MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
CHADEMA wako wapi? Wao ndo huwa viherehere kusema Kenya wanatuzidi kila kitu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanatumikishwa sana Uarabuni kufanya kazi za ndani yani wao na waphillipino ndiyo wamejaa sana Uarabuni wakitesawa.Si wanasemaga vijana wakenya wanajituma sana sio Kama sisi watz
Upigaji wa Kenya sio poa. Tanzania kwa upigaji bado chipukizi sanaHuenda wamejifunza upigaji kutoka Tz.
Siku hizi siwasikii tena na kale kamsemo kao wanakokapenda eti tuige ya wakenya.CHADEMA wako wapi? Wao ndo huwa viherehere kusema Kenya wanatuzidi kila kitu.
Wakenya wana maisha magumu sana. Ukitokea Namanga kwenda Nairobi njia nzima kunanuka ufukara ukitazama nyumba zao ambazo nyingi ni za mabati. Ukipita Kitengela ndo unaanza kuona unafuu wakati unaingia town. Huko town kwenyewe kuna magorofa mengi ya watu wachache wanazopangisha apartments. Mkenya wa kawaida kujenga nyumba ni shughuli pevu.Siku hizi siwasikii tena na kale kamsemo kao wanakokapenda eti tuige ya wakenya.
Nilishawahi sema hata ikitokea CHADEMA wameingia madarakani bado kitaendelea kuwa chama kikuu cha upinzani kwasababu hawana uwezo wa kuongoza nchi. Wataendelea kulaumu CCM. Kama ilivyo kwa Ruto hata Zambia Hichilema huwa anawalaumu chama kilichokuwa madarakani na tayari kafeli mambo mengi. Ikitokea hiyo hali basi CCM kitakuwa chama tawala nje ya serikali.Siku hizi siwasikii tena na kale kamsemo kao wanakokapenda eti tuige ya wakenya.
Mkuu usifurahie jirani yako anapougua.Mficha maradhi kifo kitamuumbua, yawahi hayawi sasa yamekuwa, ukweli halisi umeanza kujionyesha huko Kenya, hali ya maisha ni mbaya mnoo, vijijini ukame unawaua, mijijini maisha yanawanyonga na sasa Serikali imeshindwa kulipa hadi mishahara watumishi wake. Kenya kumechoka na kuchakaa balaa.
Rais wa Kenya (William Ruto) amekiri wazi wazi kuwa hali ya kiuchumi kwa wakenya na serikali yao ni tete mnoo, huku akisema serikali yake imezidiwa na madeni yaliyotokana na kukopa kiholela ili kugharamia miradi iliyojaa ufisadi mkubwa kiasi cha kushindwa kuwa na pesa za kulipa mishahara.
Sio hayo tu, zipo sehemu kadhaa (kaunti nyingi) katika Kenya ambapo mbali na kutokuweza kupokea pesa za kulipa mishahara kwa miezi kadhaa pia zimeshindwa kupokea pesa kwa ajili ya kugharamia utoaji wa huduma za Afya na elimu kutoka serikalini. Kwa lugha rahisi na fupi sana, Kenya kwa sasa ni taifa rasmi la kimaskini zaidi katika ukanda wa Afrika mashariki na kati.
Kwa hali ilivyo sasa ni dhihaka kubwa sana kutaka kuilinganisha Kenya na Tanzania, kwa kuwa Tanzania mbali na kuwa kihistoria ni nchi yenye mizizi ya kimaskini (ujamaa!) na tangu kumfukuza mkoloni imekuwa chini ya CCM (chama kinachoukumbatia umaskini) bado haijaweza kupitia vipindi vya umaskini na kufirisika kwa serikali kiasi cha kushindwa kulipa mishahara ya watumishi wake. Kwa sasa kimaskini Kenya imepitiliza.
Kama hali hii ikiendelea kwa muda mrefu kidogo kuna kila dalili kuwa huenda Kenya ikaweka rehani bandari ya Mombasa, viwanja vya ndege na mtandao wa reli ya SGR ili kulipa madeni au kuendelea kukopesheka.
