Kwa nini wanachama wasaliti wa Chadema nyota zao hupotea jumla?

Kwa nini wanachama wasaliti wa Chadema nyota zao hupotea jumla?

The Burning Spear

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
9,205
Reaction score
22,219
GT
Anayejua hili atuambie inakuwaje mtu anayetoka.chadema kwenda kwingine nyota yake hufifia mazima. Tofauti na anayetoka Chama kingine kuingia Chadema.
What is going on? Au ndo mpango.wa mungu hatujui tu
 
Ndio faida ya snitch.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Chadema ni chama kilichojipoambanua kwa kupigania haki iliyobinywa na ccm kwa wananchi wake

Nje na Chadema, huwezi kusikia popote, chama chochote kikijitaja kuwa kinapambania haki za Watanzania

Sana sana utazisikia sauti hizo kwa gerersha tu na hazimaanishi kabisa kutoka mioyoni mwa hao vyama vingine

Hii inamaana kuwa, nguvu ya ccm ni kule kizigawanya kura kupitia vyama inavyoviunda yenyewe kwa ajili ya kuihofia Chadema
 
Wanachama anabebwa na sera za chama chake na pia anajijenga mwenyewe na kuaminiwa na wanachama. Anaposaliti anatengwa na haaminiki sana hata anapohamia kwa kuwa wanahisi hana msimamo anaweza kurudi pia alikotoka kikubwa ana masalahi au uroho wa madaraka ndio uliomfanya ahame hapo mwanzo. Inampunguzia confidence pia hata vitu alivyopigania kwa haki akiwa Chadema inabidi avikane aendane na mfumo wa alikohamia. Na inapokuwa msimamo wa awali alikuwa sawa akaponda upande wa pili na kuonyesha udhaifu wao bado atajifanya kama haoni. Wananchi wengi wao nowadays wana uelewa mpana wa masuala mengi.Wana intellect safi, thinking and reasoning ability zao ni super kabisa. Wanakuchora wanakupotezea hasa hoja zinapokuwa kama za kitoto.
 
Back
Top Bottom