Kati ya wanaJF wengi hapa, ni wewe unayenipa wakati mgumu kujua hasa unasimamia wapi; Tanzania au CCM.
Mfano mzuri ni mada hii.
Umeandika ukweli mtupu usioweza kupingwa kirahisi.
Ingekuwa ni CCM kama CCM yenyewe, pengine pangekuwepo na mategemeo kwamba pamoja na udhaifu walionao vyama vya upinzani wangeweza wakajitutumua na wananchi wakawaonea huruma kwa baadhi ya maeneo.
Lakini hapa sio CCM tena, ni mtu mwenye mabavu ambaye hata CCM yenyewe haifurukuti mbele yake. Na kutokana na vifaa alivyonavyo, hakuna yeyote atakayezuia lolote analotaka yeye lifanyike.
Wapinzani, sijui kama safari hii watapona.
Na ukifikiri kwa undani wake, pengine ni bora kutokuwepo na upinzani katika hali hii, maana utakuwa unatia tu matumaini yasiyokuwepo. Upinzani usiokuwa na uwezo wa kubadili chochote hapo hakuna upinzani tena.
Ni bora uondoke tujue letu moja tu! Kwamba tunae mtu anayejua kila jambo na anayejua mahitaji yetu yote ya maendeleo yanayotakiwa kuwepo ndani ya nchi hii. Mtu anayejua kwamba wananchi hawahitaji kuwa na haki ya kuchagua viongozi wao, ila yeye anajua viongozi wanaohitajiwa na wananchi.