Kwa Rais Samia nchi inakwenda bila makelele

Alhamdu lilahi yaani lami zinamiminwa HUKU kwetu siamini macho yangu yaani barabara zinatenhenezwa hakuna MASKHARA
 
Pro magu hamna jema / MWAJITIA UPOFU.HAMUONI MAZURI YANAYOENDELEA,MAKWEPA KODI WENGI YAMEUMIZWA SANA ULIPAJI WA KODI NA TOZO MBALI KWA WOTE.
 
Naona ushapewa uji wa ulezi unasinzia tu saizi ...huna budi kuandika utopolo
 
Hizi tozo unazoziona ni kielelezo cha uadilifu wa mama Samia. Angekuwa mtu mwingine angekuwa analalamika hadharani na kusema nchi imefilisika hakuna kitu hazina. Kila mtu alikuwa anaidai serikali kuanzia watumishi, askari, wakandarasi, suppliers, wastaafu, wananchi na kila mtu. Jamaa alikuwa derever wa lori haangalii nyuma yeye ni reli, bwawa, barabara na kanda ya ziwa tu. Kama sio hizi tozo hata yeye angenyooka tu na huenda angeshaacha au kuachishwa kibarua.

Miradi mingine inalazimu aichomolee betri ili na mambo mengine yaende. Jamaa yetu alikuwa na miradi ya majukwaani isiyokuwa na uhalisia, alitembea na noti mfukoni ili kujipatia sifa za bei rahisi kama vile kununua jogoo kwa laki moja, mahindi ya kuchoma kwa sh. 10,000 kila moja huku wastaafu wakigalagala kwa kukosa stahiki zao.
 
Una maana Magufuli alikuwa vuvuzela?
 
Mmmmh! kelele zilizopita zilizidi bhana, huku yeye, kule makonda, kwakule Sabaya, na upande ule Gambo, na huku Tabora yuko Mwanri soma iyoooo, kule dodoma kuna afande mtapata tabu saaana, camera za barabarani ndo usiseme na kule wanahanikiza kwa vifijo vya kudhalilisha viongozi wakitumbuliwa kadamnasi nna matusi ya nguoni juu.
 
Mkuu yeye ndo ameuwa nchi muda mfupi sana, mnajipa moyo kwa sababu ya posho zinazowaneemesha wachache, generly Tanzania kwisha kabisa habari yake hakuna uchumi kukua wala ajira , shaghala baghala tu miripuko ya bei chakula kila kitu tafran maji, barabara , nothing new., CCM miaka 60 waliyoishi madarakani imetosha bila, Watanzania wanataka fyagio jipya.
 
Anatuumiza kimya kimya
Hakuna namna kama mnataka mamiradi makubwa ya babu yenu ya Dodoma, reli na bwawa yaendelee kujengwa, samia hana miujiza. Jamaa yetu alikuwa anayajenga kwa kunyang'anya watu hela zao, samia hawezi kunyang'anya watu kwa kuwatumia akina Sabaya na TRA. sabaya alikiri kutumwa kunyang'anya watu pesa zao ziende hazina. Ni heri njia hii ya tozo kuliko unyang'anyi.
 
Tajiri atabaki kuwa tajiri na masikini atabaki kuwa masikini.ndicho nilichogundua.
 

Vipi tena. CCM yenye ilani yake haitambuliwi rasmi? Rais peke yake ndio mtu au taasisi ya maana?
 
Vipi tena. CCM yenye ilani yake haitambuliwi rasmi? Rais peke yake ndio mtu au taasisi ya maana?
Awamu ya Tano haikuitambua CCM, CCM imepoteza mvuto, wakiona nyuki wanapita angani wanaimba "nyuki nenda kaingie kwenye mizinga ya Babu tulambe asali" . CCM Ina makundi yanayosubiri nyuki waingie kwenye mizinga ya babu Yao. Yaani kila kundi linafaidika kama mtu wao akikamata madaraka.
 
Nilijua naongea na mtu ana upeo wa akili, kumbe ni wale watu reject miongoni mwa watu.

Magu alikuwa anabadili nchi kwenda upande ambao huwez kuuona na hutakaa uuone kwa sabab umezingirwa hapo ulipo na utaona hapo ulipo na si vinginevyo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…