ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Hasa USA ila jamii ina watu wasio na uelewa wa geography kuliko kawaida.Ni jambo la kushangaza kwamba hadi leo bado kuna watu ulaya na asia huko wanaouliza “Afrika ni nchi gani?” kana kwamba Afrika si bara lenye nchi zaidi ya 50. Hii inafanya mtu kujiuliza: je, darasani hawafundishwi vizuri kuhusu dunia au kuna kitu kinapotea kwenye elimu?
Badala ya kufundishwa nchi zake moja moja, watu wengine hupata picha ya Afrika kama sehemu moja yenye hali moja tu, jambo linalopotosha uhalisia.
Swali linabaki: ni kwa nini uelewa wa msingi kama huu bado unawachanganya watu wengi duniani mpaka unajiuliza wanasoma nini kwenye geography zao na civics
Ndiyo maana Vyuo Vikuu vyao vingi vina Faculty za African Studies.Wewe hilo linakushangaza?? Kuna wamarekani wengi tu hawajui hata Tanzania iliko au hata kuna nchi inaitwa Tanzania maana uwa wanaconfuse na Tasmania. Wenzetu jiografia yao hawafundishwi kukariri miji mikuu au nchi au hata ma continent, wanafundishwa vitu vya duniani na athari zake kwa binadamu. Ni kweli wengi hawajui kua Afrika ni continent yenye nchi nyingi zenye culture tofauti na lugha tofauti.