Kwa ramani hii mkoa wa Chato utatokea wapi?

Hapa tunaeleweshana vigezo vinavyotumika kugawa mkoa na si kushindana kwa kutukanana kama unavyofanya. Kama huwezi kushindana kwa hoja basi kaa kimya.
Huwezi kumuelesha mtu kama hujui namna ya kumuelewesha. Kutojua kwako kuandika maneno rahisi ya kiswahili kunaathiri uwezo wako wa kumfundisha mtu.
 
Pasipo kupotoshana,mkoa wa Chato, utajumuisha wilaya hizi: Ngara,Biharamulo, Bukombe,Kakonko na Chato yenyewe. Chuki tu, ndo zinafanya mgogoro huu kuwepo na zaidi kukuzwa kupita kiasi, hasa kwa wasiyojua taabu anayoipata mtu wa Ngara kwenda Bukoba makao makuu ya mkoa wa Kagera, kupata huduma za ana kwa ana.
 
Tabora na morogoro ndiyo inatakiwa Lindi ina eneo kubwa lakini ni poli tu ila chato ule ni ujinga kabisa
Lakini pia ccm wanagawa gawa mikoa ili kiwe nini?
CCM ni kansa. Wanaongeza gharama tu.
 
Kwenye Kibondo, weka Kakonko
 
Sijajua kwanini Mwendazake alikazania kuipandisha hadhi Chato kwa kasi namna ile, kwa jicho la mbali nik kama Chato ilikuwa inakwenda kudai mamlaka kamili vile😆😅😂🤣kama maswahiba Burundi na Rwanda
Mimi sioni tatizo,chato,ichukue wilaya moja moja toka Tabora,morogoro na lindi,,,case closed..😒😒
 
Hivi wewe kwa akili yako ndoho tu wilaya ya Kakonko iko geita biharamlo na Ngala zipo geita? Kwa nini zikachukuliwe wilaya za mikoa mingine ili kuunda kamkoa kwa ajili tu ya mtu mmoja? Na Dar haikumegwa tu kwa sababu ya mtu
 
Acheni ushamba,
Kugawanya mikoa hawaangalii ukubwa wa eneo kama wengi wenu vilaza mnavyofikiria.
Wewe ndiyo mshamba mkoa unagawanywa kutokana na ukubwa na sio wingi wa watu kama ingekuwa wingi wa watu basi kungekiwa na mikoa hata 100
 
Enzi za Kikwete kulikuwa na mpango wa kuunda mkoa mpya wa Nzega au Urambo kwa kuugawanya mkoa wa Tabora.

Mkoa wa Tabora ndiyo unatakiwa kugawiwa kwanza, kabla ya kuanzisha Chato!
 
Geita na shinyanga iwe mkoa mmoja,Mwanza na simiyu mkoa mmoja,njombe na Iringa iwe mmoja pia,
Na hii biashara ya kuigawa nchi mpaka lini?lazima tuwe na kikomo,wananchi wakiongezeka wanataka shule,hospitari,nyumba,sio maeneo ya watawala.
Mkuu unajua ulichoandika[emoji28] ? Umenifurahisha sana. Geita na shinyanga kuna mwanza kati kati, inakuaje iwe mkoa afu uruke mwanza ?
 
Kwa maelezo yako ya kuangalia ukubwa wa eneo Dar isingekuwa mkoa au Zanzibar isingekuwa na mikoa mitano. Na kama wanaangalia idadi ya watu na uchumi au mapato ya eneo husika basi Chato inasitahili kuwa mkoa.
Kuanzisha mkoa maana yake ni kusogeza huduma kwa wananchi.

Mkoa wa Tabora ni mkubwa, na una watu wengi mpaka ndani ndani huko.

Tabora inachangia pato la Taifa kupitia Tumbaku.

Tugawe kwanza mkoa wa Tabora, baadae Morogoro, na mwisho Chato!
 
Wafanye tathmini ya jumla wagawe upya mikoa yote kutokana na vigezo sawa waliyoiweka
 
Geita na shinyanga iwe mkoa mmoja,Mwanza na simiyu mkoa mmoja,njombe na Iringa iwe mmoja pia,
Na hii biashara ya kuigawa nchi mpaka lini?lazima tuwe na kikomo,wananchi wakiongezeka wanataka shule,hospitari,nyumba,sio maeneo ya watawala.
Kugawa mikoa hata sio solution ya umaskini ni kuongeza gharama za uendeshaji mfano mkoa wa tabora ndio ni mkubwa ila population ni ndogo na asilimia 90 na kitu ni mapori hayakaliwi na watu kabisa, serikali irahisishe huduma Hadi ngazi za katani na wilayani ili kuepusha wananchi kwenda had mikoani makao makuu.
 
Sijajua kwanini Mwendazake alikazania kuipandisha hadhi Chato kwa kasi namna ile, kwa jicho la mbali nik kama Chato ilikuwa inakwenda kudai mamlaka kamili vile[emoji38][emoji28][emoji23][emoji1787]kama maswahiba Burundi na Rwanda
Acha tuu aise yan Kweli Mungu ni Fundi sana!!! Yan huwa najiuliza angemaliza miaka kumi na ile mingine kumi kutoka kwa "ndugwai" sijui hii nchi ingekuwake!!! Nakosa jibu
 
Aisee! Asante kwa kuja na kielelezo cha ramani. Hata huko TAMISEMI hebu waliangalie hili.

Kuna mikoa mikubwa kuliko hiyo wilaya ya Chato.

Tutaitumia hii ramani kupinga uanzishwaji wa mkoa wa Chato!
Lile jitu ni baya mno
 
Mungu wenu kafa hilo sahau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…