SoC02 Kwa sababu 1 + 1 = 3 na 1 + 1 + 1 ni 7; juhudi katika uelekeo sahihi ni lazima

SoC02 Kwa sababu 1 + 1 = 3 na 1 + 1 + 1 ni 7; juhudi katika uelekeo sahihi ni lazima

Stories of Change - 2022 Competition

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2022
Posts
3,644
Reaction score
4,315
Naam, moja ongeza moja ni tatu. Katika juhudi (effort) huwa ipo hivi; zikiunganishwa jitihada zaidi ya moja, matokeo yake huwa ni makubwa kuliko ile jumla yake ya kihesabu tu.

Uliwahi kutokea ubishi huko Ulaya ya karne hizo. Wamiliki wa farasi walibishana kuhusu nini kitatokea endapo farasi wawili wenye uwezo fulani watafungwa kwa pamoja. Kundi moja lilidai watavuta mzigo uleule unaobebwa na farasi mmoja. Kundi jingine likapendekeza kuwa watakuwa na uwezo wakukokota mzigo uliokuwa ni jumla ya mizigo yao ya kawaida. Yaani kihesabu ni ile ya kawaida tu ya 1 + 1 = 2, uwezo wa mara mbili! Wengine walijichagulia namba mbalimbali zilizo kati ya moja na mbili. Mwisho wengineo walichagua namba zilizo zaidi ya mbili mfano uwezo wa mara mbili na robo [2.25] au mara mbili na nusu [2.5].

Jaribio lilipokuja kufanyika cha kushangaza ni kwamba wale farasi wawili walikuwa na uwezo wa kawaida ya farasi watatu! Hapo ndipo ilipothibitika wazi kwamba; moja [1] ongeza [+] moja [1] ni sawa sawia [=] na tatu [3]!

Katika sekta yoyote na nyanja zote za kimaisha, kiuchumi na kimaendeleo hili halikwepeki. Juhudi zote unazoweka katika uelekeo wowote tambua kuwa zina matokeo makubwa mno. Haswa zikijumlishwa na juhudi za watu wengine pia. Mfano: Dereva mmoja anapotoa rushwa na askari mmoja akapokea, matokeo yake katika usalama barabarani ni mabaya kwa zaidi ya hao watu wawili tu. Watu wengi wataathirika. Lakini pia ikitokea dereva mmoja na askari mmoja tu wakakataa rushwa; basi myororo wa matokeo mazuri utaathiri watu wengi utashangaa!

Hata katika mahusiano ya aina zote; Iwe ni mahusiano ya kikazi, kirafiki, kindugu, kindoa au kimapenzi. Tambua kuwa matendo yote unayofanya yanajijumuisha kwa athari kubwa zaidi ya hicho kitukio ‘kidoogo’. Neno unalotumia, jicho unavyoangalia na midomo ulivyoiweka unavyoongea yote ni juhudi zinazojenga au kubomoa.

Hivyo basi matendo yote yanayofanyika ni juhudi zinazojijumuisha kwa kasi kubwa kuelekea uelekeo uliouchagua. Ni vizuri kabla ya kila kitendo kujiuliza; JE? Hiki ninachokiamua kipo katika uelekeo gani?;

Mwanasiasa: Je, Mkataba huu ninaousaini ni juhudi kuelekea maendeleo au la?

Mpenzi: Je, Kitendo ninachokifanya ni juhudi kuelekea ndoa au la?

Mwanandoa: Je, Hiki ninachokifanya ni juhudi kuelekea familia bora au la?

Daktari: Je, Kitendo ninachokifanya ni juhudi kuelekea afya ya jamii au la?

Mpigakura pia jitathmini, kwa kutambua kuwa kura unayotoa kwa upande wowote katika uchaguzi inaupa ushindi huo upande unaoupendelea. Kura unayopiga katika makala hizi za mabadiliko zina maana kubwa sana kwetu washiriki. Nitangulize shukrani kwa kura yako lakini malizia kusoma kwanza ndipo ukamilishe kupiga.

