Kwa Nini watu wengi Duniani hufikiri Afrika ni Nchi Moja Je, Darasani Hawafundishwi?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
Ni jambo la kushangaza kwamba hadi leo bado kuna watu ulaya na asia huko wanaouliza “Afrika ni nchi gani?” kana kwamba Afrika si bara lenye nchi zaidi ya 50. Hii inafanya mtu kujiuliza: je, darasani hawafundishwi vizuri kuhusu dunia au kuna kitu kinapotea kwenye elimu?

Badala ya kufundishwa nchi zake moja moja, watu wengine hupata picha ya Afrika kama sehemu moja yenye hali moja tu, jambo linalopotosha uhalisia.

Swali linabaki: ni kwa nini uelewa wa msingi kama huu bado unawachanganya watu wengi duniani mpaka unajiuliza wanasoma nini kwenye geography zao na civics
 
Wewe hilo linakushangaza?? Kuna wamarekani wengi tu hawajui hata Tanzania iliko au hata kuna nchi inaitwa Tanzania maana uwa wanaconfuse na Tasmania. Wenzetu jiografia yao hawafundishwi kukariri miji mikuu au nchi au hata ma continent, wanafundishwa vitu vya duniani na athari zake kwa binadamu. Ni kweli wengi hawajui kua Afrika ni continent yenye nchi nyingi zenye culture tofauti na lugha tofauti.
 
Hasa USA ila jamii ina watu wasio na uelewa wa geography kuliko kawaida.
 
Wewe hilo linakushangaza?? Kuna wamarekani wengi tu hawajui hata Tanzania iliko au hata kuna nchi inaitwa Tanzania maana uwa wanaconfuse na Tasmania. Wenzetu jiografia yao hawafundishwi kukariri miji mikuu au nchi au hata ma continent, wanafundishwa vitu vya duniani na athari zake kwa binadamu. Ni kweli wengi hawajui kua Afrika ni continent yenye nchi nyingi zenye culture tofauti na lugha tofauti.
Ndiyo maana Vyuo Vikuu vyao vingi vina Faculty za African Studies.
 
Una uhakika kwamba mitaala yao huko wanasoma civics na jiografia kama vile mfundishwavyo huku bara giza?

Mimi nilisoma history nikiwa primary tu baada ya hapo sekondari sikuhangaika nayo na haikuwepo kwenye masomo yangu.
Huko kwa wenzetu mwanafunzi anafundishwa kile alicho opt kusoma vinavyobaki ni takataka kwake.
 
Africa ndiyo tunasoma nchi zilizoendelea, sasa nchi zilizoendelea zinawezaje kusoma third world countries? Mfano Mo anaweza kuwajua masikini wa buza? Ila masikini wa Buza wanamfahamu Mo na pengine hadi huko mikocheni sjui msasani anapoishi......ila Mo hawezi kujua hata buza iko wapi anaweza fikiri kiembe mbuzi na karakata ni sehemu moja
 
Lakini mbona Africa wengi wanajua sio nchi moja? Anyways labda unaokutana nao huko.....
 
Back
Top Bottom