Kwa ramani hii, turekebishe kipi?

Kwa ramani hii, turekebishe kipi?

steph felix

Member
Joined
Jul 26, 2015
Posts
33
Reaction score
21
Habari wanajamii, kwa wale watalaamu wa architecture design na wazoefu wote wa nyumba, nilikuwa naomba ushauri wenu juu ya ramani hii.
IMG_20220625_210432_871.jpg
 
Kwa mawazo yangu hiyo master bedroom sio poa kushare ukuta na hiyo bedroom nyingine. Ukiwa unageggedua no privacy.
Ni Bora kuweka public toilet jirani na Master bedroom halafu vyumba vingine vifate?
 
option nayofikiria hapo ni kwamba wc ya master ndio iwe public toilet, master bedroom iwe chumba cha kawaida. hii public wc ndio iwe wc ya master na master bedroom iwe kwenye hiki chumba cha mwisho
Nimeipenda hii idea. Nitaedit ikae hivyo
 
Habari wanajamii, kwa wale watalaamu wa architecture design na wazoefu wote wa nyumba, nilikuwa naomba ushauri wenu juu ya ramani hii.View attachment 2272067
Mimi sio mtaalamu wala nini ila nilichoona kwa harakaharaka;

1. Sioni public toilet. Kama ni hii huku kushoto katikati ya 2 bedrooms, mi naona itakua ipo mbali sana mtu akibanwa tumbo la kuharisha akiwa dinning mpaka aje afike ameshaachia. Pia nadhani sio vizuri mgeni azunguke nyumba nzima akipita mbele ya kila chumba mpaka afike chooni.

2. Hiyo uliyoita "prayer room" haina dirisha. Mtu akijifungia humo na hili joto sidhani kama ataweza kusali dakika 2. Bora hiyo pray room ungeifanya ndio public toilet uweke kadirisha kale kadogo.

3. Kwa ukubwa wa hiyo nyumba, ka store umekaminya balaa. Kumbuka kibongo bongo hapo store ndio utahifadhi kila kitu kuanzia ma drum ya mahindi, jiko la mkaa, madumu ya maji, baiskeli, kochi lililovunjika, matairi ya gari, ndoo za rangi zilizobaki, cementi nk.

4. Nyumba haina veranda

5.
 
Mawazo mazuri sana, ila tunaweza amisha hiyo public toilet ikawa ile ya master bedroom, halafu mpangilio wa vyumba ukabadilishwa.[emoji1303]
 
Ila niulize, kwa mgeni ambaye anakuja tuu atatumia choo kipi? Hichi cha guest room? Maana sio vizuri public toilet ha wana familia pia wageni watumie
Vyoo vitakua vingi ndani, itabidi cha wapitaji kiwepo nje tu
 
Back
Top Bottom