Hapo wala sijaona ukali wa kauli za Lissu. Nilichoona ni ukali wa hatua zilizochukuliwa dhidi ya Lissu, na serikali ya Magufuli :
1) Kuzuia bunge kumgharimia matibabu. Waziri wa Afya kuna wakati alitamka kwamba serikali iko tayari kugharimia matibabu ya Lissu, popote duniani, ali mradi ndugu zake wapeleke maombi. Hayo yalifanyika lakini serikali ikabadili msimamo. Ilionekana wazi hiyo ni amri ya Magufuli mwenyewe.
2) Serikali kuamuru Polisi wasimamishe uchunguzi dhidi ya tukio la kushambuliwa Lissu. Kwa kawaida Polisi hufungua jalada la uchunguzi na watu mbalimbali huhojiwa. Mfano majirani walioshuhudia tukio. Hapa tunaona polisi wamekataa kuanza uchunguzi, mpaka kwanza wamhoji Lissu mwenyewe na dereva wake. Kwa kauli za Polisi, na hasa IGP, inaonekana kwamba Lissu mwenyewe ndio mtuhumiwa namba moja.
3) Kufuta ubunge wa Lissu katika mazingira yenye utata.
Kwa sababu hizo kuu na zingine nyingi, serikali ya Magufuli inaonekana kumtarget Lissu kama adui na inamshambulia personally, with fatal consequences. Lissu is yet to return fire