbaya au hatari za usiku. Katika baadhi ya madhehebu (kama Wakatoliki na Waanglikana), kuna sala maalum za usiku zinazojulikana kama Compline.

Uyahudi: Waumini wa Kiyahudi husoma sala inayoitwa Shema kabla ya kulala na sala ya Modeh Ani mara tu wanapofumbua macho asubuhi kumshukuru Mungu kwa kurudisha roho zao.

Uhindu: Wahindu wengi hufanya maombi (Puja) asubuhi wanapoamka na jioni/usiku kabla ya kupumzika.
 
Kwa nini Kusali iwe kabla ya kulala usiku na unapoamka asubuhi? Usingizi wa usiku unatisha ?

Ni kama vile binadamu wanaogopa wakilala wanaweza wasiamke, watakufa usingizini usiku!🤣

Sijui wanaofanya kazi usiku nao huwa wanaomba kumshukuru mungu kwa kuwafikisha asubuhi wakimaliza shift yao !
Ushawahi kuumwa degedege
 
Andiko ktk biblia lenye muongozo huo

Zaburi 5:3
BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.

Zab 119:147
Naamka kabla ya mapambazuko na kukuomba msaada, Naweka tumaini langu katika maneno yako.
 
Back
Top Bottom