Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Unachokisema nakubaliana nacho upando mmoja na mwingine nakataa, kuwa na elimu ya vitendo nijambo moja nakujua kazi nijambo lingine.. Kama unauzoefu wakazi na unajua vizuri kazi hutokosa kibarua Cha kukupa fedha zakujikimu huku ukiwa unaendelea na kutafuta furusa Bora zaidi. Hao unaosema wanaelimu za vitendo za Makaratasi nasio uhalisia wa vitendo.

Watu wengi wanaofanya kazi za ufundi asilimia 90, hawana elimu ya veta, au diploma, jiulize nafundi wengi wa electronics mtaan Kwa nn hawajaenda shule, au mafundi wa garage au welders, electrician, plumbing, painting na kadhalika wengi niwamejifunzia kazi mtaani nasio shule. Sasa chakujiuliza zaidi Hawa waliojifunzia shule wako wapii?.
 
Kazi za darasa la Saba ni zipi mkuu
Kwa uchache sana, kazi ambazo elimu ya darasa la saba inatosha kabisa kuzifanya ni hizi hapa;
1. Udereva (boda boda, bajaj, taxi, daladala)
2. Kuosha vyombo vya moto (car washer)
3. Umama/ubaba lishe
4. Kuuza duka
5. Kazi za saloon (kunyoa, kusuka)
6. Kuuza vinywaji (Glocery, bar)
7. Udalali
8. Kulima
9. Umachinga
10. Ufugaji
11. Saidia fundi
12. Vibarua wa ujenzi
13. Kuuza matunda na mboga mboga
14. Utunzaji nyumba (House girl, House boy)
15. Vibarua viwandani
16. Vibarua wa maduka ya wahindi
17. Kazi za ulinzi
18. Kuchezesha play stations
19. Kuonyesha mpira kwenye vibanda umiza
20. Kubeba mizigo (ubagazi)
21. Udobi
22. Uwakala wa pesa (tigo pesa, M-Pesa etc)
23. Kukaanga chips na mishikaki
24. Kuuza nyama kwenye mabucha
25. Kupiga debe
26. Utingo wa mabasi na malori
27. Kucheza show (dancer)
28. Ufundi nguo
29. Ufundi viatu
30. Kuuza nguo, mitumba
 
Enzi nasoma udsm B.A Education nilikua na masomo ya Linguistics & Literature. Kuna washikaji zangu nilikua na share nao course za linguistics wao wakisoma B.A Language studies, nilikua najiuliza hawa jamaa kwa nini wasisome tu education wakatembea tu na masomo ya Linguistics & Literature na ajira ni uhakika mbona ni kitu kile kile na ninachosoma mm. Sasa miaka imeenda utakuka mwingine yuko anapgwa tu maisha shida amezitaka mwenyewe.
 
Pole mkuu.
 
Book keepers watahitajika zaidi
Nani anawahitaji tena kwa wingi wao?
Kwa mshahara upi mtu awalipe?

Embu waza tu, ikiwa kwa miaka zaidi ya kumi mfululizo, kila mwaka kuna zaidi ya wahitimu elfu kumi wa accounting wanaingia mtaani kusaka ajira za kuunga unga, ni vipi soko la ajira linaweza kuwabeba hata kama lingekuwa linawahitaji?
 
Halafu kwa kujidanganya na kujitia moyo huenda hao jamaa kipindi hicho walikuwa wanasema, kozi yao ni multipurpose&wide hivyo watakuwa na uwanja mpana wa kuajiriwa popote ikiwemo kwenye ualimu! Sasa baada ya kuhitimu wako hoi, ajira hakuna na kipato hakuna.

Chuoni watu wanadanganywa na kudanganyana sana.
 
Degree ni usenge,
Miaka hiyo tunasoma unaambiwa eti ukisoma combination ya Maths na Physics utakuwa rubani. Jamani,waalimu wengine walaaniwe tu. Unaimbishwa vitu visivyo na kichwa wala miguu, basi lenyewe unalipanda kwa nadra,eti utaendesha ndege. Wengine ohhh hii ukimaliza tu,ajira za kumwaga. Daadeki,ukirudi mtaani wauza gongo wanakucheka, wewe unakalia kufua na kunyoosha kwa pasi ya mkaa, mpaka kiatu kina pinda eti unasikilizia.
Msala unaanza pale wazazi wanapokuambia hao mbuzi wakachungwe kuanzia saa kumi,mara unatakiwa ukatafute kazi uwe unajinunulia sabuni
 
Mbona hujasema mishahara? Biashara zenyewe hazieleweki unatamani na ulionao waende tu home. Hao hao,ukipiga hesabu ya gharama zake kusoma, unajikuta unahitaji vijana wa kulipa tu laki moja. Huyo utamwambia mshahara laki au laki na nusu?
 
Hakika kabisa.
Tuliwazishwa mambo ya uongo mtupu.
Kwa jinsi nilivyoaminishwa kuhusu kusoma masomo fulani ili kuja kuwa rubani halafu mpaka leo hii sijawahi kuona rubani ninayemfahamu au kuona mshikaji ninaye mfahamu ambaye alisoma hayo masomo mpaka kufikia kuwa rubani.

After all, unajiuliza hapa Tz kuna ndege ngapi kiasi kila mtu aaminishwe akasome ili aje kuwa rubani.
 
Degree ni usenge, watoto wengi wa masikini wamewekewa complications za kusoma miaka mingi 2/7/4/2 akimaliza aendelee tena miaka 3 au 4 au 5 muda wote huo watu wanasoma kimasikini na tabu tupu ni usenge tu
 
Kwaiyo mwenye degree Hana sifa ya kufanya hizo kazi
 
Sasa kuna watu ukiwaambia hayo watakwambia wewe ni mzembe, hajajitambua nk ndio maana hujatoboa kwenye ajira kwa kile ulichosomea. Bado hawajajua maisha ni nini.

Mimi huwa nawaambia, waende wasome, wakishahitimu tutakutana mtaani ndio tuongee ukweli.
 
Utakuwa kilaza kwelikweli wewe, You lack exposure or wewe ni mpumbavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…