Pre GE2025 Kwa Rais Samia kujifanya "Chura kiziwi" ni dharau kwa watanzania. Kwani yupo Ikulu kwa maslahi ya akina nani?

Pre GE2025 Kwa Rais Samia kujifanya "Chura kiziwi" ni dharau kwa watanzania. Kwani yupo Ikulu kwa maslahi ya akina nani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nyerere siyo msahafu, kwamba kila alichokifanya ama kutamka basi alikuwa yuko sahihi. Nyerere ni miongoni mwa viongozi wabaya kuwahi kutokea ktk nchi hii. Bahati yake ni kuwa alitawala enzi za giza.
Mkuu sisi tuliomuona Mwl.Nyerere hakuwa mtu wa kujibu kila jambo.
Kwanza halikuwa haruhusu kumkosoa yeye kama Raisi anakupeleka detention mapema hakuna mashtaka, ukirudi huko miaka 3 au zaidi msimlie mkeo ulivyovishwa shera.
Pili hata pale akitoa ruksa ya maswali akiona swali lako ni mtego au kumuubua anakwambia kaa chini na matusi mazito mazito,watu wanashangilia sana
Usifikiri yamekwisha subiri usiku unagongewa hodi saa nane usiku na watu wasiojulikana utapelekwa pale pasipojulikana ndio upate adabu.

Pammoja na ukali wa Mwamba Nyerere zaidi ya mara 3 walipanga njama za kumpindua,vijana wa Magomeni waliteka ndege kubwa ya ATC ikiwa na abiria ikapelekwa Uingereza wakidai Nyerere aachie madaraka ya Uraisi.
Baada ya vita ya Kagera wafadhili wake Marekani walimuekea vikwazo vya kiuchumi ukazuka ulanguzi uliokubuu alishindwa kuudhibiti.

Lakini inabidi tujuwe kuwa Raisi kapewa walinzi,kapewa escorts ya magari lukuki,Anatembea kwenye red carpet, anapigiwa mizinga 21,ndio jemedari mkuu akiamrusha vita shughuli inaanza.
Jaji atatoa hukumu ya kifo lakini Raisi ndio mtoa ruksa unyongwe au la.
Uraisi ni taasisi no.1,uraisi hauna ubia.
Wanataka Raisi acheke na nyani ili avune mabuwa?
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Wengine wakafikia kusema alikuwa akiangalia TV Msasani na kuja kutueleza.Je,kulikuwa na mnara Gani uliokuwepo kumwezesha Mwalimu kuangalia TV na kuja kueleza masuala mbalimbali yaliokuwa yanaendelea duniani??
TVZ now ZBC ilianza kurusha matangazo yake mwaka 1967.
 
Rais Samia amekiri kusikia kelele na matusi ya watanzania juu ya sera zake na uongozi wake. Lakini amesema ameamua kujifanya kuwa kama "chura kiziwi" mpaka dhamira yake na lengo lake la litakapotimia.

Katika kauli yake hii nabaini mambo 2:-
1. Ni ule ugonjwa walionao viongozi wengi wa Afrika wa kudhani "cheo ni akili". Hivyo Samia kwa kuwa yeye ni Rais, basi anajiona yeye ndiyo mwenye akili kuliko watanzania wote. Ndiyo maana anapuuza maoni (yeye kayaita kelele) na ukosoaji (matusi) yao.

2. Watanzania wameporwa madaraka yao, hivyo Samia hayuko tena kwenye kiti cha urais ili kuwatumikia. Ndiyo maana kile wanachokitaka kinaitwa kelele na matusi. Kama Rais angekuwa yuko pale kwa kuwatumikia wananchi, basi angefanya kwa kadri wanavyopendekeza.

Siyo mara ya kwanza kwa Samia kutoa kauli ya aina hii. Hata wakati wa sakata la kupinga DP World, alijitokeza na kusema atakaa kimya na kamwe hatojibu chochote. Mwisho wa siku akausaini mkataba wa DP World uliokataliwa na watanzania.

Pia, soma
=>
Rais Samia: Wananitukana ili niwajibu, najigeuza chura siwajibu

Ina maana Rais Samia anawadharau wananchi? Ni wale watu wa kusema, 'siwasikilizi, nitafanya ninavyotaka, kwani mtanifanya nini?".

Nchi inamhitaji Rais ambaye yipo kwaajili ya kuwasikiliza wananchi na kutenda yale ambayo, wananchi katika ujumla wao, wanayataka. Siyo mtu anayewapuuza.
 
