Kwa nini Watanzania Tunahusudu mambo ya Kenya kuliko nchi nyingine EA

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Posts
10,420
Reaction score
17,735
leo hadi msemo "Kama kawaida" wengine wameubatiza "Kama kenya"

Uganda kumekuwa na Uchaguzi, umepita kimya...
Rwanda sijasikia hata kada au kamanda kagusa chigali kupiga promo.
Burundi hata ukiweka swali la interview Mpinzani mkuu ni nani huko Ufipa nzima wanakula F.

kwa nini kenya?
mbona wao huwa hatuwaoni wakikomaa hivyo kama huku...

Je Tanzania bila kujifananisha na kujilinganisha na kenya kwenye kila kitu haiwezekani?

NAWAZA
 
Utawala wa sheria ni tatizo sugu kwa nchi nyng za kiafrika
Huduma bora za kijamii ni changamoto pia kwa nchi flan za africa
Miundombinu rafiki kwa maendeleo ya nchi ni tatizo pia kwa nchi nyng za africa

Sasa unapoona Kenya inajitahidi kupiga hatua kweny sector hizo na ni nchi jiran na Tz, n lazima watu tuiongelee
Na hatufany hvyo kuonesha kutukuza Kenya, la hasha. Ila tunafany hvyo ujumbe kwa viongozi tulowapa majukumu ya kusimamia na kutatua changamoto hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya ni mashaka watanzania haswa sisi tulio upinzani hatuelewi na hatujui msimamo wetu nini!
 
wamewageuza vijana wengi kuwa kama mazombie hawajui wapende nini wapinge nini au waunge mkono nini na kwa wakati gani maana kila sekunde utasikia nyuma geuka, kuanzia sasa penda ulichokua unakichukia, pinga ulichokuwa unasisitiza.
 
Utawala wa sheria ni tatizo sugu kwa nchi nyng za kiafrika
Huduma bora za kijamii ni changamoto pia kwa nchi flan za africa
Miundombinu rafiki kwa maendeleo ya nchi ni tatizo pia kwa nchi nyng za africa

Sasa unapoona Kenya inajitahidi kupiga hatua kweny sector hizo na ni nchi jiran na Tz, n lazima watu tuiongelee
Na hatufany hvyo kuonesha kutukuza Kenya, la hasha. Ila tunafany hvyo ujumbe kwa viongozi tulowapa majukumu ya kusimamia na kutatua changamoto hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
pamoja na yote kwa nini nguvu kubwa isingepelekwa kulaani aliyechakachua uchaguzi kupelekea gharama kubwa ya kuurudia badala yake tunataka kuaminishwa ni shujaa wa demokrasia.
unadhani kwa nini nguvu kubwa hasa ya wapinzani isiende burundi,uganda na rwanda
 
Hata wakenya wanahusudu sana mambo ya Tanzania.
Nchi hizi Ni jirani na zaidi zinashare lugha moja.
Hizi ndo sababu zinazoleta muingiliano wa ukaribu kati ya Tz na Kenya.
Ukifatilia media za Kenya muda mwingi wanafuatilia masuala ya Tz hali kadhalika midia za kwetu
 
wamewageuza vijana wengi kuwa kama mazombie hawajui wapende nini wapinge nini au waunge mkono nini na kwa wakati gani maana kila sekunde utasikia nyuma geuka, kuanzia sasa penda ulichokua unakichukia, pinga ulichokuwa unasisitiza.
Hapa unakosea na unaonesha jinsi gani ulivyo ACCORDER
Wakati unayasema hayo, urudi nyuma na kukumbuka kuwa issue zote za ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka, kudorola kwa uchumi, uhaba wa huduma kam dawa, maji n.k, ubovu wa mfumo wa elimu, uduni wa miundombinu, kujilipa posho kubwa kwa kazi ndogo, ukosefu wa ajira, mishahara midogo, mazingira magum ya kufanyia kaz n.k.....vimekuwa vikiibuliwa na kuongelewa na wapinzani

Sasa unaposema wapinzani hawana msimamo kwa kurejelea hoja moja tu, unakuwa hauko sahihi sana.

