Kwa nyomi ya walimu wa kiswahili ile nilioshuhudia siku ya usaili wao, hakika nawashauri vyeti wachome moto na wasahau suala la ajira

Na vyuo navyo vinazidi kufyatua tu.

Nchi hii imekosa direction
Hatari, vyuo vinahitaji pesa za fees ili kujiendesha, kulipa mishahara nk, wao, hawajari kinachoenda sokoni,wanalinda ajira zao, ni kufyatua tu,
Juzi, nilitembelea chuo kimoja kinachofundisha kuendesha na ku operate heavy machines, cranes, vijiko, caterpillars, ni, Karo ni kama 1.2M kwa miezi, miwili, ila ukimaliza ajira kibao, maana wataalamu wa baadhi ya mitambo ni wachache, (kule Tanga, linapojengwa bomba LA mafuta,wataalamu ni wachache), Bora kijana asomee hii kitu kuliko huu upuuzi wa kiswahili,
Swahili bila lugha nyingine, ni upuuzi, unamfundishaje machina, mkorea,mjapan kiswahili na wewe hata kizungu, kifaransa shida! Hawa vijana hawauziki nje ya mipaka! Wataishia kuendesha vimeza vya mpesa,kudanga, bodaboda, na content za kutikisa makalio
 
Vijana wanaosoma vyuo wajifunze ujuzi mwingine tofauti na ule wanaousomea ambao utawasaidia kusurvive mtaani. Mfano useremala, welding au kutengeneza magari la sivyo ataona maisha magumu.
Ili wajifunze huo ujuzi mwingine inawakazimu kwanza wahitimu huko wanakosoma, kisha wazazi/walezi waendelee kukusanya nguvu za kuwapeleka vyuo vya Kati; huku umri unasonga.
Siasa zikar pembeni, kuna haha ya kuditisha udahiki kwa baadhi ya kozi kwa muda.
 
Naunga mkono hoja
 
Umeongea pointi kubwa sana
 
K
Kabisa naunga mkono hoja
 
Nafikiri serikali ihakikishe kwenye mitaala ya elimu wanayotoa somo la Ujasiriamali linaingizwa!
Mwanafunzi ajengwe kisaikolojia kabisa kuwa hakuna ajira ikitokea basi.
 
Kwa hali hii kuna haja ya watoto wetu kuwaambia someni sana?
Haja ipo kubwa tu.
Lakini swali la kujiuliza, ni wasome kitu gani ili wapate nini!
Mzazi ukimwongoza vizuri mwanao kulijibu swali hili, atafika mbali!
 
Kiko wapi hiki chuo mkuu,nataka nipeleke mtoto wangu
 
Kwa ushauri wako, kwa hizo nafasi 200 ni njia gn itumike ili wenye vigezo waajiriwe
Screen CV upate watu 1000 tu.

Sio unajaza watu 20K unawasafirisha mkoa hadi mkoa for nothing.

Ni uvivi tu ule ule wa kiafrika na kutumia matatizo ya mwenzako kujinufaisha
 
Screen CV upate watu 1000 tu.

Sio unajaza watu 20K unawasafirisha mkoa hadi mkoa for nothing.

Ni uvivi tu ule ule wa kiafrika na kutumia matatizo ya mwenzako kujinufaisha
Kumaanisha hao watakaoachwa n sawa na walienda kupoteza muda chuo?
 
Kuna mtu alisema anawatafutia kazi ya kufundisha kiswahili nje ya nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…