Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Naona ile dhana ya division na gpa inajifia yenyewe itabaki kusoma na kupata ujuzi tu hata usipopata ufaulu huo inatosha kwenda kujiajiri kwenye mambo yako. Hayo ma divisheni na gpa tuwaachie serikali wachague wafanyakazi wao sie wengine tunajijua wenyewe akili zetu namna ya kutengeneza uchumi.
 
Unachosema nikweli, ajira zimekua ngumu Sana kupatikana, nataman kama nchi ingejikita zaidi kwenye elimu ya vitendo Kwa zaidi ya 70%.
Hakuna cha elimu ya vitendo wala nini ,suala ni kwamba ajira hamna na mitaji na mazingira ni mabovu kitaani kwa hao wahitimu kujiajiri kupitia fani zao .
Mbona kuna lundo la watu wana certificates na diploma zao za technical courses na bado hawana ajira na hawajaweza kujiajiri ?
Hili suala watu wasioelewa uhalisia ndio wataishia kuponda tu ukosefu wa ajira kwa hao wa degree ,
Hao wa diploma na certificates nao mbona wako wanaranda randa kitaa kama machokoraa ?
Uchumi duni wa nchi na fursa kuwa duni ,result ndio hicho mnachokiona
Na hali itaendelea kuwa mbaya tu
 

Big four Auditing firms zenyewe siku hizi zinakwepa kuajiri graduates wenye degree za accounts.

Zinaajiri graduates wenye degree za engineering ama acturial science. Kisha kazini wanaenda msomesha ACCA na CPA.

Wanadai watu wanaojua hesabu ngumu ( advance mathematics) ndio wana attention to small details kwenye kazi zao za audit.

kuajiri wenye degree za accounts ni ujinga huku engineers wanaweza kufanya kazi za accounts kwa ubora zaidi wakielekezwa siku chache tu
 
Ungekuwa mhitimu wa fani yoyote ya uhandisi ungeamini vizuri mbona ?
Ungekula msoto na kupata first hand experience soon baada ya kugraduate
Hali ni mbaya kwa fani zote ,ni kama soko la ajira lipo kwenye" standstill "mode
Mimi ni mhandisi wa fani moja wapo ya uhandisi ,ila ninafanya issue tofauti kabisa na fani yangu
 
Maarifa yasiyo na mtaji ni sawa na kazi bure.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kumbe basi tusilaumu mfumo wa elimu yetu. Kuna tatizo zaidi ya mfumo wa elimu.

Binafsi nadhani ni siasa mbovu na uongozi wa hovyo ndivyo vinavyopelekea ajira kukosekana katika taifa letu lenye baraka tele.

Hakuna sera na mipango inayotabirika na kufanya taasisi za fedha, wawekezaji na vyuo kushindwa kuandaa programu na mipango ya kifedha kulingana na mwelekeo wa kisera na mipango ya serikali.

Kila awamu inakuja na mipango yake"kilimo kwanza, Tanzania ya viwanda, Royal tour",
 
Kumbe hadi mainjinia wanakosa kazi?
 
Kama huna industrial base / sekta ya viwanda na technology iliyokomaa ,hicho unachoandika na kudhani ndio solution ni kazi bure .
Supply and demand ,hii mizania ndio wengi mmeshindwa kuelewa , hamna sekta wala uchumi komavu na demand ya kubeba hao mafundi na technicians nchi hii ,hata leo hii vyuo vyote vya degree vifutwe na hao wanafunzi wapelekwe veta na technical colleges ni kazi bure .
Supply should be in line with the demand
 
Alaf unakakuta haka kajamaa kanasubiri mshahara laki 6 mwisho wa mwezi.
 
20. Mineral processing engr
21. Bachelor of art with education
22. Fine art and design
23. Statistics
24.Mathematics
25.Physics
26. Civil engr
27. Chemistry
28. Agroeconomy
29. Biochemistry
30. French
31. Arabic
32.
33.
34.

Hapo kwenye civil eng nakataa. Niko kwenye hiyo game for long time bado zinauhitaj but lazima ujue sector ipi inauhitaj currently

Ila hizo zingine Mungu saidia aisee ni vilio
 
Sasa braza au sisita,kumbuka nyingine za mchongo.
-enzi hizo wazazi wa leo walikuwa wakisoma kweli kweli. Humu tu kwenyewe ukiangalia waliokula matunda kimasihala,ni wanachuo, na walikuwa wanakula wenzao humo humo. Eti baada ya hapo,ikawa ndo kila nikitaka najilia vyangu. Na mwenzie ndo hivo hivo akitakwa analiwa. Hao wanachuo au wanandoa? Wanawaza tu kugegedana,masomo saa ngapi?

-Elimu na maadili vinaenda sambamba. Wakati mwingine unakuta muajiri na yeye anaangalia na chuo chenyewe. Mkisema Mabibo Hostel wanaliwa kwa buku 2, mwajiri unategemea atachukuliaje hicho chuo?

-Unaenda kutafuta kazi umevaa mlegezo, mwingine mikucha ya bandia unategemea nini? Unaanza kuomba kazi, Boss mtarajiwa anaanza kutongoza. Ulivyoingia, ndo hivo hivo utakavyopokelewa.

-Mwenzenu katokea Kigoma huko Kasuru,tena siyo Kigoma mjini,akimaliza anarudi kwao. Kwenye ajira ni miji mikubwa. Haijui huenda na nauli hupata kwa shida.
Wakienda Dar kwa ndugu zao, ndo hao mnawavizia stendi na kuwagegeda,wanaondoka na mimba. Wanaofanya hivyo,utasikia toka siku hio hata namba hatukupeana. Huyu akishakuwa na msongo wa mawazo au kurudishwa alikotoka,ile degree haina msaada tena.

Kwenye maarifa ya kipato,na kwenyewe changamoto.
Hakuna kazi isiyolipa. Lakini,unawaza,mi na elimu yangu nikawe konda kwenye basi la mikoani? Je,nikikutana na Asha nilokuwa namuaminisha kwamba mi nikimaliza kazi ipo ni uhakika?
Vitu kama hivyo. Au mbona kazi hii haina hadhi ya elimu yangu? Changamoto zinakua nyingi. Sema tu labda yangeongezwa masomo practical,na wahitimu wakaweza kupata hata mikopo kuendesha biashara zao kwa watakaokosa ajira,lakini wakawa na uhakika wa soko.
Hayo ni badhi,ila mambo ni mengi. Af cha ajabu,unakuta kuna watu wengine wapo hata nje,wanazijua fursa lakini hawastui wenzao. Wengine hawajui wawapate wapi.
 
Taasisi haziajiri wenye uzoefu bali wenye connection.
 
Yale yale mkuu. Boss akishakuchungulia, ujue umeisha. Usipokubali,kazi huna. Ukikubali, hukai mda mrefu. Ukishaliwa tu,utajiona unawazidi wenzako. Akimtaka mwenzio,anakula, kuepuka lawama,unapumzishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…