Nafikiri Rais hakumaanisha kutosikiliza hoja na malalamiko ya wananchi.Amezungimzia kuwa "chura" kwa wale wasio na adabu kwenye kauli zao.Utakuta mtu anasema hovyo kwenye suala asilolielewa au kulikuwa.Wale wanaofuata mkumbo wa maneno,wasiojielewa na wasiotaka kutafiti ukweli.Ndio anaowazungumzia.
Tanzania Kuna ugomjwa mmoja mbaya na hatari kwa afya ya akili.
Mifano kadhaa kama hii ndio utajua Kuna tatizo.Ukiweka kando utawala wa Mwalimu Nyerere,
1) Wakati wa Utawala wa Marehemu Mzee Mwinyi,Kila kilichoonekana kipya mahali iwe kiwanda,hoteli,kituo Cha mafuta n.k,tuliaminishwa na "wasemaji wasio rasmi" kwamba ni vya Mama Sitti Mwinyi.Wakati wake wa uongozi ukamalizika.Sina hakika Leo ukiwauliza juu ya walichoaminishwa kama kipo.
2)Ukaja utawala wa Marehemu Mzee Benjamin Mkapa.Mchezo wa maneno ukawa ule ule Kila kipya mjini ni vya Anna Mkapa! Utawala ukamaliza muda wake.Sijui Kuna ukweli upi.
3)Ukaimgia utawala wa Mzee Jakaya Kikwete.Movie ikawa ileile.Kila kipya mjini ni vya Ridhwani Kikwete na kiasi Mama Salma Kikwete.Nasema Sina hakika kama Kuna ukweli wowote au ni "kwa mujibu wa lile kundi la.wasemaji wasio rasmi".Utawala ukamalizika.
4) Ukaingia utawala wa John Magufuli.Yamesemwa mengi.Hapa sijui ukweli ni upi,pamoja na utofauti wa maoni ya wasemaji wasio rasmi!
Safari ya utawala wa Magufuli aka Jiwe uliishia njiani kabla ya wakati.
5)Sasa tuna utawala wa Mama Samia Suluhu Hassan.Episode imebadilika kidogo.Amegeuka kuwa muuzaji wa Kila kitu.Tuliaminishwa bandari YOTE imeuzwa pamoja na anga na Kila kitu.Ukawa mjadala uliowachanganya watu hasa wale wanaodakia mambo hewani! Wengine walidiriki kusema kwamba Waarabu watajaa mjini na hatutapumua.Sina hakika kama Hilo lipo.
Mwanzoni niliepuka kuzungumzia utawala wa awamu ya kwanza.Na sababu kubwa wakati ule nchi ilikuwa na adabu.Wapo wliosema Mwalimu aliwabana watu katika elimu na mambo kadhaa kiuchumi.
Lakini tujikumbushe kihistoria nchi hii ilishatawaliwa na Wazungu.
Mjerumani 1885-1918 na Muingereza 1918-1961.Miaka 76 ya utawala wenye Bunge(wakati huo lilijulikana kama Baraza la kutunga Sheria),Jeshi,mahakama n.k.
Utawala wa miaka 76 ya mzungu!
Mwaka 1961 wakati Mwalimu anachukua utawala alikuta viwanda havizidi vinne kama sio vitatu! Tanganyika Packers,TPC,Amboni (Mkonge).
Madaftari wawili Watanganyika na mmojawapo alifariki mara baada ya Uhuru.
Walijua kusoma na kuandika walikuwa wachache.Akaanzisha taasisi ya elimu ya watu wazima,sera ya UPE na kiwanda Cha kutengeneza vifaa vya elimu Tanzania Elimu Supplies.Ujenzi wa viwanda mbali mbali bila kusahau reli ya Tazara akishirikiana na Zambia.Yapo mengi.Lakini Bado wasemaji wasio rasmi watasema alikuwa anadanganya watu kwamba kaota mambo Fulani na akaja kuwahutubia! Wengine wakafikia alikuwa akiangalia TV Msasani na kuja kutueleza.Je,kulikuwa na mnara Gani uliokuwepo kumwezesha Mwalimu kuangalia TV na kuja kueleza masuala mbalimbali yaliokuwa yanaendelea duniani?? Au ni kwamba kama Mkuu wa nchi aliweza kupata taarifa kwa njia mbalimbali na baada ya uchambuzi kuwaeleza wananchi?
Mwacheni Mama Samia awe chura kama alivyosema!