Punguza hisia boss, jaribu kupanua kichwa kidogo kabla hujaongea jambo, itakusaidia na watu watarejea maneno yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sababu Kenya inapiga hatua kwenda mbele, Tanzania inapiga hatua kurudi nyumba. Jeneral Ulimwengu alisema tumerudi nyuma miaka 50. Kwa hali ilivyo, mimi nafikiri tumerudi nyuma miaka 100. Can you imagine, it is 2017 lakini sheria zetu bado zinakataza kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais mahakamani?
 
pamoja na yote kwa nini nguvu kubwa isingepelekwa kulaani aliyechakachua uchaguzi kupelekea gharama kubwa ya kuurudia badala yake tunataka kuaminishwa ni shujaa wa demokrasia.
unadhani kwa nini nguvu kubwa hasa ya wapinzani isiende burundi,uganda na rwanda
Hapa ndio unapoonesha kukerwa kwa jambo lililokuwa sahihi
Unafikiri kilio cha waafrika wengi ni nin kweny masuala ya utawala wa sheria??
Jibu n jepesi, NI UBOVU WA MIFUMO

Sasa unapoona mwenzako kajitahid kuweka mifumo vizur, unapaswa kupongeza na kuiambia serikali "iga kwa huyu"

Kuhusu Rwanda ama Burundi na hata Congo, si kazi ya wapinzani pekee kuelezea hilo.
Na kwakuwa tunafanan nao, hatuna haja ya kuwarejelea maana hakuna faida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
leo hadi msemo "Kama kawaida" wengine wameubatiza "Kama kenya"

Uganda kumekuwa na Uchaguzi, umepita kimya...
Rwanda sijasikia hata kada au kamanda kagusa chigali kupiga promo.
Burundi hata ukiweka swali la interview Mpinzani mkuu ni nani huko Ufipa nzima wanakula F.

kwa nini kenya?
mbona wao huwa hatuwaoni wakikomaa hivyo kama huku...

Je Tanzania bila kujifananisha na kujilinganisha na kenya kwenye kila kitu haiwezekani?

NAWAZA

Nyinyi maccm ndo mjifunze kuheshimu democrasia na uhuru wa mahakama acheni kuwatisha majaji
 
1-Kenya
2-Tanzania
3-Uganda
4- Rwanda
5- Burundi
1-itafuatilia mambo ya Ulaya,Asia America nk
2- itafuatilia mambo ya Kenya,Ulaya ,Asia,America nk
3- Tanzania,Kenya Ulaya,Asia ,America nk

Mtiririko ni huo mpaka tujitambue hatuwezi kuipita Kenya bila kuijadili na kutenda kama wao ktk masuala makubwa ya kimaamuzi kama KATIBA
 
Kielimu kiuchumi wapo juu, nilienda huko Mkenya hana blaablaa anaenda na wakati. Kama break ya chai ni robo saa hapunguzi au kuongeza. Mbongo baada ya chai ni story, mara clabu kubwa za Ulaya mara mambo ya udaku. Tukiwaiga tutapiga hatua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa unakosea na unaonesha jinsi gani ulivyo ACCORDER
Wakati unayasema hayo, urudi nyuma na kukumbuka kuwa issue zote za ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka, kudorola kwa uchumi, uhaba wa huduma kam dawa, maji n.k, ubovu wa mfumo wa elimu, uduni wa miundombinu, kujilipa posho kubwa kwa kazi ndogo, ukosefu wa ajira, mishahara midogo, mazingira magum ya kufanyia kaz n.k.....vimekuwa vikiibuliwa na kuongelewa na wapinzani

Sasa unaposema wapinzani hawana msimamo kwa kurejelea hoja moja tu, unakuwa hauko sahihi sana.

Punguza hisia boss, jaribu kupanua kichwa kidogo kabla hujaongea jambo, itakusaidia na watu watarejea maneno yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
hilo jambo moja ndilo linalojadiliwa sasa, hayo mengine unayoleta mkuu ccm hiyohiyo kupitia mwenyekiti wake anayashughulikia
 
Back
Top Bottom