sblandes
JF-Expert Member
- Apr 25, 2010
- 6,632
- 4,737
Mkuu sisi tuliomuona Mwl.Nyerere hakuwa mtu wa kujibu kila jambo.Nyerere siyo msahafu, kwamba kila alichokifanya ama kutamka basi alikuwa yuko sahihi. Nyerere ni miongoni mwa viongozi wabaya kuwahi kutokea ktk nchi hii. Bahati yake ni kuwa alitawala enzi za giza.
Kwanza halikuwa haruhusu kumkosoa yeye kama Raisi anakupeleka detention mapema hakuna mashtaka, ukirudi huko miaka 3 au zaidi msimlie mkeo ulivyovishwa shera.
Pili hata pale akitoa ruksa ya maswali akiona swali lako ni mtego au kumuubua anakwambia kaa chini na matusi mazito mazito,watu wanashangilia sana
Usifikiri yamekwisha subiri usiku unagongewa hodi saa nane usiku na watu wasiojulikana utapelekwa pale pasipojulikana ndio upate adabu.
Pammoja na ukali wa Mwamba Nyerere zaidi ya mara 3 walipanga njama za kumpindua,vijana wa Magomeni waliteka ndege kubwa ya ATC ikiwa na abiria ikapelekwa Uingereza wakidai Nyerere aachie madaraka ya Uraisi.
Baada ya vita ya Kagera wafadhili wake Marekani walimuekea vikwazo vya kiuchumi ukazuka ulanguzi uliokubuu alishindwa kuudhibiti.
Lakini inabidi tujuwe kuwa Raisi kapewa walinzi,kapewa escorts ya magari lukuki,Anatembea kwenye red carpet, anapigiwa mizinga 21,ndio jemedari mkuu akiamrusha vita shughuli inaanza.
Jaji atatoa hukumu ya kifo lakini Raisi ndio mtoa ruksa unyongwe au la.
Uraisi ni taasisi no.1,uraisi hauna ubia.
Wanataka Raisi acheke na nyani ili avune mabuwa?