Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Kwaiyo mwenye degree Hana sifa ya kufanya hizo kazi
Nimesema huhitaji kuwa na degree ili uweze kuzifanya hizo kazi za elimu ya darasa la Saba. Ukiona mtu mwenye degree anazifanya hizo kazi basi ujue degree yake imeshindwa kumpa ajira na kipato alichokitarajia, hivyo ameitupa kabatini na kuishi bila degree ili maisha yaende.
 
Hakika kabisa.
Tuliwazishwa mambo ya uongo mtupu.
Kwa jinsi nilivyoaminishwa kuhusu kusoma masomo fulani ili kuja kuwa rubani halafu mpaka leo hii sijawahi kuona rubani ninayemfahamu au kuona mshikaji ninaye mfahamu ambaye alisoma hayo masomo mpaka kufikia kuwa rubani.

After all, unajiuliza hapa Tz kuna ndege ngapi kiasi kila mtu aaminishwe akasome ili aje kuwa rubani.
Ndo maana hatufai kumlaum mtu. Mwalimu anaekufundisha hizo Maths na Physics,mwenyewe ukute hata Airport hajawahi kuiona. Huyo huyo,ndo anaekuaminisha kuwa unaenda kuwa rubani miaka 6 au kumi badae. Akili ya kujiuluza kwa nini yeye hajaenda kuwa rubani,ndo zero. Unategemea nini?
Sasa mwisho wa siku unaamua usepe kijijini ukawaache walime, vijana wanajenga,wanaoa,unabaki mjini kuwa tapeli
 
Utakuwa kilaza kwelikweli wewe, You lack exposure or wewe ni mpumbavu
Lakini mkuu,huna haja ya ugomvi. Sasa unataka aamini unachokiamini wewe? Hapana. Huenda ametoboa kimaisha na hiyo elimu hana. Utamuaminisha kwamba bila elimu maisha huwezi?
Na wewe kama umetoboa kwa elimu,hakika unaamini bila elimu kutoboa ni ngumu
 
Utakuwa kilaza kwelikweli wewe, You lack exposure or wewe ni mpumbavu
Sawa mimi ni kilaza, tena kilaza kweli kweli!
Lakini wewe tambua tu, mimi ni mjumbe wa 'vilaza' ambao tuko mtaani tukiwa na degree zetu bila ajira au kipato cha kuzitegemea hizo degree. Ni kundi la 'vilaza' lenye kubeba 90% ya wahitimu wa degree wa sasa.
 
Ukweli usemwe na usemwe wazi ili kila mtu aujue. Wigo wa watanzania kusoma mpaka chuo kikuu ili kupata degree umekuwa mkubwa lakini huo mfumo umekuwa ni hasara na upotevu wa rasimali (muda, pesa na nguvu) kwa 90%.

Ajira mtaani kwa 90% hakuna kwa fani nyingi, ni sawa na kucheza kamili, na elimu ya vyeti vya chuo kikuu haina mchango wowote wa mhitimu wa level ya degree kuweza kujiajiri moja kwa moja. Hapa chini ni baadhi ya fani zinazoangukia kwenye kundi hilo.

1. Public administration
2. Political science
3. Business administration
4. Procurement and supply
5. Human resource
6. Sociology
7. Environment
8. Language
9. Mass communication
10. Tourism
11. Banking
12. Accounting
13. Economy
14. Finance
15. History
16. Insurance
17. Tax
18. Cooperative
19. Marketing
20.

Kama wewe ni mhitimu wa hizo fani kwa miaka ya karibuni utaelewa hicho nilichokiandika, na kama wewe ni mwanafunzi wa hizo fani anza kujiandaa kisaikolojia, hali ni mbaya mtaani. Wahitimu ni wengi na hawana ajira yoyote, wamechoka vibaya, wameshazunguka na mabahasha mpaka soli za viatu kuchakaa, wamejitolea mpaka basi, wameshikiza mpaka wamedondoka na wengi wamekata tamaa kabisa, vyeti vyao wamesahau hata vipo wapi, havina msaada. Bado wanakula, kulala na kutunzwa na wazazi wao, mashemeji au wajomba. Wengine wameamua kujiajiri katika fani zingine ambazo hazina uhusiano wowote wa fani walizosomea na zenye kuhitaji elimu ya darasa la nne tu.
Wajanja wengine wameamua kurudi chuo, hususani kwa ngazi ya Diploma kusoma fani za ualimu au afya ili kuingia kwenye mkondo wa kuja kupata ajira hapo baadaye.

Jamani hali ni mbaya na tete.
Ukweli usemwe!
Watoto wa maskini hawasomagi hizo course. ..i
 
Degree ni usenge, watoto wengi wa masikini wamewekewa complications za kusoma miaka mingi 2/7/4/2 akimaliza aendelee tena miaka 3 au 4 au 5 muda wote huo watu wanasoma kimasikini na tabu tupu ni usenge tu
 
Mkuu hakuna degree nzuri au mbaya. Hata medicine wapo kitaa wanaendesha bodaboda.

Tatizo kubwa in lipo kwenye mtazamo (mindset) wa wasomi. Wengi mmejengwa na kuandaliwa kupewa ajira. Hapa ndipo penye kosa kubwa.

Lengo la degree siyo kuajiriwa kwenye fani uliyosomea kama mleta mada unavyotaka kutuaminisha. Lengo la degree ni kupanua mawanda ya kufikiri ili msomi aweze kuyakabili mazingira yake kwa namna toauti na asiyesoma.