Tanzania ujiandae na hiyo hali muda si mrefuMficha maradhi kifo kitamuumbua, yawahi hayawi sasa yamekuwa, ukweli halisi umeanza kujionyesha huko Kenya, hali ya maisha ni mbaya mnoo, vijijini ukame unawaua, mijijini maisha yanawanyonga na sasa Serikali imeshindwa kulipa hadi mishahara watumishi wake. Kenya kumechoka na kuchakaa balaa.
Rais wa Kenya (William Ruto) amekiri wazi wazi kuwa hali ya kiuchumi kwa wakenya na serikali yao ni tete mnoo, huku akisema serikali yake imezidiwa na madeni yaliyotokana na kukopa kiholela ili kugharamia miradi iliyojaa ufisadi mkubwa kiasi cha kushindwa kuwa na pesa za kulipa mishahara.
Sio hayo tu, zipo sehemu kadhaa (kaunti nyingi) katika Kenya ambapo mbali na kutokuweza kupokea pesa za kulipa mishahara kwa miezi kadhaa pia zimeshindwa kupokea pesa kwa ajili ya kugharamia utoaji wa huduma za Afya na elimu kutoka serikalini. Kwa lugha rahisi na fupi sana, Kenya kwa sasa ni taifa rasmi la kimaskini zaidi katika ukanda wa Afrika mashariki na kati.
Kwa hali ilivyo sasa ni dhihaka kubwa sana kutaka kuilinganisha Kenya na Tanzania, kwa kuwa Tanzania mbali na kuwa kihistoria ni nchi yenye mizizi ya kimaskini (ujamaa!) na tangu kumfukuza mkoloni imekuwa chini ya CCM (chama kinachoukumbatia umaskini) bado haijaweza kupitia vipindi vya umaskini na kufirisika kwa serikali kiasi cha kushindwa kulipa mishahara ya watumishi wake. Kwa sasa kimaskini Kenya imepitiliza.
Kama hali hii ikiendelea kwa muda mrefu kidogo kuna kila dalili kuwa huenda Kenya ikaweka rehani bandari ya Mombasa, viwanja vya ndege na mtandao wa reli ya SGR ili kulipa madeni au kuendelea kukopesheka.
Waache wakenue tu ,hii global financial crisis itaexpose kila serikali yenye uvundo , Tanzania soon itaingia huko , kama Nigeria ,Ghana ,Kenya wote hao wana uchumi mkubwa Africa Ila Mbinyo wa uchumi unawanyoosha hii serikali ya Tanzania inayokopa kila siku IMF ili kujiendesha ndio inawapa matumaini na nguvu ya kucheka Kenya ?Tanzania ujiandae na hiyo hali muda si mrefu
Ufisadi kwenye Miradi na ukopaji n wa kiwango cha juu
Mikopo yetu inaenda kwenye uwekezaji wenye tija na inayoinua uchumi unlike Kenya ambapo mikopo huelekezwa kwe uwekezaji usio na tija na pia nusu ya hela ya mikopo inapotea kwa upigaji na pilferageWaache wakenue tu ,hii global financial crisis itaexpose kila serikali yenye uvundo , Tanzania soon itaingia huko , kama Nigeria ,Ghana ,Kenya wote hao wana uchumi mkubwa Africa Ila Mbinyo wa uchumi unawanyoosha hii serikali ya Tanzania inayokopa kila siku IMF ili kujiendesha ndio inawapa matumaini na nguvu ya kucheka Kenya ?
Laiti ningejua yanayokuja ndani ya miezi michache ijayo mngelia sana na kupata kichaa kabisa
Sio kweliWakenya wanajituma kulima na kuuza mirungi, kunywa chang'aa na kupiga siasa za kikabila. Hivyo vitu ni kweli wametuzidi sana, vingine tupo tu sawa, tofauti hakuna.
Huo ndio ukweli, Kenya ni miongoni mwa nchi za hovyo zaidi hapa Afrika kwa SasaSio kweli