Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Kama msingi wa elimu ya digrii ni kuajiriwa lazima tukae chini tuangalie ni wapi hasa katika jamii yetu ni muajibikaji wa ajira. Sekta ya uchumi lazima itupe majibu

Na iwe na uwezo wa kubeba watu wengi zaidi kila mwaka mana waafrika kwa kuzaana hatujambo. Any way Kuna marifa unatakiwa uyapate. Tafuta kitabu kimoja ameandika Adam jamrozik 1998
 
Kuliko kupoteza pesa, muda na nguvu kusoma degree ambayo mtaani kwa 90% haiwezi kuajirika, kwanini asijikite kujifunza ujuzi mahususi ambao elimu ya darasa la saba inatosha sana kuweza kuumudu na moja kwa moja aingie mtaani kupambana kuitumia.
 
Maisha ya watanzania wengi yamejengwa kwenye uchumi mdogo mdogo na Uchumi mdogo mdogo wa Tanzania kwa 80% sio rasmi, hauhitaji hata cheti, huo ndio tunapaswa tuongelee na kuupambania. Hatuna sababu ya kusaka degree ili kushinda hiyo vita, ni suala la Elimu ya darasa la saba mpaka fomu four, kisha moja kwa moja watu wakajifunze fani husika. Kama ni kilimo, basi tukutane shambani, kama ni biashara tukutane sokoni, kama ni ufundi basi tukutane kwenye karakana, vyuo pekee labda ni VETA tu.
 
Nadhani elimu ya ufundi hasa vyuo vya VETA vingeboreshwa zaidi kuanzia mitaala na aina ya wanafunzi.

Magari yameongezeka,ujenzi wa nyumba umekuwa mkubwa sana.Taifa linahitaji vijana wenye skills ufundi umeme,ujenzi,bomba,ufundi magari ya kisasa (utumiaji wa diagnosis) ili tuache kudanganya watu Dualis zinaungua kumbe mafundi wa chini ya Mwembe hawana ujuzi wa kuzitengeneza.

Hizi degree za Procurement,Accounting,Library,Banking,Geography,History ........ kazi zake ni chache sana.
 
Tatizo lipo katika mindset na sio degree
 
Do you know anything about social force?
 
Mimi nakuelewa mkuu, ni kweli kundi kubwa la wahitimu wengi wa degree hawana ajira na ukizingatia mitaala yetu imeshindwa kumuandaa mhitimu kujiajiri pia serikali bado haijaweka mazingira wezeshi kwa mtu kujiajiri na pia sekta binafsi kukua kwa ujumla.

Ajira za sasa kwa uchache wake kama huna connection inakuwa ngumu kupata ni wachache sana wanao zingatia ufaulu na uwezo wa mtu.
 
Hivyo tunarudi pale pale, kwa 90% hakuna tena ulazima wa watu kusoma mpaka chuo kikuu ili kupata degree. Ni kupoteza rasimali tu. Maana mwisho wa siku hupati ajira wala huwezi kutumia degree yako kutengeneza kipato.
Tatizo ni wenge la wazazi na vijana wenyewe, huwezi kuwaeleza kitu kwamba wasisome degree.......na hii yote ni kutaka wawe kama waliowatangulia bila kujua mambo huwa yanabadilika kuendana na nyakati.

Jambo jingine lilitokea wimbi hapo kati la kuua vyuo vya kati na kuvifanya kuwa vyuo vikuu na baada ya bodi ya mikopo kuanza kufadhili hadi kwenye vyuo binafsi mtifuano wa kuongeza idadi ya vyuo, kozi na idadi ya wanafunzi ukawa mkubwa.

Mimi naona serikali ingejikita kufadhili masomo ya degree kwenye vyuo vikuu vya umma kulingana na bajeti na uhitaji na kupanua zaidi elimu ya vyuo vya awali na kati (certicate, diploma, VETA).​
 
Kama kazi ni chache je, hizo digrii hazina maana?
 
Tatizo ni wenge la wazazi na vijana wenyewe, huwezi kuwaeleza kitu kwamba wasisome degree.......na hii yote ni kutaka wawe kama waliowatangulia bila kujua mambo huwa yanabadilika kuendana na nyakati.​
Mkuu mfano ukisema vijana waache wenge la kusoma degree je ndio solution naona vilevile tu kimsingi hakuna tofauti ya aliyesoma na asiyesoma endapo aliyesoma hakupata kazi so kutokwenda degree si solution mimi niliowaacha mtaani hadi sasa wote tuna maisha sawa tu hawana Steps zozote kiuchumi
 
Ukweli mtupu
mtaani kwa sasa hatujivunii digree bali kipato
 
sio kweli, ni uwezo mdogo tu wa kufikiria wa watu tuliowapa mamlaka ya kutuongoza.

