Hizi tozo unazoziona ni kielelezo cha uadilifu wa mama Samia. Angekuwa mtu mwingine angekuwa analalamika hadharani na kusema nchi imefilisika hakuna kitu hazina. Kila mtu alikuwa anaidai serikali kuanzia watumishi, askari, wakandarasi, suppliers, wastaafu, wananchi na kila mtu. Jamaa alikuwa derever wa lori haangalii nyuma yeye ni reli, bwawa, barabara na kanda ya ziwa tu. Kama sio hizi tozo hata yeye angenyooka tu na huenda angeshaacha au kuachishwa kibarua.
Miradi mingine inalazimu aichomolee betri ili na mambo mengine yaende. Jamaa yetu alikuwa na miradi ya majukwaani isiyokuwa na uhalisia, alitembea na noti mfukoni ili kujipatia sifa za bei rahisi kama vile kununua jogoo kwa laki moja, mahindi ya kuchoma kwa sh. 10,000 kila moja huku wastaafu wakigalagala kwa kukosa stahiki zao.