Hadi pale ambapo tutatambua na kukubali binafsi kuwa 1 + 1 = 3, 1 + 1 + 1 = 7 na 1 + 1 + 1 + 1 = 25 na zaidi na zaidi basi tutakuwa makini zaidi na juhudi zetu. Amini kwamba juhudi hizo ndogondogo zinacheza kwa nafasi kubwa kuyapeleka maisha katika uelekeo husika. Kwa nafasi yako popote ulipo unaalikwa kuwa kani ya mabadiliko chanya. Karibu tuijenge kesho njema tunayoitamani.

Taz: Jedwali linaloonesha uhusiano kati ya juhudi na matokeo.

Effort vs results n!+1.JPG

Yaani idadi imechukuliwa kama jumla ya juhudi moja moja kama jedwali linavyoonesha👇
Juhudi na matokeo n!+1.JPG


Baada ya kuwa tumejionea huo uhalisia wa mambo katika kujumulisha. Hata katika mahesabu mengine mambo sio rahisi tu kama moja kutoa moja ni sifuri [1 – 1 = 0]. Unaweza kukuta katika mambo ya kipekee [mfano watu wa kipekee, mke, mtoto au mpendwa] ukifanya moja kutoa moja unapata matokeo hasi yaani 1 – 1 = -1. Chukulia kifo cha mpendwa wako, huwa anaacha pengo [-1] tena hata ikatokea akapatikana mpendwa mwingine bado utakuta kuna hesabu tata zaidi kama mtu anakuwa na + 1 + -1 na haisolviki kuwa sifuri!

Ukifuatilia hata hesabu za kugawanya mambo nazo huwa sio rahisi tu hasa utakapofanya kazi na vitu/hali ambazo huwa ni za kipekee. Niliwahi kuzungumzia kuhusu uumbaji wa jambo jipya kwa kuigawanya sifuri na kupata mambo mapya penyewe hesabu yake ilikuwa 0/2 = -1 + 1 + 0! Achana na yule aliyekufundisha kuwa sifuri haiwezi kugawia mbili, kubali kujifunza tena.

Mambo mapya yanayojengwa kwa muoano kamili wa vitu mbalimbali au mgawanyo wake huwa katika namna ambayo akili iliyo kawaida sana haiwezi kun’gamua. Mfano rahisi ni suala sahili tu la maji. Ona kila mmoja anafahamu kuwa maji huzima moto bila ubishi. Sasa kama tuking’ang’ana na suala la kwamba moja ongeza moja ni mbili tu na si vinginevyo hatutaweza kutoboa.

Maji [H20] yameundwa kwa dutu za kipekee za hydrojeni mbili na oksijeni moja. Oksijeni ikiwa peke yake inayo sifa ya kuchochea moto kuwaka. Na haidrojeni yenyewe ndiyo kabisaa, sio kuwaka tu bali huwa na ile tamaa ya kulipuka! Sasa pigia mahesabu uunganishe hivyo vitu viwili moto/mlipuko wake utakuweje? Lakini cha kustaajabisha vimeungana na matokeo yake badala ya kulipuka ndiyo kwanzaa vinazima moto. Hii ni kwa sababu kilichopo hivi sasa ni kitu kipya cha tatu ambacho nacho kina sifa na tabia zake na kinayaishi maisha yake binafsi.

Naomba kuhitimisha kwa kusema: Tuitambue nafasi kubwa tuliyonayo katika kuathiri mambo. Juhudi na vitendo vidogo vidogo vinayo maana kubwa pindi vinapojumuishwa. Lakini pia kila tunapokosa kutenda athari zake ni zaidi ya sifuri kwa kuwa ndogo zaidi[ yaani zaidi ya hasi moja]. Kubeba majukumu ni sifa yetu wanadamu maana tunawajibika kwa kila tunachokifanya.

Kila mmoja ajipime na atambue ukweli kwamba; Kuamini kuwa mambo hutokea tu menyewe ni filosofia mbovu kabisa kuishi nayo. Kuamini kuwa mambo hutokea kwa sababu huleta afya. Na chenye afya zaidi ni kuishi kwa kuamini kuwa sisi [sote] ndio hufanya mambo yatokee. Kwa kuwa kimsingi yule mwenye majukumu/wajibu mkubwa zaidi ndiye mwenye nguvu zaidi [Taz: avatar yangu].​
 
Upvote 0
Last chance ya kupitiapitia haya madini na kutia kura..... shindano linaisha hili wakuu
 
Back
Top Bottom