Pre GE2025 Kwa Rais Samia kujifanya "Chura kiziwi" ni dharau kwa watanzania. Kwani yupo Ikulu kwa maslahi ya akina nani?

Pre GE2025 Kwa Rais Samia kujifanya "Chura kiziwi" ni dharau kwa watanzania. Kwani yupo Ikulu kwa maslahi ya akina nani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Siyo kweli mange ni kisingizio tu. Dp world waraka umesomwa kila kitongoji. Hata katikati ya tusi moja la mange kuna hoja kibao na ukosoaji mwingi ambao unajenga anatoa. Rais mwenye kujali utawala bora angetuliza mizuka na kuyafanyia kazi hayo yanayopigiwa kelele na watanzania.
👍👌👏🤝🙋‍♂️🛡️
 
Prezda akijigeuza chura manake ikulu inakuwa inaongozwa na frogi sio?
Anayejua tabia za 🐸 atujuze tafazali...
Kurukaruka,makelele hasa usiku,kukaa madimbwini,ulimi mreefu....
🤣 🤣 🤣
 
Rais yuko sahihi kabisa. Asipoteze muda kuwajibu kina Pumbulu, Mdude na wapinzani wengine wasio na hoja. Akianza kujishughulisha kuwajibu atageuka dikteta. Anaepusha mengi sana
 
Kiukweli nilisha wai kushangazwa na ukimya wa Samia hasa nilipo angalia mamlaka yake na jinsi watu wanavyo mwongelea na namna wanavyo mwongelea with fear less

Hakili yangu ikaniambia huyu president anakitu Cha ziada zaidi ya jamii yetu unavyo mchukulia

Ana hakili

Ana subila

Anajiamini na ndio maana kafika hapo alipo

Kwa kifupi Samia Ana hueka za kiume japo ni mwanamke

Nime jalibu kum compare na jpm nimejikuta namwona jpm ni samia af Samia ni jpm

Kiukweli president tunae ila wasaidizi zake ni watu wabaya Sana kwake kwani..

Hawapendi mafanikio yake

Hawa pendi kuinuka kwake

Wana chukia juhudi zake kwa inchi na watu wake kwani hawataki aje kuwa mfano kwa vizazi vijavyo

Kiukweli Samia Hana ubaya na Tanzania ila wenye nia mbaya na Tanzania wana jitahidi kumfaya Samia awe mbaya kwa wa tanzania
 
Mkuu sisi tuliomuona Mwl.Nyerere hakuwa mtu wa kujibu kila jambo.
Kwanza halikuwa haruhusu kumkosoa yeye kama Raisi anakupeleka detention mapema hakuna mashtaka, ukirudi huko miaka 3 au zaidi msimlie mkeo ulivyovishwa shera.
Pili hata pale akitoa ruksa ya maswali akiona swali lako ni mtego au kumuubua anakwambia kaa chini na matusi mazito mazito,watu wanashangilia sana
Usifikiri yamekwisha subiri usiku unagongewa hodi saa nane usiku na watu wasiojulikana utapelekwa pale pasipojulikana ndio upate adabu.

Pammoja na ukali wa Mwamba Nyerere zaidi ya mara 3 walipanga njama za kumpindua,vijana wa Magomeni waliteka ndege kubwa ya ATC ikiwa na abiria ikapelekwa Uingereza wakidai Nyerere aachie madaraka ya Uraisi.
Baada ya vita ya Kagera wafadhili wake Marekani walimuekea vikwazo vya kiuchumi ukazuka ulanguzi uliokubuu alishindwa kuudhibiti.

Lakini inabidi tujuwe kuwa Raisi kapewa walinzi,kapewa escorts ya magari lukuki,Anatembea kwenye red carpet, anapigiwa mizinga 21,ndio jemedari mkuu akiamrusha vita shughuli inaanza.
Jaji atatoa hukumu ya kifo lakini Raisi ndio mtoa ruksa unyongwe au la.
Uraisi ni taasisi no.1,uraisi hauna ubia.
Wanataka Raisi acheke na nyani ili avune mabuwa?
Mkuu kuna jambo ulitaka kulisema ila umelipotezea katikati ya hoja yako.

Hujaeleweka ulitaka kusema nini!!

Kimsingi huwezi kuunga hoja na kuipinga at the same time kwenye andiko lako!!!
 