Unapokuwa Rais ni lazima uwe na msimamo alichosema leo SSH Hakina tofauti na ile hotuba ya Mwalimu Nyerere ya kiongozi kutosikiliza maneno mengi kutoka kila
Upande, “ huyooo , huyooo” lakini Rais anabakia na msimamo ulioimara na usiotetereka.

Hakuna Rais mwenye kutekeleza kila analolisikia kutoka kwa kila mtu, atafeli mapema sana Rais mwenye hulka hiyo.
Upo sahihi na hupo sahihi pia. Kiongozi unatakiwa kusikiliza lakini huwezi kulifanyia kazi kila unalolisikia. Kiongozi hutakiwi kuw kiziwi, kipofu wala bubu. Unatakiw kusikiliza, kutazama, kuchunguza, kufanya maamuzi, na kutoa kauli kwa nini umefanya maamuzi ya aina fulani na siyo vinginevyo.
 
Mamilioni ya watanzania wanamuunga mkono Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi.hawataki kuona Rais wetu akijibu uzushi ,utoto utoto na uongo wa kupikwa unaokuwa ukitolewa na wanasiasa uchwara waliofirisika na kuishiwa hoja. Wapinzani janja yenu mlitaka muwe mnazusha vitu vya uongo ili muwe mnajibiwa kuwaweka midomoni.

Sasa Rais hana muda huo mchafu wa kujibu uzushi na uongo .yupo Bize kuwatumikia watanzania na kuwaletea maendeleo,kazi ambayo ndio tuliyomkabidhi na kumpatia.hatumlipi mshahara kukaa ikulu kwa ajili ya kujibu uzushi wa wanasiasa uchwara wa CHADEMA
Mzee wa mamilion, vp hawajabubujikwa na machozi?
 
Yaani Samia sijui amefikiria nini! Yaani katika vyote, kamwona chura ndiye kiumbe mzuri wa kumuiga!!
Mimi nawaza tu hilo jina likitumika kama aka yake. Simba fc itabidi wewe waangalifu kwenye kulitumia wanapowatania Yangafc
 
  • Kicheko
Reactions: G4N
Unapokuwa Rais ni lazima uwe na msimamo alichosema leo SSH Hakina tofauti na ile hotuba ya Mwalimu Nyerere ya kiongozi kutosikiliza maneno mengi kutoka kila
Upande, “ huyooo , huyooo” lakini Rais anabakia na msimamo ulioimara na usiotetereka.

Hakuna Rais mwenye kutekeleza kila analolisikia kutoka kwa kila mtu, atafeli mapema sana Rais mwenye hulka hiyo.
👍👌👏🤝
 
Naanza kupata ukakasi kulitumia hili neno, japokuwa lilikuwa neno langu pendwa
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Watu wanaomtukana hawafanyi hivyo kukosoa bali mitusi ya nguoni. Mfano mange anasema semia anasagana. Sasa unataka ajibu upuuzi wa mange na upuuzi wa lisu. Keep calm mama ni jibu la wapumbavu akina lisu
What if hajajibu kwa sababu ni kweli Mkuu!
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Hawa Watanzania siyo wa kuwasikia sana kwa kuwa hawajui wanachikitaka. Rais Samia shika hapo hapo, fanya yale unaona yana tija kwa Taifa.

Nchi hii ina wajinga sana. Magufuli alibana demokrasia, aka sigina katiba, akaminya uhuru wa kujieleza, akaua wapinzani, akafilisi matajiri ila Mungu akatusaidi kwa kumtupa jehanam.

Amekuja Samia mnamtukana tu kwa uhuru aliowapa,
Mkuu yote uliyo sema ni mazuri and nobody is denying that. Wananchi wanacho sema ni kuwa hali ya uchumi wao ni mbaya mno mtaani na mfukoni!

Wanasema hawaoni unafuu wowote kiuchumi Mkuu, Hawaoni tofauti ya ugumu wa maisha licha ya mazuri hayo uliyo ya taja.
 
Nyerere siyo msahafu, kwamba kila alichokifanya ama kutamka basi alikuwa yuko sahihi. Nyerere ni miongoni mwa viongozi wabaya kuwahi kutokea ktk nchi hii. Bahati yake ni kuwa alitawala enzi za giza.
👍👌👏🤝🙋‍♂️
 
Back
Top Bottom