Tanzania bado ni nchi masikini yenye opportunities nyingi ambazo zinahitaji hao watu, shida ni uwezo mdogo wa watu kutengeza fursa zitakazotanua uwanja na kutoa ajira nyingi.

Taifa lolote linalojengwa katika stage za mwanzo, halipaswi kuwa na shida ya ajira.
 
Tunarudi pale pale.
Kwa sasa Degree pekee kwa 90% ya wahitimu haina mchango wowote wa kukupa ajira au kipato.

Kumbe mtaani watu wanataka connection na ujuzi mahususi ili utoboe kwenye ajira, sio degree yako.
Degree inakupa knowledge Ila haikupi skills za kuitumia hiyo knowledge Ila kwa sasa kuna initiatives nyingi kama incubators ambazo zinawasaidia hawa vijana kuwa na vitu vyote viwili.. Ubaya hizi initiatives ni za hiyari na wengi hawazichukui

Kwanza tutoke huko kwenye kusubiria degree ikufanyie kitu badala ya wewe kuitumia ikufanikishie mambo yako. Degree haikutumii Ila wewe ndiye mwenye jukumu la kuitumia,

Kama ulichagua course flani for the wrong reasons na hukuweka plan ya kuitumia, usilaumu pale unapofeli maana kufaulu ni responsibility yako

Tunachoweza kulaumu ni hiyo job market kutokukua kiasi cha kuitegemea serikali kama muajiri mkuu, only that
 
Hongera mkuu,

Na ukweli ni kuwa skills hazihitaji GPA ndio maana nikawashauri watumie hiyo gap maana kampuni ikihitaji videographer, photographer au graphic designer, hawaangalii cheti bali portfolio ya kazi mtu alizowahi kuzifanya..na kama ni extremely corporate,wanaweza omba kujua kiingereza kama qualification

Ila pia kama mtu anaona course yake haimpi maslahi, hakuna gap lililo wazi kama sales kwenye makampuni makubwa

Uzuri hiyo ni game of numbers, anaeweza kuleta mapato mengi zaidi ndio anapata opportunities zaidi kwenye hizo kampuni.. Sema wengi huwa tunazidharau kwa sababu lazma uvuje jasho na damu hadi uwe good salesman unless iwe ni inborn character yako kuweza kushawishi watu kununua bidhaa na ile aggressiveness bhasi

Na hivyo ndivyo wakenya wametuzidi "wapo aggressive".

Hongera mkuu
 
Bomu limeshalipuka tayari....matapeli wa mtandao wengi ni graduates. We are slowly becoming a second Nigeria kwa idadi ya matapeli wasomi!
 
Hapa umemaliza kila kitu.
Umekuja na majibu kamili namna ya kukabiliana na hii hali.
Huo ushauri kuanzia serikali, taasisi na mtu mmoja mmoja tunapaswa kuufuata.

VETA, vyuo vya kati na elimu ya ufundi na stadi za maisha ndio mkombozi wetu wa hii hali ya sasa.

Vyuo vikuu tuviache kwa wataalamu wachache sana hususani watafiti.
 
Siyo kweli. Ukisoma literature kuhusu 'the work of the future' kuna msisitizo kwamba besides technical skills (na siyo without technical skills - ambazo mtu hupata wakati wa kusomea taaluma fulani) mfanyakazi anatakiwa awe na soft skills (employability, 21st century, transferable skills). Yaani waajiri wanataka mtu mwenye both types of skills kuliko mwenye aina moja tu.
 
Mimi siamini kama civil engineer atakosa cha kufanya, siamini kabisa.
Our Engineers are mostly administrators...sasa projects zinahitaji administrators wangapi...only a few ndiyo maana wapo na wanakosa ajira.

Fundi mwashi wa VETA au fundi mchundo mwenye FTC can easily get a job kuliko engineer.

Kosa lilifanyika kuua mfumo wa elimu wa tabaka la kati la watendaji: Diploma na FTC holders ambao ndiyo wanashinda na kulala sites...tumezalisha administrators wengi(degree holders) na sasa hatuna pa kuwapeleka.

Na hakuna miujiza wala maombi...we just need to go back, restructure and ensure we do the basics right!
 
Well said and ahsante sana mkuu jitihada,bidii,displine na kutokata tamaa hulipa daima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…