Kwa nini Yesu alipenda kuingia Nyumba za MATAJIRI na SIO masikini rafiki zake?

Kwa nini Yesu alipenda kuingia Nyumba za MATAJIRI na SIO masikini rafiki zake?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
9,514
Reaction score
23,523
Kuna mchungaji mmoja nilimuuliza KWA nini unapenda kutembelea Nyumba za MATAJIRI na Sio masikini akasema hata Yesu aliifanya hivyo. Mwingine Nigeria anashambuliwa KWA kutoa kauli kama hiyo.

Ikabidi nizame kwenye NENO kumchunguza Yesu. Nikagundua....

Yesu alipokutana na Tajiri Zakayo, alimwambia Leo ntakuja nyumbani kwako.

Yesu alichukua karibu siku nzima KWA Tajiri Simon. Akila na kupiga stori.

Yesu alikuwa na Urafiki na Razalo na dada zake. Hawa nao hawakuwa choka mbaya kama walikuwa na uwezo wa kuulisha msafara wa Yesu KWA siku kadhaa.

Najiuliza hii ilimaanisha nini na inamaanisha nini KWA watumishi wa siku za Mwisho kujenga ukaribu na MATAJIRI na kupenda kuwatembelea kuliko masikini wa kifedha ili kuwaombea wazipate?.

Ni hayo tu
Mtumishi Matunduizi.
 
You know,

Kati ya vitu vya ajabu kuwahi kutokea duniani ni muafrika na tathmini yake ya biblia na mambo ya kiroho.

Biblia imeeleeza matendo ya Yesu ila haijailezea historia kamili ya Yesu.

Hakuna kila kifungu kilicho muongelea Yesu katika kila hatua ya Maisha yake thus kuna mengi aliyafanya ambayo hayakuwa noted.

Sasa kwnda tu kwa tajiri wawili sasa ndio muafriak ooh Mungu hafanyi agano na masikini ,blah blah

Tantalizing africans🤡🤡
 
Mambo ambayo Yesu amefanya imeandikwa ili yarekodiwe inabidi dunia iwe karatasi na miti iwe kalamu.

Ila haya yameandikwa ili KWA kuyaamini tupate wokovu. Kwa hiyo statistics zilizoandikwa zinatupa uhalali wa kuzifanyia maamuzi na tafakuri.
 
Ukweli ni kwamba Mali au utajiri una mchango mkubwa katika kuendesha dini
 
Ukweli ni kwamba Mali au utajiri una mchango mkubwa katika kuendesha dini
Dini zilizochelewa waumini kumiliki uchumi ili kazi ya Bwana Yesu isonge mbele zimejikuta nyuma Kila kitu. Kajengo ambako waumini watatu wanaweza kuilmaliza, watajenga watu 20,000 huku shughuli nyingine za kiroho zikibaki zimesimama tena KWA miongo kadhaa.

Yesu ili kazi yake iende ilihitaji masponsa. Tena wengine walikuwa wafanyakazi Ikulu ya Herode.

Huu ndio Msingi wa hoja.
 
Na huo ndio ukweli halisi
 
Umesahau pia ndio walionzika
Ni kweli, alizikwa na Tajiri Yusuph wa Armathaya kwenye makaburi ya matajiri.

Mtazamo KUWA utajiri ni ushetani ni mbinu ya shetani kuwahafifisha wafuasi wa Yesu.
 
Back
Top Bottom