Kwa sababu hizi nitawahamasisha wananchi kutokwenda kuipigia kura katiba inayopendekezwa.

ligera

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2014
Posts
2,646
Reaction score
1,171
Humu JF ukiangalia comment zote za members zinaonesha ni dhahiri watu wana mapenzi na nchi yao ndiyo maana nimekuja na thread inayotutaka sisi wanaJF kushiriki katika kutoa elimu kwa watanzania kama yafanyavyo makundi mengine mbalimbali kama CWT, TEC, n.k.

Ni sisi tu wanaJF hatujatoa tamko kuhusu zoezi zima la upigaji wa kura kwa katiba hiyo.

Ushauri wangu kama members tuwahamasishe wananchi kutokwenda kwenye vituo vya kupigia kura siku ya kupiga kura kwa sababu kuu tatu.

1: Wakuu wa mikoa , wakuu wa wilaya , wabunge na wakurugenzi wameambiwa wahakikishe katiba hiyo inapita kwa namna yoyote.

2: Nani atalinda kura zetu vituoni

3: CCM wana kawaida ya kulazimisha mambo kwa kupitisha vitu kwa nguvu huku wakidai kwamba yamepitishwa kwa maoni ya wengi hata kama si kweli.

Kwa hiyo kwa sababu hizo tatu ni afadhari kuwahamasisha wananchi wananchi kutokwenda kabisa kupiga kura kwa sababu wakienda watatumia mwanya huo kufanya maamuzi yasiyo sahihi huku wakidai wananchi wamepiga kura ya ndio kwa katiba hiyo.

Kwa mazingira hayo kwa upande wa bara ni vema kuwa ambia wananchi siku hiyo wasiende ila kwa upande wa Zanzibar waende tu mazingira yaliyopo kule ni ngumu kubadili matokeo ya hapana na kuwa ndiyo.
 
Mimi na wife hatuendi, mother dingi na madogo home hawaendi, shemeji zangu wote sita hawaendi, bado nahangaika na mama mkwe, huyu ni shida sana huyu mama. katiba yenyewe haielewi ila anasema lazima akapige kura.
 
naunga mkono hoja na nimeanza kutoa elimu bure kwa wananchi kuendelea na business zao siku ya kuipigia kura katiba hiyo ya sitta
 
Mimi na wife hatuendi, mother dingi na madogo home hawaendi, shemeji zangu wote sita hawaendi, bado nahangaika na mama mkwe, huyu ni shida sana huyu mama. katiba yenyewe haielewi ila anasema lazima akapige kura.

mkuu njia rahisi ficha kitambulisho chake na huumpe baada ya zoezi kukamilika
 
Kitambulisho chake aliisha ficha siku nyingi sana mkuu. hata kupiga kura anaenda na ma ccm wenzake haamini hata watoto wake wenyewe nasikia 2010 walimpigisha kwa lipumba akajua. hahaha
 
hiyo kali
 
Sasa kama hauendi kupiga kura, ni kura ipi unakwenda kuilinda?
 
Mimi na wife hatuendi, mother dingi na madogo home hawaendi, shemeji zangu wote sita hawaendi, bado nahangaika na mama mkwe, huyu ni shida sana huyu mama. katiba yenyewe haielewi ila anasema lazima akapige kura.
Mama mkwe wako anawazidi akili wote .
 
Kitambulisho chake aliisha ficha siku nyingi sana mkuu. hata kupiga kura anaenda na ma ccm wenzake haamini hata watoto wake wenyewe nasikia 2010 walimpigisha kwa lipumba akajua. hahaha
MICHADEMA hizo ndizo zenu, hamuwezi kushika dola kwa kuwalazimisha watu.
 
Mimi na wife hatuendi, mother dingi na madogo home hawaendi, shemeji zangu wote sita hawaendi, bado nahangaika na mama mkwe, huyu ni shida sana huyu mama. katiba yenyewe haielewi ila anasema lazima akapige kura.

Dah! Sangarara unanifurahishaga ktk post zako nyingi
 
Back
Top Bottom