Kwa nini Wanajeshi, polisi, magereza na Usalama wa Taifa bado wanamlilia Rais Magufuli?


Ulifanya sensa lini na ukapita makambi yote kuwauliza?
 
Sawa Kama alikuwa panya road unategemea Nini?

Mwisho mfumo wa sheria yaani Polisi na Mahakama Kuna uonevu na rushwa Sana huko.
Huwa sipendi kuweka hisia mbele ila tukisema kama hivyo kwa Lissu huwa mnatuona tuna roho mbaya, watu wanakamatwa kwa uonevu tu wa polisi na kujitengenezea kamradi chao wanapiga hela.

Kwahiyo polisi bado wanafanya mambo yao kama si wamezidisha sasa hivi.
 
Vipi umeamka au bado unaota majinamizi ya shetani mkuu!
 
Uwongo mtupu!
 
Katika kuwadodosa, wanasema wazi Magufuli aliboresha maisha yao na kuwapa meno kwa kiasi kikubwa..

Rais Samia kwa upande mwingine anaonekana kuwabana na kuwarudisha katika mstari wa kusimamia haki na kuwalinda Raia.
Sasa majibu si haya hapa tayari unayo
 
JPM aliamini katika hulka za kibabe na kiuonevu labda alilelewa kitemi utotoni na ikamwathiri mpaka uzeeni.

SSH ni tofauti ni mzenji mwenye kuamini katika hulka laini za mwambao, mambo yale ya jioni saa kumi na mbili badala ya ugali au ndizi wao wanakula chapati na mikate na nyumba nzima imefukuziwa udi.
 
Yuko wapi Cyprian Musiba anaweza akaja hapa atueleza kwani amekuwa kama amepigwa kitu nzito kichwani ndio utajua kweli ya uliyoeleza! Alikuwa anatumwa????

Sent from my T810S using JamiiForums mobile app
 
Acha uongo watu wakipata masilahi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…