Ukweli usemwe na usemwe wazi ili kila mtu aujue. Wigo wa watanzania kusoma mpaka chuo kikuu ili kupata degree umekuwa mkubwa lakini huo mfumo umekuwa ni hasara na upotevu wa rasimali (muda, pesa na nguvu) kwa 90%.
Ajira mtaani kwa 90% hakuna kwa fani nyingi, ni sawa na kucheza kamili, na elimu ya vyeti vya chuo kikuu haina mchango wowote wa mhitimu wa level ya degree kuweza kujiajiri moja kwa moja. Hapa chini ni baadhi ya fani zinazoangukia kwenye kundi hilo.
1. Public administration
2. Political science
3. Business administration
4. Procurement and supply
5. Human resource
6. Sociology
7. Environment
8. Language
9. Mass communication
10. Tourism
11. Banking
12. Accounting
13. Economy
14. Finance
15. History
16. Insurance
17. Tax
18. Cooperative
19. Marketing
20.
Kama wewe ni mhitimu wa hizo fani kwa miaka ya karibuni utaelewa hicho nilichokiandika, na kama wewe ni mwanafunzi wa hizo fani anza kujiandaa kisaikolojia, hali ni mbaya mtaani. Wahitimu ni wengi na hawana ajira yoyote, wamechoka vibaya, wameshazunguka na mabahasha mpaka soli za viatu kuchakaa, wamejitolea mpaka basi, wameshikiza mpaka wamedondoka na wengi wamekata tamaa kabisa, vyeti vyao wamesahau hata vipo wapi, havina msaada. Bado wanakula, kulala na kutunzwa na wazazi wao, mashemeji au wajomba. Wengine wameamua kujiajiri katika fani zingine ambazo hazina uhusiano wowote wa fani walizosomea na zenye kuhitaji elimu ya darasa la nne tu.
Wajanja wengine wameamua kurudi chuo, hususani kwa ngazi ya Diploma kusoma fani za ualimu au afya ili kuingia kwenye mkondo wa kuja kupata ajira hapo baadaye.
Jamani hali ni mbaya na tete.
Ukweli usemwe!
Sasa braza au sisita,kumbuka nyingine za mchongo.
-enzi hizo wazazi wa leo walikuwa wakisoma kweli kweli. Humu tu kwenyewe ukiangalia waliokula matunda kimasihala,ni wanachuo, na walikuwa wanakula wenzao humo humo. Eti baada ya hapo,ikawa ndo kila nikitaka najilia vyangu. Na mwenzie ndo hivo hivo akitakwa analiwa. Hao wanachuo au wanandoa? Wanawaza tu kugegedana,masomo saa ngapi?
-Elimu na maadili vinaenda sambamba. Wakati mwingine unakuta muajiri na yeye anaangalia na chuo chenyewe. Mkisema Mabibo Hostel wanaliwa kwa buku 2, mwajiri unategemea atachukuliaje hicho chuo?
-Unaenda kutafuta kazi umevaa mlegezo, mwingine mikucha ya bandia unategemea nini? Unaanza kuomba kazi, Boss mtarajiwa anaanza kutongoza. Ulivyoingia, ndo hivo hivo utakavyopokelewa.
-Mwenzenu katokea Kigoma huko Kasuru,tena siyo Kigoma mjini,akimaliza anarudi kwao. Kwenye ajira ni miji mikubwa. Haijui huenda na nauli hupata kwa shida.
Wakienda Dar kwa ndugu zao, ndo hao mnawavizia stendi na kuwagegeda,wanaondoka na mimba. Wanaofanya hivyo,utasikia toka siku hio hata namba hatukupeana. Huyu akishakuwa na msongo wa mawazo au kurudishwa alikotoka,ile degree haina msaada tena.
Kwenye maarifa ya kipato,na kwenyewe changamoto.
Hakuna kazi isiyolipa. Lakini,unawaza,mi na elimu yangu nikawe konda kwenye basi la mikoani? Je,nikikutana na Asha nilokuwa namuaminisha kwamba mi nikimaliza kazi ipo ni uhakika?
Vitu kama hivyo. Au mbona kazi hii haina hadhi ya elimu yangu? Changamoto zinakua nyingi. Sema tu labda yangeongezwa masomo practical,na wahitimu wakaweza kupata hata mikopo kuendesha biashara zao kwa watakaokosa ajira,lakini wakawa na uhakika wa soko.
Hayo ni badhi,ila mambo ni mengi. Af cha ajabu,unakuta kuna watu wengine wapo hata nje,wanazijua fursa lakini hawastui wenzao. Wengine hawajui wawapate wapi.