Mamilioni ya watanzania wanamuunga mkono Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi.hawataki kuona Rais wetu akijibu uzushi ,utoto utoto na uongo wa kupikwa unaokuwa ukitolewa na wanasiasa uchwara waliofirisika na kuishiwa hoja. Wapinzani janja yenu mlitaka muwe mnazusha vitu vya uongo ili muwe mnajibiwa kuwaweka midomoni.

Sasa Rais hana muda huo mchafu wa kujibu uzushi na uongo .yupo Bize kuwatumikia watanzania na kuwaletea maendeleo,kazi ambayo ndio tuliyomkabidhi na kumpatia.hatumlipi mshahara kukaa ikulu kwa ajili ya kujibu uzushi wa wanasiasa uchwara wa CHADEMA
Nilikuwa nataka usije huku maana utaharibu ila ushakuja wacha twende
Wananchi wapi watanzania au watu wanaojiita watanzania huu sio
 
Mkuu kuna jambo ulitaka ulisema ila umepotezea katikati ya hoja yako. Mkuu huwezi kuunga hoja na kuipinga at the same time kwenye andiko lako!!!
Mkuu life is like magazine.
In short President ni Mungu.
 
Nafikiri Rais hakumaanisha kutosikiliza hoja na malalamiko ya wananchi.Amezungimzia kuwa "chura" kwa wale wasio na adabu kwenye kauli zao.Utakuta mtu anasema hovyo kwenye suala asilolielewa au kulikuwa.Wale wanaofuata mkumbo wa maneno,wasiojielewa na wasiotaka kutafiti ukweli.Ndio anaowazungumzia.

Tanzania Kuna ugomjwa mmoja mbaya na hatari kwa afya ya akili.
Mifano kadhaa kama hii ndio utajua Kuna tatizo.Ukiweka kando utawala wa Mwalimu Nyerere,
1) Wakati wa Utawala wa Marehemu Mzee Mwinyi,Kila kilichoonekana kipya mahali iwe kiwanda,hoteli,kituo Cha mafuta n.k,tuliaminishwa na "wasemaji wasio rasmi" kwamba ni vya Mama Sitti Mwinyi.Wakati wake wa uongozi ukamalizika.Sina hakika Leo ukiwauliza juu ya walichoaminishwa kama kipo.
2)Ukaja utawala wa Marehemu Mzee Benjamin Mkapa.Mchezo wa maneno ukawa ule ule Kila kipya mjini ni vya Anna Mkapa! Utawala ukamaliza muda wake.Sijui Kuna ukweli upi.
3)Ukaimgia utawala wa Mzee Jakaya Kikwete.Movie ikawa ileile.Kila kipya mjini ni vya Ridhwani Kikwete na kiasi Mama Salma Kikwete.Nasema Sina hakika kama Kuna ukweli wowote au ni "kwa mujibu wa lile kundi la.wasemaji wasio rasmi".Utawala ukamalizika.
4) Ukaingia utawala wa John Magufuli.Yamesemwa mengi.Hapa sijui ukweli ni upi,pamoja na utofauti wa maoni ya wasemaji wasio rasmi!
Safari ya utawala wa Magufuli aka Jiwe uliishia njiani kabla ya wakati.
5)Sasa tuna utawala wa Mama Samia Suluhu Hassan.Episode imebadilika kidogo.Amegeuka kuwa muuzaji wa Kila kitu.Tuliaminishwa bandari YOTE imeuzwa pamoja na anga na Kila kitu.Ukawa mjadala uliowachanganya watu hasa wale wanaodakia mambo hewani! Wengine walidiriki kusema kwamba Waarabu watajaa mjini na hatutapumua.Sina hakika kama Hilo lipo.
Mwanzoni niliepuka kuzungumzia utawala wa awamu ya kwanza.Na sababu kubwa wakati ule nchi ilikuwa na adabu.Wapo wliosema Mwalimu aliwabana watu katika elimu na mambo kadhaa kiuchumi.
Lakini tujikumbushe kihistoria nchi hii ilishatawaliwa na Wazungu.
Mjerumani 1885-1918 na Muingereza 1918-1961.Miaka 76 ya utawala wenye Bunge(wakati huo lilijulikana kama Baraza la kutunga Sheria),Jeshi,mahakama n.k.
Utawala wa miaka 76 ya mzungu!
Mwaka 1961 wakati Mwalimu anachukua utawala alikuta viwanda havizidi vinne kama sio vitatu! Tanganyika Packers,TPC,Amboni (Mkonge).
Madaftari wawili Watanganyika na mmojawapo alifariki mara baada ya Uhuru.
Walijua kusoma na kuandika walikuwa wachache.Akaanzisha taasisi ya elimu ya watu wazima,sera ya UPE na kiwanda Cha kutengeneza vifaa vya elimu Tanzania Elimu Supplies.Ujenzi wa viwanda mbali mbali bila kusahau reli ya Tazara akishirikiana na Zambia.Yapo mengi.Lakini Bado wasemaji wasio rasmi watasema alikuwa anadanganya watu kwamba kaota mambo Fulani na akaja kuwahutubia! Wengine wakafikia alikuwa akiangalia TV Msasani na kuja kutueleza.Je,kulikuwa na mnara Gani uliokuwepo kumwezesha Mwalimu kuangalia TV na kuja kueleza masuala mbalimbali yaliokuwa yanaendelea duniani?? Au ni kwamba kama Mkuu wa nchi aliweza kupata taarifa kwa njia mbalimbali na baada ya uchambuzi kuwaeleza wananchi?
Mwacheni Mama Samia awe chura kama alivyosema!
🙋‍♂️👌👍👏🤝🛡️
 