Kwahiyo ktk nchi kama Tanzania iliyobarikiwa ardhi kubwa yenye rutuba na imezungukwa na mito, maziwa na bahati ni aibu kwa wasomi kuleta mada za kulalamikikia kukosa kuajiriwa. Mlienda chuo kudanga, kubet na kuvuta shisha badala ya kujielimisha. Shubamiti, ndengeleki ninyi!
Hilo ni tatizo la msomi !?
 
Tunarudi pale pale.
Kwa sasa Degree pekee kwa 90% ya wahitimu haina mchango wowote wa kukupa ajira au kipato.

Kumbe mtaani watu wanataka connection na ujuzi mahususi ili utoboe kwenye ajira, sio degree yako.
Hiki kitu kinanifikirisha sana kwa hawa watoto wetu wadogo.... Bila mabadiliko yoyote kwa mwendo huu Huko baadae hali itakuwa mbaya zaidi mara dufu.
 
Halafu kwa kujidanganya na kujitia moyo huenda hao jamaa kipindi hicho walikuwa wanasema, kozi yao ni multipurpose&wide hivyo watakuwa na uwanja mpana wa kuajiriwa popote ikiwemo kwenye ualimu! Sasa baada ya kuhitimu wako hoi, ajira hakuna na kipato hakuna.

Chuoni watu wanadanganywa na kudanganyana sana.
Mi nakumbuka Advance yote nasoma kichwani kwangu nipate one nikasome udsm sheria.... Baadae six nimemaliza na nina one, kuchekecha akili nikaona law haina ajira useng tu bora nisome education uhakika wa ajira mbeleni ntajua cha kufanya. Ningesoma miaka ya kizazi hiki huenda ningeenda veta maana kusomea ualimu nao pia ni usenge maana hamna ajira.
 
Hivi mfano wa karibu. Watu wanaopelekwa Israel,kujifunza mambo ya kilimo,
1. Hawa watu hawaendi tu hivi hivi. Wanalipwa.
2. Watu hawa hawa, ukija kuangalia,si kwamba kuna vigezo vya kwenda huko,bali connection tu. Ndugu yangu akaonje hela ya serikali.
3. Wakirudi, nani anajua wanakopotelea?
4. Sasa kama wamepelekwa kujiendeleza, af hawana mchango wowote, unategemea huyu huyu ambaye hajafika hata Dar atadai ana uwezo wa kuendelea kilimo?
5. Kwa nini hao wa Israel wasiletwe wakawafikie wenye uhitaji?
6. Ikiwa mifumo ya kiAfrika bado ya kimagumashi,ni ngumu sana.
7. Leo hii Israel inadai inahitaji nguvu kazi kutoka Afrika. Hasa kwenye sekta ya kilimo. Wanalima wakauze nje.
Ni kwamba hayo masoko wanayouza,hayapokei mazao kutoka Afrika?
Je, Israel ina ardhi kubwa na nzuli kuliko ya TZ?
Mfumo wa maisha ndo ulivyo bila kushikana mkono, ni ngumu. Sasa wenye nafasi za kuwapa maisha vijana, wasipotaka, miaka ijayo mtakuta vibaka ni wasomi. Sasa hivi wanaojiuza si wasomi?
 
Ukweli usemwe na usemwe wazi ili kila mtu aujue. Wigo wa watanzania kusoma mpaka chuo kikuu ili kupata degree umekuwa mkubwa lakini huo mfumo umekuwa ni hasara na upotevu wa rasimali (muda, pesa na nguvu) kwa 90%.

Ajira mtaani kwa 90% hakuna kwa fani nyingi, ni sawa na kucheza kamili, na elimu ya vyeti vya chuo kikuu haina mchango wowote wa mhitimu wa level ya degree kuweza kujiajiri moja kwa moja. Hapa chini ni baadhi ya fani zinazoangukia kwenye kundi hilo.

1. Public administration
2. Political science
3. Business administration
4. Procurement and supply
5. Human resource
6. Sociology
7. Environment
8. Language
9. Mass communication
10. Tourism
11. Banking
12. Accounting
13. Economy
14. Finance
15. History
16. Insurance
17. Tax
18. Cooperative
19. Marketing
20.

Kama wewe ni mhitimu wa hizo fani kwa miaka ya karibuni utaelewa hicho nilichokiandika, na kama wewe ni mwanafunzi wa hizo fani anza kujiandaa kisaikolojia, hali ni mbaya mtaani. Wahitimu ni wengi na hawana ajira yoyote, wamechoka vibaya, wameshazunguka na mabahasha mpaka soli za viatu kuchakaa, wamejitolea mpaka basi, wameshikiza mpaka wamedondoka na wengi wamekata tamaa kabisa, vyeti vyao wamesahau hata vipo wapi, havina msaada. Bado wanakula, kulala na kutunzwa na wazazi wao, mashemeji au wajomba. Wengine wameamua kujiajiri katika fani zingine ambazo hazina uhusiano wowote wa fani walizosomea na zenye kuhitaji elimu ya darasa la nne tu.
Wajanja wengine wameamua kurudi chuo, hususani kwa ngazi ya Diploma kusoma fani za ualimu au afya ili kuingia kwenye mkondo wa kuja kupata ajira hapo baadaye.

Jamani hali ni mbaya na tete.
Ukweli usemwe!
Fani zipi ndo uhakika mkuu?
Maana tuna walim,famasia huku mtaani pia sijawaona hapo?
 
Hivyo tunarudi pale pale, kwa 90% hakuna tena ulazima wa watu kusoma mpaka chuo kikuu ili kupata degree. Ni kupoteza rasimali tu. Maana mwisho wa siku hupati ajira wala huwezi kutumia degree yako kutengeneza kipato.
Kupoteza muda, pesa
Najuta kabisa Bora waliodisco wakatafuta maisha mengine
 
Back
Top Bottom