Mkuu kuna jambo ulitaka ulisema ila umepotezea katikati ya hoja yako. Mkuu huwezi kuunga hoja na kuipinga at the same time kwenye andiko lako!!!
Ahsante sana. Matapeli wamezidi sana siku hizi, hasa huku kwenye mitandao amabako watu hawajulikani ni akina nani..
Huyu kapiga soga zake hapa, na mwisho kasahau alichonuia kuwasilisha kwa wasomaji wake.
Sijui kama kweli alinuia kumlinganisha Nyerere na Samia, katika jambo lolote lile!
 
Upo sahihi na hupo sahihi pia. Kiongozi unatakiwa kusikiliza lakini huwezi kulifanyia kazi kila unalolisikia. Kiongozi hutakiwi kuw kiziwi, kipofu wala bubu. Unatakiw kusikiliza, kutazama, kuchunguza, kufanya maamuzi, na kutoa kauli kwa nini umefanya maamuzi ya aina fulani na siyo vinginevyo.
🙋‍♂️👌👍👏🤝🛡️
 
Kiukweli nilisha wai kushangazwa na ukimya wa Samia hasa nilipo angalia mamlaka yake na jinsi watu wanavyo mwongelea na namna wanavyo mwongelea with fear less

Hakili yangu ikaniambia huyu president anakitu Cha ziada zaidi ya jamii yetu unavyo mchukulia

Ana hakili

Ana subila

Anajiamini na ndio maana kafika hapo alipo

Kwa kifupi Samia Ana hueka za kiume japo ni mwanamke

Nime jalibu kum compare na jpm nimejikuta namwona jpm ni samia af Samia ni jpm

Kiukweli president tunae ila wasaidizi zake ni watu wabaya Sana kwake kwani..

Hawapendi mafanikio yake

Hawa pendi kuinuka kwake

Wana chukia juhudi zake kwa inchi na watu wake kwani hawataki aje kuwa mfano kwa vizazi vijavyo

Kiukweli Samia Hana ubaya na Tanzania ila wenye nia mbaya na Tanzania wana jitahidi kumfaya Samia awe mbaya kwa wa tanzania
👍👏🤝🙋‍♂️💐🛡️
 
Nyerere siyo msahafu, kwamba kila alichokifanya ama kutamka basi alikuwa yuko sahihi. Nyerere ni miongoni mwa viongozi wabaya kuwahi kutokea ktk nchi hii. Bahati yake ni kuwa alitawala enzi za giza.
Kiongozi mzuri hana hata huo muda wa kusikiliza au kusoma kile ambacho mimi na wewe tunaandika huku jamii forum.
 
Upo sahihi na hupo sahihi pia. Kiongozi unatakiwa kusikiliza lakini huwezi kulifanyia kazi kila unalolisikia. Kiongozi hutakiwi kuw kiziwi, kipofu wala bubu. Unatakiw kusikiliza, kutazama, kuchunguza, kufanya maamuzi, na kutoa kauli kwa nini umefanya maamuzi ya aina fulani na siyo vinginevyo.
Rais anafanya kazi na team ya washauri.

Urais ni taasisi katika ukamilifu wake.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Back
Top Bottom